Erick G. Mkinga
Member
- May 19, 2011
- 62
- 5
Ndugu zanguni,katika mafundisho yangu ya dini nimefundishwa kuwa Uongozi wowote ule unatoka kwa Mungu,..Na sio kwa SHETANI hata kama umeingia kwa RUshwa...Lakini mwenyezi Mungu anaacha ata ule uongozi mbaya ili tukome,tutambue kwamba tumesahau kumfikiria yeye na kuabudu miungu mingine,..Tunaona mfano wana waisrael walipokuwa wanakosea Mungu aliwaadhibu kwa Kuwaweka chini ya mataifa mpaka walipotubu...Sasa je Leo Tanzania huu uliopo ni Uongozi wa namna Ipi..?Umetoka kwa Mungu hakuna ubishi lakini ni ili TUKOME au TUFURAHI..na kama ili TUKOME ,,..unaamini kwamba Maandamano ya CHADEMA ndio njia Ya Mwenyezi Kutukomboa,..Bila ya watu kumgeukia YEYE...