Hodi Mwanza

Hodi Mwanza

Mimi najua yamekuja mapya mazuri na yameondoka mabovu ya zamani..[emoji3][emoji3]

Yote ni heri vile umekuwa kabinti kakubwa...teeeena, wanasema mvinyo wa zamani ndio mtam zaidi[emoji13][emoji2957]
Naaaaaaam....umemaliza yote..Niseme nini tena....

Mvinyo ni kama mbege tu.. unavyozidi kukaa ndivyo unazidi kuchachuka[emoji3]
 
We sijakusoma...kwanza njoo huku pembeni unipatie ule ubuyu bwana wengine hatujaelewa hata
 
Kwa mara ya kwanza Mwenye enzi Mungu akipenda nitawasili Mwanza siku ya kesho.

Gari wakati wa kwenda nitapanda basi la lampuni ya Kisbo halafu nitarudi na basi la kampuni ya happy nation.

Kwa nini kisbo? Kwa sababu sitapenda nilale njiani.

Wale wa ooh kapande mwewe (ndege) hapa sio mahali penu.... wengine passport tulishazichafua sana huko duniani so ndege sio issue sana! me kwa sasa ni basi mwanzo mwisho.

Ushauri mlionishauri kipindi kile kwenye uzi wangu wa wapi nikapumzike nimeuzingatia sana.

Baada ya mapumziko nitarudi na dagaa na samaki so msisite kunipatia oda zenu (Si mnajua tena yatima hadeki)

Haya mniombee safari njema.



Updates:
Nilifika saa 6 na dakika kadhaa usiku, safari ilikuwa ya kuchosha kiasi lakini Mungu mkubwa hatimaye kwa mara ya kwanza maishani mwangu nipo Mwanza.

Nilibahatisha kukutana na mwana jamii forums ambaye amekuwa na msaada mkubwa sana kwangu na kunifanya nipapende Mwanza na kutoboreka sana.
Huyu amekuwa kama tour guide wa hiyari kwangu bila kujali gharama na kuharibu ratiba zake ( yani Ana moyo wa dhahabu huyu). Mkuu shukrani sana sana sana. Unaingia kwenye list ya watu waliogusa maisha yangu tangu nipate akili za kupambanua mambo.

Nilichogundua watu wa huu mkoa wana upendo kuzidi baadhi ya mikoa niliyowahi kufika.
Pia kwa siku ya Leo tu nimeweza kuona fursa mbali mbali japo kwa juu juu zilizopo Mwanza na kama mambo yakienda sawa nitawajuza ni kwa vipi safari yangu ya kuja Mwanza itakavyoniinua kiuchumi.

Updates: Tarehe 4/6/2022
Baada ya kuzunguka hapa jijini mwanza kwa siku kadhaa, kesho nitarejea jijini Dar es salaam. Leo jioni nitapitamo (kimwanza mwanza) pale stend ya Nata kwa ajili ya kukata ticket ya basi lolote ambalo nitashauriwa na wenyeji lenye mwendo mzuri.
Bado ninaaga aga

Wana wa mwanza mbaki salama...ticket nimepata ya basi la ally's ....

Leo nilikuwa busy sana ninawaaga wana hata kulala nimeshindwa. Ila kmeniuma kuna mwana JF flani sijui Leo alibanwa na mama la mama akashindwa kuja kuniaga au vp [emoji12]

Mda huu wa saa saba na dakika 12 usiku mkubwa namalizia kuumwagilia moyo wangu hapa bonasera pamoja na kupata kondoo fresh kabisa then niangalie kiwanja kingine hadi saa 10 alfajiri nitaibukia kwenye basi la ally's tayari kwa kurudi jiji la joto kwa ajili ya michakato mingine.

Dah mwanza patamu sana sema tu mfuko unone. Isngekuwa Xmas naenda kujengea kaburi la bi mkubwa basi ningekuja huku mwanza tena. Ningekuja kipindi cha Sikukuu ya Mwaka mpya ila hii sikukuu huwa ninaitumia kwa ajili ya familia yangu.

Mungu akipenda tukutane pasaka ya 2023.
Kama utapenda tuungane tuje tule maraha na hawa masukuma huku...ujue wako wapweke sana hawana pa kupeleka hela za samaki.
Mwenyeji hajakula kimasihara kweli,karibu tena mwanza
 
Jaman wanawake sisi
Yani nyuma yangu hapa wamekaa couple...
Mdada anavyogombana na mumewe jaman . Mume anagombezwa huyu sijui huko ndani wanaishije...
Mara amsengenye WiFi yake ambaye alikuwa hana kazi sasa kapata kaziii...mara amsilibie dada wa watu kwa kaka yake ...
Yani jamani wanawake wa hivi ni mashetani. Hata umgombanishe mume na ndugu zake na wakagombana kweli ujue ipo siku upendo wa ndugu utarudi tu maana damu nzito...


Ila hayanihusu ngoja nisikilize huu wimbo wa gundu wa lava lava unaopiga hapa kwenye gari.

BTW niko nzega na chuma ya ally's
 
Jaman wanawake sisi
Yani nyuma yangu hapa wamekaa couple...
Mdada anavyogombana na mumewe jaman . Mume anagombezwa huyu sijui huko ndani wanaishije...
Mara amsengenye WiFi yake ambaye alikuwa hana kazi sasa kapata kaziii...mara amsilibie dada wa watu kwa kaka yake ...
Yani jamani wanawake wa hivi ni mashetani. Hata umgombanishe mume na ndugu zake na wakagombana kweli ujue ipo siku upendo wa ndugu utarudi tu maana damu nzito...


Ila hayanihusu ngoja nisikilize huu wimbo wa gundu wa lava lava unaopiga hapa kwenye gari.

BTW niko nzega na chuma ya ally's
Nakadori bana
 
Back
Top Bottom