Hata hivyo, ngoja nikueleze shida iko wapi. Asilimia kubwa ya mambo ninayosoma, yameandikwa kwa kiingereza. Nikikwambia nina kiu ya kusoma maandiko ya kiswahili yaliyoandikwa kwa ustadi wa kuzidi uwezo wangu kiuandishi katika lugha, utashangaa?
Halafu nikiwa nimechoka, napata tabu kujieleza kwa kiswahili. Huwa sipendezwi na kile nilichoandika. 🙁