Hofu ya kunguni Ufaransa

Hofu ya kunguni Ufaransa

Duh! Saa saba usiku, aljazeera wanaripoti habari za kunguni huko ufaransa. Kumbe ni habari kubwa mpaka imeripotiwa na mashirika makubwa ya habari duniani. Kunguni wanaitwa bud bed
kwa kimombo wanaitwa bed bugs mkuu siyo bud bed.
 
kwa kimombo wanaitwa bed bugs mkuu siyo bud bed.
ni sawa mkuu, nilipishanisha sentensi, ile nataka kurekebisha tu naona notificatio toka kwako huku aljazeera nao wakirudia taarifa hiyo kwa kutaja bed bugs
 
Niliwahi kulala ugenini nikashindwa kutambua ni upi muwasho wa kung'atwa kati ya kunguni na mbu. Nilishambuliwa na wadudu wote wawili kunguni na mbu usiku kucha. Kitanda hakikuwa na net walau mbu wasining'ate. Haikuishia hapo tu chawa na viroboto nao walinishambulia. Mara homa hiyo, kupimwa maralia ipo
 
View attachment 2771374


Wananchi wa Ufaransa pamoja na watalii wanaoitembelea nchi hiyo wanaugulia maumivu baada ya kungátwa na kunguni ambao wamesambaa katika maeneo mengi hasa ya umma.

Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionesha kuwepo kwa wadudu hao hasa katika jiji la Paris kwenye treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles-de-Gaulle, Serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.

"Jimbo linahitaji haraka kuweka mpango wa utekelezaji dhidi ya janga hili wakati Ufaransa inajiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralympic 2024," ameandika Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire katika barua yake kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne.
Wazungunnisio wapenda duniani wanapatikana Ufaransa...sema ni vile wananizidi vitu vingi vinavyo define quality living standard
 
ni sawa mkuu, nilipishanisha sentensi, ile nataka kurekebisha tu naona notificatio toka kwako huku aljazeera nao wakirudia taarifa hiyo kwa kutaja bed bugs
eh! kumbe aljazeera ndo wamekutoa tongotongo, ulikuwa hujui kuwa kunguni kwa kimombo wanaitwa bed bugs?
 
eh! kumbe aljazeera ndo wamekutoa tongotongo, ulikuwa hujui kuwa kunguni kwa kimombo wanaitwa bed bugs?
najua mkuu, ni typing erra tu, kwa sie tunaeandika maneno mengi kukosea sentensi ni kawaida no matter ni lugha gani tunatumia, ndio maana kuna ma editor katika news room. Nina hoja nyingi za kujitetea katika uandishi wangu ninapokosea huwa si makusudi, kuna over look pia
 
Mkumbuke wapo chawa wa kwenye magogo, wood lice, wao hawaishi kwa kunyonya damu za kiumbe hai, wao wana namna yao kula. Huenda kuna kunguni wasiotegemea kunyonya damu wakawa wapo kwenye mimea tu kama kimatiro na mbu wasionyonya damu wananyonya maua tu.
Hao tuwaite kunguni wa kimataifa
 
eh! kumbe aljazeera ndo wamekutoa tongotongo, ulikuwa hujui kuwa kunguni kwa kimombo wanaitwa bed bugs?
sasa kama nawajua wood lice nashindwaje kuwajua bed bugs? Kama kuna wood lice na leaf buds wapo ujue. Unashangaa nini mi kuchanganya madesa wakati ni kawaida?
 
Kiboko yao wavamiwe na kundi kubwa la mende hakuna rangi wataacha kuona. Mende nao wana kero ila kwa kuwakomesha kunguni mende utawapenda
Hii mpya hii kwa hio kunguni huwafanya nini mende? Maana Mimi mende ndio siwapendi kuliko kunguni sababu wananuka japokua kunguni wananuka Ila mende wananuka zaidi

Yaan sipendi kukaa sehemu Ina mende, kunguni, mbu, panya na sisimizi hii timu naichukia,
 
Uchafu ni zao la hao kunguni.Hakuna lingine.Jiji zima wanastarehe tu hadi kunguni wanazaliana.Ni sawa na funza.Hawatokei tu kama 👽 aliens.Sababu ni uchafu.
 
Niliwahi kulala ugenini nikashindwa kutambua ni upi muwasho wa kung'atwa kati ya kunguni na mbu. Nilishambuliwa na wadudu wote wawili kunguni na mbu usiku kucha. Kitanda hakikuwa na net walau mbu wasining'ate. Haikuishia hapo tu chawa na viroboto nao walinishambulia. Mara homa hiyo, kupimwa maralia ipo
Kitanda Cha mbao used ndio kiliniingizia kunguni jamaa walijificha kwenye tendegu mule kwenye kona za kitanda unapokichomeka kwa ndani nilikuja kushtuka baadae wakitoka mule wanaanza kutaga kwenye godoro kunguni wanapenda Giza hawapendi mwanga kukiwa na Giza na kajotojoto ndio wana-enjoy na wakitaga kwenye godoro km lina cover basi wanaingia' ndani ya cover mule ndio wanaenda kuishi humo unalilalia cover kumbe ndani umewalalia kunguni usiku wanatoka wanaanza kukutafuta na kukutafuna wanazaliana kwenye godoro na yale mayai yao yanaliharibu godoro linapatwa na ukungu ukija kushtuka unaweza ukalichemsha godoro kunguni hawafani Ila niliwakomesha hawakurudi tena kwanza walikimbia nyumba wenyewe mwanga mwanga mwanga usafi usafi usafi usafi kunguni hakai eneo hilo lazima akimbie japokua wanasema kunguni anaweza akakaa hata mwaka bila kula bila kutaga
 
Ndio madhara ya kuruhusu wakimbizi wa kiarabu,sasa wamekuja na kunguni kutoka arabia,inasikitisha sana.
 
Olympic ni sawa na mbio za mwenge, Olympic ni kidunia zaidi
 
Kunguni hakai sehemu chafu tu
We humjui huyo mdudu akiingia ameingia.
Hata ikulu anaishi na anatamba vizuri
Watu wa afya walitudanganya sana kwa hiyo wahuni bado wanaamini kunguni anakaa sehemu chafu tu yeye popote kambi ili mradi apate password ya kuingia tuu...
 
Tuambiane ukweli, hawa kunguni wa sasa ndio wale wale wa zamani? Hawa wa sasa wanaongezeka lakini huoni mabuu/mayai yao yaliyotagwa na kuanguliwa, unaona madoadoa meusi kinyesi chao tu. Wale kunguni wa zamani mabuu/mayai yao yalionekana. Au na wenyewe wamekuwa kama nzi? Kuna nzi wanaotaga mayai/mabuu na kuna nzi wanozaa funza/mafinyufinyu. Nyoka nao wapo wanaotaga mayai na wanaozaa. Sioni mayai ya kunguni siku hizi naona madoadoa tu
 
Back
Top Bottom