Hofu ya kunguni Ufaransa

Hofu ya kunguni Ufaransa

View attachment 2771374


Wananchi wa Ufaransa pamoja na watalii wanaoitembelea nchi hiyo wanaugulia maumivu baada ya kungátwa na kunguni ambao wamesambaa katika maeneo mengi hasa ya umma.

Kufuatia kuwepo kwa picha mbalimbali za video mitandaoni zikionesha kuwepo kwa wadudu hao hasa katika jiji la Paris kwenye treni za mwendokasi, hospitali, nyumba za sinema na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles-de-Gaulle, Serikali ya Ufaransa imesema inaelekeza juhudi zake katika kupambana na kunguni hao.

"Jimbo linahitaji haraka kuweka mpango wa utekelezaji dhidi ya janga hili wakati Ufaransa inajiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralympic 2024," ameandika Naibu Meya wa Paris, Emmanuel Gregoire katika barua yake kwa Waziri Mkuu Elisabeth Borne.
Aibu
 
Wakati kunguuni wakitawala na kutangazwa na vyombo vikubwa vya utangazaji duniani kuwa wanasumbua ufaransa, ndugu zao papasi wamepotea kabisa, kulikuwa na homa inaitwa homa ya papasi iliogopeka sana. Sijawaona na siwasikii papasi kama wapo duniani, kwetu papasi wanaitwa nkundi, anaanza kukunyonya damu akiwa mdogo akishiba anakuwa mkubwa, ukishituka ukamshika anapasuka na kukuchafu kwa damu halafu alipokunyonyea damu anaacha alama ya damu iliyovia mwilini
 
Ndio, chawa anadhibitika kwa usafi ila kunguni huwezi mdhibiti hvo, unaweza ukawa msafi sana ila ukapata mgeni akaja na kunguni, ndo tayari hyo, mpaka utumia dawa kuwaangamiza la sivo watazaana mpaka, na usafi wako, chezea kunguni wewe.
Oh na inasemekana Paris kunguni wameletwa na blacks from West Africa😂😂
 
chawa anapenda mazingira yenye jotojoto la kiumbe anayeishi nae japo wakati mwingine alipo kunguni na chawa yupo
Yeah hata mimi hivi ndivyo nilivyokuwa najua. Ila kunguni dah, akikung'ata anaacha alama alafu haifutiki mapema😄
 
Na kweli,nimeona vyombo vya habari wale matianalist wamehusha immigrants ndo wameleta kunguni.Maana waafrica wanakuja kwa Boti kwenye mazingira machafu.
Hapana ,Ni kwamba serikali za miji mingi zipo kwenye ukata wa kifedha so wamepunguza budget za public sanitation kwenye miji ,so kuna tatizo la uchafu kwenye miji mingi Ulaya na Marekani .
Na msongamano wa homeless people na wahamiaji haramu wasio na makazi .
Newyork pia inapambana na tatizo kubwa la panya , yes panya na unaweza staajabu jiji kubwa kama Newyork linakosaje pesa za kukabiliana na tatizo la uchafu ? ,Ila ndio hivyo sasa hali halisi

 
Kunguni hakai sehemu chafu tu
We humjui huyo mdudu akiingia ameingia.
Hata ikulu anaishi na anatamba vizuri
1. Kunguni hukaa sehemu isiyo na hewa safi ya kutosha na huzaliana kwa wingi wa ajabu
2. Kunguni hukaa sehemu chafu full stop.

Ukitaka kuamini hili, nyumba yoyote yenye kunguni hata wawe wakubwa kama watoto wa mende ukiruhusu hewa safi ya kutosha tu kunguni hufa na kuto zaliana tena.

Lakini usiporuhusu hewa safi ya kutosha hata upige dawa gani kunguni huwa wengi zaid kuliko mwanzo.

Sumu ya kunguni huwa na joto kwakuwa mayai ya kunguni huhitaji joto kali ili kuanguliwa ukipiga sumu tu bila kuwa na HEWA SAFI YA KUTOSHA KINACHOTOKEA MAMA KUNGUNI HUFA NA MAYAI HUANGULIWA

HIVYO INAKUWA UMEFANYA KAZI BURE!!
 
Kunguni akishatia maguu sehemu tayari kimenuka, haijalishi kuna usafi wa hali gani, kunguni sehemu zenye uficho ficho ndio mahali pake.
 
Kumbe kunguni zipo hadi ulaya [emoji23]
Mwalim gan sasa hujui kuwa magonjwa yote ya mlipuko yanmeanzia huko.kunbuka the black plague, huko ulay ndio watu walikua wanaua vikongwe kwa tuhuma za uchaw ykiinekana nna macho mekund ummeenda.refer kitu inaitwa purge
 
Kipindi Cha Summer, wengi huko ulaya hukitumia kusafiri sehemu mbalimbali na interaction inkaua kubwa, inasemekana hii ndio sababu ya kusambaa kwa wadudu hao Kila Summer inapokua inaisha.
 
Huku tunao CHAWA WA MAMA ABDULI wala haturingi.!!
 
Nilijua kunguni ni wadudu Wa sisi maskini tu
 
Back
Top Bottom