lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Ukweli siku alipokufa nilifurahi, sikufurahia kifo chake, bali nilifurahi kwa sababu ameondoka kwenye kiti cha taifa. Nilifurahi kapisha kiti hicho kwa sababu Mimi nilimuona hakufaa kukalia kiti hicho.
Alikua ana uwezo lakini hakufaa. Kwa sababu gani alikua ana uwezo lakini hakufaa Nina sababu nyingi mno. Lakini chache ni hizi. Kazi kubwa ya Rais ni kuiunganisha nchi yaani kuwafanya raia wawe wamoja, hakua na dhamira hiyo, hakua na uwezo huo.
Kama ni ujenzi wa miundombinu, waliomtangulia walijenga na watakaokuja baada yake watajenga. Hakufata katiba, sheria, kanuni, miongozo, Mila na desturi zetu tulizojiwekea.
Ningefurahi pia kama angeondoka madarakani kwa njia yoyote ile. Furaha yangu sio njia ya kuondoka,furaha yangu Ni kupisha kiti.
Ningefurahi angeondolewa kwa nguvu,
Angejiuzilu,
Angeugua,
Angekubali kushindwa na namna nyingine yoyote ya kuondoka, mimi ningefurahi tu.
CCM ndio chama dhaifu Sana hapa nchini na Duniani kote, lakini Ni miongoni kwa vyama vyenye propaganda kubwa na uongo mwingi Sana.
Sababu kubwa ya CCM na wafuasi wake kuikataa katiba Bora ni hofu ya kutoka madarakani.
CCM inadanganyaga watu kuwa inapendwa,imeshinda kwa kishindo,Marais wake wanapendwa lakini pamoja na kujitekenya yenyewe hucheka yenyewe. CCM hakiwezi kuruhusu kuleta kwa katiba itakayotoa haki kwa sababu itapelekwa Shimoni kwa speed ya 6G.
Hivyo basi kila kiongozi kutoka Chama hicho huogopa kuleta katiba Bora kwa sababu anaogopa lawama za kuwa Raisi aliepelekea CCM kuondolewa madarakani.
Wao hawaangalii maslahi mapana ya Taifa,hawaangalii iko siku nchi inaweza kuingiza machafukoni kwa sababu ya katiba hii ya sasa kutokua bora.
Kwa hiyo viongozi wetu hawa wanawazaga chama tu badala ya nchi. Chama kinaweza kikafa lakini nchi ikabaki. Mfano KANU haipo kivile lakini KENYA inastawi.
Samia nilimshangilia Sana, sio kwa sababu ni mtu anefaa sana, hapana, kwa sababu alikalia kiti kilichoachwa na mtu ambae kwangu Mimi hakufaa. Nilimfurahia Samia kwa sababu ya kuwazomea wafuasi wa yule. Nilimfurahia kwa sababu sasa ndoto za kutawala milele zimezikwa rasmi. Nilimfurahia kwa sababu Naamini hawezi kuwa na tabia za ajabu kama za yule.
Ila nilijua na ninajua Samia ni zao la CCM na CCM na katiba ni kama Binadamu na corona19. Binadamu anaiogopa korona kwa sababu inaua,na CCM anaiogopa katiba mpya kwa sababu itamuondoa.
Na kwa sababu Samia ni zao la CCM,na Viongozi wa kutoka CCM hawana ujasiri kama aliokua nao Fredrick De Klerk aliewahi kuwa Rais wa mwisho Kaburu wa Afrika KUSINI.
Samia anaenda kupuuzwa kwa Kasi ya mwanga. Atachekwa na kupuuzwa na Magufuli Gang, atapuuzwa na wastaarabu wote duniani.
Kitu pekee Cha kufanya ili Jina lake kubaki hai milele na milele kama Shujaa wa kweli wa Tanzania na Afrika Ni kuwa upande wa wananchi na kuachana na kikundi kidogo tu ndani ya CCM.
Atumie Maguvu ya Urais aliyonayo kuleta katiba,atumie ubabe wa Urais kwa manufaa ya nchi sio kama Yule alitumia Maguvu kwa faida binafsi. Mama Jina lake litaishi Miele kama akileta katiba Bora.
Wapo watu Kama akina Fredrick De Klerk ambao wanakumbukwa kwa kuifanya SA kuwa Taifa Moja. Kikundi kidogo Sana Cha Makaburu wachache kilimpinga,lakini Makaburu wengi na Dunia vilimuunga mkono.
Karibu Samia suluhu Hassan. Usiruhusu kuingia kwenye Historia ya akina Mwendazake na Ben waliokuja kujuta na kuomba misamaha ikiwa too late.
Walikua na nguvu wakazitumia kwa kufanya ujinga.