Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Utabiri wa mwisho wa dunia umetolewa miaka mingi na mbali mbali huko nyuma.Utabiri wa namna hiyo ulipita na kuondoka na baadae watu kurudi kwenye shughuli zao na starehe zao kama kawaida.
Tangu kuzuka kwa corona binadamu wamepatwa na hofu iliyo kubwa kiasi kwamba wale waliozowea kuona dunia kama sehemu ya kustarehe wameingiwa na hofu kubwa sana kiasi kwamba wanakufa kwa hofu kabla ya corona.
Wale matajiri wa dunia na wenye fedha nyingi hasa Ulaya na mashariki ya kati wameona ugonjwa huu umewakatishia furaha zao.
Wamejiona hawana pa kutokea hasa kila kukicha wanapata taarifa za wimbi la kwanza na la pili na la tatu linafuatia.
Pamoja na kugunduliwa kwa chanjo mataifa tajiri wanaona haitoshi na wanazidi kujifungia ndani ya majumba na mipakani mwa nchi zao. Dunia imegeuka sura na kuanza kujivisha kiza cha siku ya kiama.
Mwenyezi Mungu azidi kutuhofisha na iwe sababu ya kumuogopa na kuachana na upuuzi wa dunia wa kudhulumiana na kufanya ufisadi wa kila namna.