Hofu ya kunguni Ufaransa

Hofu ya kunguni Ufaransa

Ila kunguni msumbufu aisee nilikuaga nasota na viroboto mkoani ila nilipofika Jiji x kunguni nilipitia salute
 
View attachment 2771374


Wananchi wa Ufaransa pamoja na watalii wanaoitembelea nchi hiyo wanaugulia maumivu baada ya kungátwa na kunguni ambao wamesambaa katika maeneo mengi hasa ya umma.

Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionesha kuwepo kwa wadudu hao hasa katika jiji la Paris kwenye treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles-de-Gaulle, Serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.

"Jimbo linahitaji haraka kuweka mpango wa utekelezaji dhidi ya janga hili wakati Ufaransa inajiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralympic 2024," ameandika Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire katika barua yake kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne.
Hii iliwahi kutokea Canada.
 
Anakimbia balaa Ila wakiwa wengi sasa wanaanza kujionyesha ukiona hadi unaanza kuwaona jua unamfugo wa Jeshi la kunguni mpaka wengine wamekosa pa kujificha
ukiwafikinya damu yao inanuka vibaya. Kwanza ni kinyaa kuona kundi la kunguni wamejificha kwenye mpasuko wa godoro au kitanda/kochi. Kiboko yao wavamiwe na kundi kubwa la mende hakuna rangi wataacha kuona. Mende nao wana kero ila kwa kuwakomesha kunguni mende utawapenda
 

NCHI 10 ZILIZO NA MATATIZO MABAYA ZAIDI YA KUNGUNI NA JINSI YA KUKABILIANA NAO

INDIA

India ina moja ya wadudu mbaya zaidi duniani, na infestations katika maeneo ya mijini na vijijini. Tatizo linatokana na ukosefu wa maarifa kuhusu mende za kitanda na jinsi ya kuzizuia, pamoja na uhaba wa suluhisho bora za kudhibiti wadudu.

MAREKANI

Uvamizi wa mdudu wa mdudu umeisumbua Marekani kwa miaka, hasa, katika miji mikubwa kama vile New York, Los Angeles, na Washington, DC Sababu zinazochangia ni pamoja na kiwango cha juu cha kusafiri na uhamaji wa nchi, pamoja na ukosefu wa mbinu bora za kudhibiti wadudu.

UINGEREZA

Katika miaka ya hivi karibuni, Uingereza imeona ongezeko kubwa la maambukizi ya mdudu wa kitanda, na London kuwa moja ya miji iliyoathirika zaidi. Hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha safari za kimataifa nchini, pamoja na ukosefu wa maarifa kuhusu mende za vitanda na jinsi ya kuzizuia.

KANADA

Canada pia imekumbwa na maambukizi ya virusi vya corona, huku Toronto na Vancouver zikiwa miongoni mwa miji iliyoathirika zaidi. Tatizo hilo linachangiwa na hali ya hewa ya nchi hiyo na kuongezeka kwa usafiri.

AUSTRALIA

mende za kitanda zinazidi kuenea nchini Australia, haswa katika miji mikubwa kama vile Sydney na Melbourne. Maambukizi yanaongezeka kwa sababu ya mazingira ya joto ya nchi na kuongezeka kwa usafiri.

CHINA

Wadudu wa mbu ni wasiwasi mkubwa nchini China, na infestations kuripotiwa katika maeneo ya mijini na vijijini. Tatizo hilo linazidishwa na kiwango cha juu cha uhamaji nchini na ukosefu wa hatua za kutosha za kudhibiti wadudu.

BRAZILI

Maambukizi ya wadudu yameongezeka nchini Brazil katika miaka ya hivi karibuni, hasa katika miji mikubwa kama vile Rio de Janeiro na Sao Paulo. Sababu zinazochangia ni pamoja na mazingira ya joto nchini na ukosefu wa taratibu za kutosha za kudhibiti wadudu.

URUSI

Urusi inakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya mdudu wa kitanda, na infestations kuripotiwa katika miji mikubwa kama vile Moscow na St Petersburg. Tatizo hilo linachangiwa na hali ya hewa ya nchi hiyo na kuongezeka kwa usafiri.

AFRIKA KUSINI

Maambukizi ya wadudu yameongezeka nchini Afrika Kusini, hasa katika miji mikubwa kama vile Johannesburg na Cape Town. Tatizo hili linachangiwa na hali ya hewa ya joto na utalii wa mara kwa mara.

MISRI

Misri ina tatizo kubwa la mdudu wa kitanda, na infestations kumbukumbu katika maeneo ya mijini na vijijini. Mazingira ya joto nchini na ukosefu wa taratibu za kutosha za usimamizi wa wadudu wote wanaongeza tatizo.
Ili kushughulikia maswala ya mdudu wa kitanda, ni muhimu kutambua viashiria vya uvamizi na kutekeleza hatua za kuzuia. Miongoni mwa hatua za ufanisi ni:
  1. Kusafisha na kusafisha mara kwa mara.
  2. Kutumia magodoro ya ushahidi wa kitanda na vifuniko vya mto.
  3. Wakati wa kusafiri, weka mizigo kwenye sakafu na mbali na vitanda.
  4. Kuchunguza samani kutumika kabla ya kuleta ndani ya nyumba.
  5. Tumia dawa ya asili ya mende ya kitanda.
Kwa kumalizia, uvamizi wa mdudu wa kitanda unazidi kuwa wa kawaida ulimwenguni, na India, Merika, Uingereza, Canada, Australia, China, Brazil, Urusi, Afrika Kusini, na Misri kati ya walioathirika zaidi. Kwa kuchukua hatua za kuzuia au kutumia mdudu wa kitanda cha mitishamba unaweza kushinda tatizo hili.
 
Hawa kunguni wana ndugu zao wengine akina kupe, papasi, chawa, utitiri na viroboto ambao kwa pamoja wanaitwa hectoparasites kwa kuwa wananyonya damu wakiwa nje ya kiumbe wanayemyonya damu, ongeza na mbu, mbung'o na ndorobo. Wale wanaonyonya damu au virutubisha wakiwa ndani ya mwili wa kiumbe wanayemfonza wanaitwa endoparasites, ndio minyoo. All in all kunguni ni mshenzi kuliko wote japo mbu na minyoo ni hatari, kuishi na kunguni ni uzembe na uchafu. Chawa wa kichwani wamepotea siku hizi kuona mtu ana mayai ya chawa kichwani ila chawa wa nguoni bado wapo, unaweza kuambikizwa kwa kubanana kwenye usafiri au kukaa kwa kugusana na mtu mwenye chawa. Mbaya zaidi umevaa nguo safi uko kanisani/msikitini mara kungunguni/chawa anakutambalia humuoni anaonwa na ulio nao karibu, utaaibika na kuonekana huna usafi
 
Kunguni hakai sehemu chafu tu
We humjui huyo mdudu akiingia ameingia.
Hata ikulu anaishi na anatamba vizuri
kunguni hana adabu, unakuta mtu ana masofa safi ukikalia tu wanakuibukia na kuanza kukung'ata mchana kweupe
 
Mkumbuke wapo chawa wa kwenye magogo, wood lice, wao hawaishi kwa kunyonya damu za kiumbe hai, wao wana namna yao kula. Huenda kuna kunguni wasiotegemea kunyonya damu wakawa wapo kwenye mimea tu kama kimatiro na mbu wasionyonya damu wananyonya maua tu.
 
Kuna gesti kadhaa maeneo mbalimbali niliwahi kulala na kujikuta usingizi umevurugika kwa kung'atwa na kunguni. Kuna gesti ni wachafu hawachunguzi vitanda kama tayari vimepata kunguni. Vitanda vinaliliwa na wageni wengi, wengine husafiri na kunguni/chawa na kwenda kuwaambukiza huko.
 
Sina imani na wageni wangu wanaokuja na kulala naona kama wana wadudu wasumbufu, chawa/kunguni. Masela wanaokuja chumbani kwangu na kukalia kitanda nimewaandikia bango usilete kunguni na chawa. Bora upambane na umbu kwa net, kunguni hata uweke net utawaona pakipambazuka wanatambalia net kwenda kupana juu ya net, ukiwaacha wataongezeka na utaibika kwa kuishi na wadudu hao wenye kukupa sifa ya uchafu. Kiboko yao ilikuwa dawa ya ngao, iliwateketeza sambamba na mbu pamoja na wadudu wengine watakaogusana na net, we mwenye ukigusana na ngao utahisi mwili unawaka moto, uko karibu na jiko
 
Duh! Saa saba usiku, aljazeera wanaripoti habari za kunguni huko ufaransa. Kumbe ni habari kubwa mpaka imeripotiwa na mashirika makubwa ya habari duniani. Kunguni wanaitwa bed bug
 
Hivi mkuu mazingira anayoishi kunguni na chawa ni tofauti?
Ndio, chawa anadhibitika kwa usafi ila kunguni huwezi mdhibiti hvo, unaweza ukawa msafi sana ila ukapata mgeni akaja na kunguni, ndo tayari hyo, mpaka utumia dawa kuwaangamiza la sivo watazaana mpaka, na usafi wako, chezea kunguni wewe.
 
Aljazeera nao wameripoti habari za kunguni huko ufaransa. Sisi huku tumewazoea na hatuoni tatizo japo wanasumbua hasa vitandani mwetu. Huko kenya tv zao ziliwahi kuripoti wananchi wao kusumbuliwa na wadudu hao. Sisi kwa nini tunawachukulia poa kunguni wakati ni ishara ya uchafu? Kama mbu anaundiwa kampeni ya kumtokomeza kwa nini kunguni nae asiundiwe kampeni ya kummaliza? Huyu mdudu ni kero na aibu kuwa naye
 
Back
Top Bottom