UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Katika wodi za uzazi, sauti za uchungu na matumaini hukutana. Wakati mwingine, dakika chache ndizo hutenganisha uhai na mauti. Ndipo upasuaji wa dharura unapokuwa tumaini la mwisho. Lakini nyuma ya kila uamuzi huo, kuna swali lisiloepukika: je, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu sahihi za kitabibu au kuna uwezekano wa kuzidi matumizi?
Huu ni uhalisia wa njiapanda ya kila siku unaowakabili madaktari siyo wa mkoani Njombe pekee bali pengine katika sehemu nyingine nchini. Kwa wataalamu wa afya, uamuzi wa kufanya upasuaji si jambo la kubahatisha. Ni hatua inayotokana na tathmini ya kina ya hali ya mama na mtoto.
Takwimu zinaonyesha wazi kwamba mkoa wa Njombe unaongoza kwa kinamama wajawazito kujifungua kwa upasuaji, huku hali ikiwa na pande zake mbili kwa asilimia 29, karibu mara mbili ya kiwango cha juu kinachopendekezwa na WHO ambacho ni kati ya asilimia 10 -15.
Kwa mujibu wa takwimu za kitafiti, upasuaji wa kujifungua (CS) unapozidi kuongezeka ni kama ishara ya mafanikio ya afya ya mama na mtoto. Lakini kwa upande mwingine, wadadisi wana wasiwasi wakiuliza iwapo ongezeko hili ni la kiafya au linaendeshwa na sababu zisizo za lazima?
Upande mzuri, upasuaji unaookoa maisha unapatikana kwa wanawake wengi, hasa wakati mtoto yuko hatarini, mama ana matatizo ya kiafya, au uchungu wa kujifungua hausogei. Hii inapunguza vifo vya akina mama na watoto.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe, Dk. Mhina Edward anasema hali ya dharura inaweza kumfanya mjamzito kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha ya mama na mtoto yanapokuwa hatarini.
Dharura hizo zinaweza kuwa pale mtoto anapokuwa hatarini tumboni, uchungu hausogei, au mama ana matatizo ya kiafya yanayoweza kuhatarisha maisha, upasuaji huwa suluhisho la kuokoa maisha. Katika mazingira haya, kuchelewa kuchukua hatua kunaweza kuwa na gharama kubwa zaidi kuliko upasuaji wenyewe.
Hata hivyo, upande mwingine unaowasha taa ya tahadhari. Utafiti unaonyesha baadhi ya upasuaji hufanywa bila sababu za kutosha za kiafya. Wanawake wanaweza kuchagua CS hata isipokuwa lazima, na madaktari wanaweza kupendelea CS kutokana na usalama au shinikizo la muda.
Matokeo yake ni upasuaji mwingi usio wa lazima unaoleta hatari kubwa: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, sepsis, kuhitaji damu ya kuongezewa, kupona polepole, na katika mimba zijazo hatari ya kupasuka kwa nyonga. Kwa watoto, madhara ya ganzi na matatizo ya kupumua yanaweza kutokea.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Dk. Jabir Juma, anasema kuna mikakati ya kupunguza upasuaji usio wa lazima, ikihusisha kushirikiana na hospitali binafsi, kuelimisha jamii kuhusu uzazi wa mpango, kuboresha lishe na kuzuia udumavu ili kuwawezesha wanawake kujifungua kwa njia ya kawaida.
Dk. Juma anaeleza kuwa lengo ni kupunguza kiwango cha upasuaji hadi asilimia 15, huku asilimia 85 ya wanawake wakijifungua kwa njia ya kawaida. Anasisitiza umuhimu wa tathmini za kina kwa wajawazito na matumizi sahihi ya fomu za uchungu ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
Anabainisha kuwa upasuaji wa dharura mara nyingi husababishwa na hali kama uzazi pingamizi, mtoto kuwa mkubwa kuliko njia ya uzazi, mapacha, mtoto kushindwa kupumua tumboni, au kifafa cha mimba. Hizi ni hali zinazohitaji uamuzi wa haraka na sahihi wa daktari.
Maadili ya ushirikishwaji
Katika chumba cha matibabu, maamuzi hufanyika kwa dakika chache lakini athari zake hudumu maisha yote. Ndipo maadili ya udaktari yanapochukua nafasi—yakiongozwa na kanuni kuu ya ridhaa ya mgonjwa. Kwa mama mjamzito au mgonjwa yeyote, haki ya kupewa taarifa sahihi na kushiriki katika maamuzi si hiari ya daktari, bali ni msingi wa huduma bora.
Dk. Mhina anasisitiza kuwa taarifa kamili humwezesha mgonjwa kuelewa hali yake, chaguzi za matibabu na hatari zake. “Mama anapaswa kuelewa hali yake, chaguzi zilizopo, na hatari zinazoweza kutokea. Hii hujenga uaminifu na kumwezesha kufanya uamuzi sahihi,” anasema.
Hili si suala la mawasiliano tu bali ni ujenzi wa uaminifu ambao ni nguzo inayounganisha mgonjwa na mtoa huduma. Pale ambapo mgonjwa anahusishwa kikamilifu, hata uamuzi mgumu hupokelewa kwa uelewa mpana zaidi.
Dk. Mhina anaongeza kuwa ushirikiano wa timu ya madaktari pamoja na uwekaji sahihi wa kumbukumbu za matibabu ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa mama na mtoto na kwamba huo siyo taratibu tu, bali ni haki ya msingi ya mgonjwa kujua na kushiriki katika maamuzi yanayohusu mwili wake.
Hata hivyo, taaluma ya udaktari haifanyi kazi katika mazingira mepesi kila wakati. Kuna nyakati za dharura ambapo mgonjwa hawezi kutoa ridhaa, na ndipo kanuni ya implied consent hutumika, ikiwaruhusu madaktari kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha. Lakini hata katika hali hizi, maamuzi yanapaswa kuongozwa na weledi, ushahidi wa kitabibu na uadilifu usiotetereka.
Mtihani wa kesi
Misingi hii ya maadili iliwahi kupitia mtihani katika Kesi ya Madai Na. 89 ya mwaka 2019 iliyohusu madai ya uzembe wa kitabibu dhidi ya Hospitali ya Kairuki na Dk. George Chugulu. Mlalamikaji, Florah Lengwana, alidai kuwa alifanyiwa upasuaji mkubwa bila ridhaa yake na baadaye kupoteza mfuko wa uzazi, hali iliyomnyima uwezo wa kupata watoto.
Kwa upande wake, utetezi ulieleza kuwa Florah aliwasili hospitalini akiwa na historia ya utasa na maambukizi katika mfumo wa uzazi, na kwamba vipimo na upasuaji vilikuwa muhimu kitabibu. Walisisitiza pia kuwa alisaini fomu ya ridhaa iliyoruhusu hatua za ziada wakati wa matibabu.
Mahakama ilipochambua hoja hizi, haikuishia tu kuangalia matokeo ya matibabu bali ilijikita katika mchakato mzima wa kitaaluma. Kwa kutumia kipimo cha kesi ya Bolam dhidi ya Friern Hospital, ilitathmini kama hatua zilizochukuliwa zililingana na kile ambacho daktari mwingine mwenye ujuzi wa kawaida angefanya katika mazingira kama hayo.
Ilionekana kuwa madaktari walifuata viwango vinavyokubalika kitaaluma: walifanya vipimo vinavyohitajika, walichukua hatua ya upasuaji kutokana na hali halisi waliyoikuta, na walikuwa na msingi wa ridhaa ulioruhusu hatua za ziada. Aidha, mahakama ilikumbusha kupitia kanuni ya kesi ya Jacob Mathew dhidi ya State of Punjab kuwa matokeo mabaya pekee hayawezi kuthibitisha uzembe wa kitabibu.
Jambo jingine lililobeba uzito ni mchango wa mgonjwa mwenyewe katika mchakato wa matibabu. Mahakama ilibaini kuwa Florah hakufuata ushauri wa madaktari kwani alikataa kulazwa na hakurejea kwa ufuatiliaji, hali iliyopunguza uwezekano wa kupata huduma endelevu na kuongeza hatari ya madhara.
Hatimaye, hukumu ilitupilia mbali madai ya uzembe, ikisisitiza kuwa ushahidi uliopo haukufikia kiwango cha kuthibitisha kosa hilo. Hakukuwa na fidia iliyotolewa, na mlalamikaji alibebeshwa gharama za kesi.
Ujumbe kwa wahusika
Kwa madaktari, kesi hii ni ukumbusho kwamba taaluma si tu kuhusu ujuzi wa kitabibu bali pia uwazi, mawasiliano na uwekaji sahihi wa kumbukumbu. Ridhaa ya mgonjwa lazima iwe ya kweli na si karatasi tu, bali mchakato wa kumwezesha mgonjwa kuelewa na kushiriki kikamilifu.
Kwa wagonjwa, funzo ni wazi: kushiriki katika matibabu si kusaini fomu pekee, bali ni kufuata ushauri, kuuliza maswali na kurejea kwa ufuatiliaji. Afya ni ushirikiano wa pande zote, na pale upande mmoja unaposhindwa kutimiza wajibu wake, matokeo yanaweza kuwa mabaya hata kama nia ya matibabu ilikuwa sahihi.
Kimsingi kesi ya Florah Lengwana inaacha somo lenye uzito: katika mizani ya tiba na sheria, ukweli haupimwi kwa matokeo pekee, bali kwa uadilifu wa mchakato mzima wa maamuzi.
Sheria na miiko
Kwa mujibu wa Sheria ya Madaktari na Wataalamu wa Afya Na. 11 ya mwaka 2017, daktari anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kufutiwa leseni endapo atakiuka maadili ya taaluma.
Kifungu cha 40(2)(a) kinakataza daktari kwenda kinyume na miiko ya udaktari, huku kifungu cha 40(3)(j) kikimzuia kumshawishi au kumlazimisha mgonjwa kubadili maamuzi yake ya kiafya bila sababu za dharura.
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Innocent Kibadu anasema kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Maadili na Mwenendo wa Kitaaluma kwa Madaktari (2005), hususan kifungu 8.2, uhusiano kati ya daktari na mgonjwa unapaswa kujengwa juu ya uaminifu na kulinda maslahi ya mgonjwa pekee.
“Daktari anapokiuka msingi huo, anakiuka maadili ya taaluma yake. Maslahi ya mgonjwa yanamaanisha matibabu sahihi, ya lazima na yenye lengo la kuokoa maisha ya mama na mtoto, si vinginevyo,” anasisitiza.
Kwa mujibu wa miiko ya taaluma ya udaktari, daktari hatakiwi kumlazimisha mgonjwa kufanyiwa matibabu yanayokwenda kinyume na tathmini ya kitaaluma, wala kumshawishi kubadili maamuzi yake bila sababu za dharura.
Sheria ya Madaktari na Wataalamu wa Afya Na. 11 ya mwaka 2017 inaweka wazi kuwa ukiukwaji wa maadili unaweza kusababisha hatua za kinidhamu, ikiwemo kufutiwa leseni ya kazi.
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Innocent Kibadu, anasisitiza kuwa uhusiano kati ya daktari na mgonjwa unapaswa kujengwa juu ya uaminifu. “Maslahi ya mgonjwa ndiyo msingi mkuu. Hii inamaanisha matibabu sahihi, ya lazima na yenye lengo la kuokoa maisha si vinginevyo,” anasema.
ANDIKO LA: Elizabeth John , NJOMBE
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.