Hofu inatawala kuliko uhalisia

Hofu inatawala kuliko uhalisia

Sawa
IMG_20230406_223803.jpg
 
Picha ya chini baada ya andiko lako ni tafsiri kua Yanga inakutesa sana kwa maana ya maandiko yako hayana uhusiano na picha..

Twende kwenye hoja sasa..

As vital kufungwa moja kule Casablanca haina uhusiano wowote na matokeo ya simba dhidi ya wydad katika mechi ya mkondo wa pili kule Morroco.

Ikumbukwe Yanga amemfunga Us Monastir, Monastir amemfunga As Barkane then Barkane amemfunga Wydad CAF super cup.

Hivyo basi haina maana kua Yanga kwasababu amemfunga US Monastir basi anaweza pia kumfunga As Barkane au Wydad kwasababu kwenye mpira kuna factors nyingi.

Finally,hauwezi kwenda peponi bila kufa, hivyo basi pia hauwezi kwenda Semi final kama hutopita robo kwa kumfunga Wydad.
 
Mechi mbili za Wydad Casablanca dhidi ya As vita ya Congo limepatikana bao 1 tu , tena bao hilo lilifungwa pale MOHAMED V STADIUM .

As vita amemaliza akishika mkia kwenye kundi A , yani ina maanisha As Vita ndiye alikuwa kibonde wa kundi kila mtu anachukua point kwake .

As Vita hana ubora kuliko Simba Sc kwasasa kwenye michuano ya CAF na wala hakuna timu bora zaidi ya SIMBA SC kwenye ukanda wa Afrika mashariki na kati linapokuja suala zima la CAF upande wa vilabu .

As Vita anakutana na Wydad tena kwao anaruhusu bao moja tu , anaenda kwake anapata sare ya 0-0 , hapo unapata funzo yakwamba kule Mohamed v Mohamed ,panatisha vibe la mashabiki ila kanda za video za As vita zinaweza kutumika kwenye kuifunza Simba Sc jinsi ya kucheza na Wydad pale Mohamed v Mohamed .

Cha maana Simba Sc inabidi imalize mchezo palepale LUPASO alafu ugenini ,wanaishi na Wydad ile KIFAZA yani mifumo ya Jose Mourinho, kuanzia namba ya nyuma hadi kwa washambuliaji wanaweka mabeki .....

Hofu ni hii inayotambaa kwasasa lakini Uhalisia Wydad anawezekan a ,na kama Simba Sc ina ndoto ya kutwaa taji hili inabidi icheze na timu kama hizi zenye Ubingwa huu , maana hatua hii wanacheza mabingwa huwezi ikuta Lipuli huku , kwahiyo hofu isitawale sana , Uhalisia ni kwamba Wydad wanawezekana ..kibaya zaidi wenye hofu zaidi ni watu wa Yanga kuliko simba wenye shughuli yao....




View attachment 2580989
Mpira hauna hesabu za hivyo mkuu kwamba kwavile fulani katoa sare au kafungwa goli moja basi na timu fulani kwavile ni bora kuliko fulani basi atashinda tu. Hakuna kitu kama hicho kwenye mpira na kama kipo basi anza kwa kuhofia kitendo cha juzi Wydad kutoka sare ya mbili mbili na timu iliyompiga simba goli tatu tatu
 
Wenye hofu na mechi ya Simba na wydad Ni Yanga, Simba wenyewe wala hawana shaka.

Wanaoongea sana Ni Utopolo.

Km alivyosema , uto wanapenda mechi ndogo ndogo na vitimu dhaifu
 
Naona mpira umeanza kuujua leo, Raja kakugonga nje ndani, kampiga Vipers 5 kaenda ku draw Kampala, wewe ukampiga Vipers nje ndani kwa kutumia mfano huo tunga sentence inayo anza na neno mimi ni bwege

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Umaandazi umekuzidi.

Kimsingi kasema Simba wakikaza inawezekana, kwanini AsVita na ubovu wao walionesha kitu halafu Simba ishindwe.

Ukizingatia Simba Ndiyo timu bora pekee ktk ukanda huu wa mashariki na Kati. Km hutaki hili ulete takwimu.
 
Mechi ya Wydad nmeziangalia nyingi Wydad hii sio ile ya mwaka jana,msimu huu hawana kasi wapo kawaida zile mechi zote na As vita niliangali mechi ya Js kabyile wanashinda 3 nliangalia Wydad wanafungika hawachezi soka la kasi kama Raja kwakua timu yao umri umeenda Raja wanavijana wengi,viungo wao wawili pale kati wana umri wa miaka 30+ ,striker yule msenegal ana mwili jumba na anapenda kugongana kwaio sio wale striker wakutumia akili ambao wanamshinda onyango,simba wanatakiwa watumie nafasi vizuri na kuwakimbiza mechi ya kwa Mkapa,Ubora wa Wydad kwamba wanacheza kikubwa sana na wanajua kutumia nafasi na kama ilivyo timu za kiarabu wakiwa kwao wanabebwa sana kwa mfano ile mechi na JSK goli walikabwa mda wote dkk kama ya 44 unapigwa mpira striker wao msenegal ana control mpira kwa mkono refa anapeta anafunga goli la kwanza,muhimu simba kuwaheshimu Wydad maana hawana mambo mengi wao pasi 3 wapo golini

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Hata Raja alidroo na vipers mliyoipiga nje ndani.
Piga ua galagaza simba havuki
 
Utaonaje kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati una boriti kwenye jicho lako?

jamiiforums1291591030-jpg.2581101

Habari ndiyo hiyo!! Hakuna mahali Simba imefungwa 6-0 michuano yoyote ya CAF!!
Mbumbumbu kazi mnayo. Yeye ndio kaanza kunitumia hiyo picha mimi nikamrudishia hiyo
 
Back
Top Bottom