Hodi katika jamvi hili tukufu la uchambuzi yakinifu. Nakula kiapo leo hii kuwa mwanaJamvi muadilifu,na kuchangia mada kwa weledi na heshima kwa wanaJamvi wenzangu. Nitakubali kukosolewa pale nitakapokosea....maana lengo la mimi kujiunga kwenye Jamvi hili ni kujifunza na kupata uelewa katika mambo yanayonitatiza katika jamii na maisha yetu ya kila siku. Eeh Mungu nisaidie.
Ahsanteni.
Wakuu naomba Msaada jinsi ya kuweka Avatar kwenye profile yangu...
Nashukuru mkuu. Nimejaribu hiyo before lakini nilipofika pale kwenye kuchagua picha kwa custom avatar hainipi clickable option. Natumia iPad mara kwa mara kuliko desktop,inawezekana ikawa ni tatizo? Natanguliza shukrani zangu mkuu.juu kabisa kuna sehemu wameandika "settings" , click hapo then itakupeleaka sehemu unapoweza ku-edit kila kitu kuhusu profile yako,
kushoto hapo pa ku-edit settings utaona "avatar edit" , utaclick hapo, then utaselect custom avatar, then utachagua picha kama ipo kwenye deskop na folda gani,