Hofu: Kilimanjaro inaweza kutangazwa mkoa maalumu kwa sherehe za krismas.

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
2,026
Reaction score
3,107
Salama wakuu,

Ni hofu yangu tu nipo njiani kurudi nikitokea mgombani... Nimekutana na washkaji kibao ambao sio wachaga lakini naona swaga la kwenda kwetu kila krismas limewabamba. Pamoja na hayo wapo Jamaa kibao ambao wameahidi kushiriki krismas ijayo mkoani kili mwakani, baada ya kuvutiwa na namna ambayo tunafanya yetu.

Inawezekana kabisaaaa miaka kadhaa ijayo, huu mkoa ukatangazwa sehemu maalumu ya kusherekea krismas.

Karibuni wakuu.... Huku kwetu hamuibi kitu ila mtatumia na kutuachia maendeleo yetu.

Ni hofu tu.
 
hiyo ni kweli
ila usisahau na bukoba pia
 
hujui Christmas nini wewe unawaza starehe tu. kunywa mipombe na ngono zembe, hata hao wachaga wanaojua maana ya hii Siku hawafanyi kufuru.
 
Hold oooooon!!! Maana unaingilia mlango wa kutokea.... We huna kwenu.... Usotunyime kwenda kwetu
 
Ni wazo zuri sana likipata wabunifu na wakarembesha kidogo wazo lako linaweza kuvutia watu wengi wanaotafuta mahali pa kuspend during holidays haaswa Chrismass
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Ni wazo zuri sana likipata wabunifu na wakarembesha kidogo wazo lako linaweza kuvutia watu wengi wanaotafuta mahali pa kuspend during holidays haaswa Chrismass
Echungulia kwa jicho la kibiashara zaidi.... Inaeza ikaanza kama utamaduni ila badae ikawa kama utalii wa aina yake kukipatikana wapanga mipango wazuri ukizingatia kuna Kilimanjaro Mountain.....
 
Tatizo lenu mna kelele sana. Makabila kibao yanarudi kwao lakini hawafanyi matangazo.
 
Back
Top Bottom