Hofu ya maambukizi ya VVU inanimaliza kiafya, nilishiriki ngono na muathirika wa UKIMWI

Hofu ya maambukizi ya VVU inanimaliza kiafya, nilishiriki ngono na muathirika wa UKIMWI

Ni siku ya 31 leo tangu nianze kutumia dawa za Kuzuia maambukizi ya Ukimwi kwa watu walio mazingira hatarishi kupata ugonjwa huo (PEP), Dozi hii nimeimaliza jana.Hofu niliyo nayo imenifanya nishndwe kufanya kitu chochote cha maana zaidi ya kuzorota mwili.

Binafsi nina utaratibu wa kupima afya kwa kila mwanamke mpya ninaekutana nae, lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Huyu mdada sikuwahi kukutana nae katika maisha yangu, kwa mara ya kwanza nimekutana nae MALAIKA BEACH HOTEL MWANZA ilikuwa ni usiku wa Jumapili, Mimi nikiwa ni mgeni pale kwa siku kadhaa na huyu dada alikuwa na marafiki zake kwenye meza iliyokuwa pembeni yangu. Kwa umbo na uzuri wamebarikiwa haswa.

Alikuwa amevaa vazi ambalo ukichanganya umbo na rangi yake kwa namna yoyote ile mwanaume yeyote aliyekamilika lazma atatamani kuwa karibu, na vyombo vilikuwa vimeshanikolea kama saa 6 hivi usiku nikamuita kumuomba kampani ahamie kwenye meza yangu hakusita, huo ukawa mwanzo ambao mwisho wake tukawa wote kwenye room yangu niliyofkia pale hotelini. Siku hii sikuwa na vipimo, nilijaribu kutafuta pale hotelini nikakosa ilibidi nichukue condom, Tukafanya sikuwa na vurugu katkati ya mchezo mwenyewe nikaomba kuchomoa ile condom akakubali hata hivyo sikuchukua mda nikamaliza baada ya kumaliza nikawa najilaumu sana na sikurudia tena mpaka alivyoondoka tukapanga, tukutane kesho yake ili tuweze kupima tufanye mambo yetu kwa uhuru, Akakubali.

kesho yake Jumatatu Akaja, na mimi nikawa tayari nimeshanunua Vipimo. Mwenzangu akabadilika akagoma kupima baada ya kumbembeleza kwa mda mrefu akakubali kwa sharti nianze mimi na majibu yeye nisimpe nibaki nayo mimi. Baada ya kupima majibu yake yakawa na changamoto. Nilijihisi kufa na isitoshe kipindi tunapimana ile kujitoboa nilishika kile kidole chake bila tahadhari, Sehemu ya damu yake ikagusana na kidole chngu nilichojitoboa kutoa damu. Hapa nilichanganyikiwa zaidi.

Asubuhi ya Jumanne nimeamka mapema kazi ilikuwa ni kusaka hospital ambayo naweza Kupata dawa za PEP ili nianze dozi, nilizunguka na boda kama kichaa. Jana nimemaliza hii dozi na kila wiki tangu nianze kutumia hii dozi nacheki afya yangu. Mpaka mda huu bado sijapata maambukizi ila nina hofu sana.

Kila nikifikiria huu ugonjwa napata shida sana.
Kwani hizo pep zinatumikaje jamani
 
Uko sahihi mkuu. Watu wengi wasichojua ni namna gani HIV AIDS inapipwa, na hapo ndipi wanapopigiwa.

Mwili wa binadamu umeumbwa kiasi kwamba unaweza kupambana na magonjwa kwa kutumia Kinga hasili ya mwili/antibody (assume antibody ni kama wizara ya ulinzi). Leo hii uking'atwa na mbu wa malaria, antibody (wizara ya ulinzi) ikidetect ilo jambo itarelease antigens (assume hawa ni askari sasa) ili kuweza kufight vimelea vya malaria. Na ikivishinda, mwili utakuwa salama, hautopata malaria. Kwahiyo tukisema tukupime wewe, tukikuta una antigens waliokuwa wanapigana na vimelea vya malaria, hatuwez kusema unamalaria, Bali tutaupongeza mwili kwa kuweza kujilinda. Ili tuseme una Malaria, lazima wale bacteria wanaosababisha Malaria wawe nidetected, wakishaonekana kwenye vipimo hapo tunasema unamalaria, then unapewa dozi ya malaria. Na antigens wapo wa aina tofauti tofauti kutegemeana na mwili unapambana na tatizo gani.

Sasa tukirudi kwa upande wa ukimwi, jinsi unavyopimwa ndio inashangaza. Vipimo karibia vyote vya huu ugonjwa fake vinapima uwepo wa antigens. Kwamba Kuna specific antigens wakiwa detected tu, basi utaambiwa una ukimwi. Yani badala waupongeze mwili kwamba umetoa askari wa kuupambania, wao wanauhukumu na kusema uwepo wa wale Askari (antigens) maana yake ww ni mgonjwa. Kwanini magonjwa mengine yote huwa tunapima vimelea vya ugonjwa husika, Ila kwa ukimwi tunapima antigens?

UKIMWI = Upungufu wa Kinga Mwilini, yani wakuu mnaamini kuwa Upungufu wa Kinga aliokuwa nao mtu mmoja, unaweza kuambukiza mtu mwingine?

Tuchukulie mfano rahisi, yani mpenzi wako akiwa na utapiamlo, then akuambukize utapiamlo wake kwa kujamiiana? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Antibody ndo inapimwa
 
Back
Top Bottom