Hizo Dhahabu zinazo chimbwa Geita na kwingineko kanda ya Ziwa, mbona bado Umasikini uko juu sana?

 
Nadhani wakazi wa asilia wa Geita ni masikini kuliko watu wote duniani wanaoishi maeneo ya machimbo. Angalia nyumba wanazoishi ni duni, ukiwa barabara kuu huwezi kuona ila ukiingia ndani walau nusu kilometa ndo utajionea makazi duni kabisa ya wananchi wa Geita.
 
Hunufaisha wachache
 
Ccm wanavyohusudu madini sasa utadhani waako marekani.

Inonekana wanafaidika wao
 
Acha uongo pesa hazijifichi sehemu zilipo
 
Bado ni masikini Kwa sababu ya mfumo wa ugawanyaji mapato ya nchi.pesa inayopatikana huko hupelekwa dar esalaamu na majiji mengine kujenga miundombinu ya kijamii wakati huohuo huko wakipewa robo ya mapato ambayo nayo huishia Kwa viongozi Wala rushwa.Ndiyo maana makamanda wa chadema waliliona Hilo na kutaka endapo wataingia madarakani wataunda serikali za majimbo ambapo mapato ya sehemu husika yataendeleza sehemu husika na kiwango kidogo ndiyo kitapelekwa serikali kuu.peopleeees
 
Sio kweli, mbona chunya Kuna machimbo na wakazi wanaozunguka hayo maeneo ni maskini pia sana? Kuna hoja nyingine zaidi ya hii uliyoandika

Sehemu nyingi za machimbo hali ni hiyo hiyo. Hata ukienda nyamongo north Mara Hali ipo hivyo
 

Wangej8funza kwa Botswana. Kuna vitu vingi kama asilimia Tani hadi kumi itumike kujenga vitu vya maendeleo kama hospitali, shule, maji, umeme, masoko, barabara zinajengwa, hadi kufikia kuwalipa wananchi asilimia flani ya mapato ya jimbo lao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…