Hodi hodi Morogoro

Zipuwawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
3,050
Reaction score
656
Wa FJ nilikuwa sipo hapa nchini sasa nimerudi na nategemea kuwa nitakutana na wana JF hapa Moro nitakapokuwa nikiishi sasa naomba nikaribishwe. Ni kweli kuna siku nilisema ipo siku angalau nitamfahamu mtu hata wa ndani ya nyumba hii lakini hadi leo hakuna hata mmoja ninayemfahamu hata kwa kumuona hivyo wale wa Dar na Moro napenda kushirikiana nanyi kama mwana jamii mwenzenu. Hapa nipo Kilakala kwa sasa.
 
Moro ndo kwetu Maskani,
Niwapo najivinjari asilani
Viwanja tulivu kama jamvini
Karibu sana Moro, mji kasoro bahari

zunguka zunguka mitani, utaona utulivu mwanana
kama si mtawala, Kihonda, Forest, Kigurunyembe hata kilakala
karibu sana Moro Mji kasoro bahari.

Uwapo hapo Moro viwanja huzuria,
Kingstone, Moro hotel na hilux bila kusita
pitapita pale kahumba asiliani usivue viatu
zungukia Moro night lakini nako uwe makini
karibu sana Moro, mji kasoro bahari.
 
....Bong'ola au wapi?
 
Ukifika hakikisha unamtafuat Akili Unazo au Next Level utapata good time kuliko maelezo!!Pia unaweza kumtafuta mnyalu mmoja hivi ila kama vipi npm nikupe contact za hawa watu ili uwe unajuwa kunywa siyo unabip maake nihamisha TBL na SBL counter.huku pork au foil inasubiriwa kule liti executive pub
 
asante kwa mashairi yako kaumba siendi maana si mchezo pale au kumebadilika?
 
poa nitafanya hivyo
 
Front View kwa jioni si haba
Kama ilivyo E-Pub isivyo jaza kibaba
Blue Palm murua japo hakuna Palm ya blue
Karibu sana Moro, na Weekend ndo hii!
 
mtu akikuambia usiku utembelee pale mjini kati bynight sijui blue gani usithubutu, inavyoelekea serikali haipo pale, sidhani hata hao wanaojingamba kuwa wanapigania haki za watoto kama wapo, maisha ni ya aibu sana pale, ni huzuni kubwa kuona vitendo vya kiasherati na kihuni vinafanyika katikati ya mji bila kuona chombo chochote cha dola kuchukua hatua. Tafadhali usiende eneo lile ni hatari!!!!!!
 
Kilakala Bong'ola? Mie huwa nakula maji Rombo bar. Alafu nguruwe (KITIMOTO) napata pale Madizini. Kwa sasa siko huko, ila nikifika nitakutafuta. Lakini ni vema uwe unalamba ulabu.
 
asante kwa mashairi yako kaumba siendi maana si mchezo pale au kumebadilika?

Aiseee usitie mguu jamaa yangu... pale hapawezi badilika sana sana ndo panakuwa worse!!!
Tembelea Bush Bar barabara ya kwenda SUA!!!
Tarehe 20/02 Ntakuwa Home Moro kwa Likizo Nta-kuMP kaka!!!
 
Kilakala Bong'ola? Mie huwa nakula maji Rombo bar. Alafu nguruwe (KITIMOTO) napata pale Madizini. Kwa sasa siko huko, ila nikifika nitakutafuta. Lakini ni vema uwe unalamba ulabu.

.... Umenikumbusha Maeneo ya home....... Mizambatauni pale, Ukikata kushoto unakutana na Kitu cha Dragonare
 
ukitoka Moro ...... uje na huku makao makuu ya JF hapa A-Town....huku huwa hakuna mzaha.....binafsi nitakutembeza hadi maeneo ya Yaeda.....natumaini unatumia nyanyi choma
 
Niko moro pm number kuna mwanajf amefiwa 2nataka kwenda muona anapita moro kesho anaenda mazishini fanya hivyo mpendwa
 
Kahumba eneo hatarishi mkuu. Karibu Morogoro mji hauna migogoro wala kokoro. Mji wahitaji nafasi kama kula nanasi. Wahitaji kufikiri sio kikiri.
 
ukitoka Moro ...... uje na huku makao makuu ya JF hapa A-Town....huku huwa hakuna mzaha.....binafsi nitakutembeza hadi maeneo ya Yaeda.....natumaini unatumia nyanyi choma
Kipenzi, sasa ile nyama ya twiga ndo umenichunia? Orait, sasa kwa nini unataka ugomvi? Kipapatio cha arusha!
 
Kahumba eneo hatarishi mkuu. Karibu Morogoro mji hauna migogoro wala kokoro. Mji wahitaji nafasi kama kula nanasi. Wahitaji kufikiri sio kikiri.
Mkuu mcheki maty fasta you will be connected hasaka sana. We in dar, tunakukaribisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…