Hofu yatanda, wakimbizi wa Burundi wadaiwa ‘Kufukuzwa’ Tanzania

Hofu yatanda, wakimbizi wa Burundi wadaiwa ‘Kufukuzwa’ Tanzania

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
2522d516-8b6f-47c0-956f-ca2352b035d7.jpeg
​

Wasiwasi umeibuka kuhusu kurejeshwa kwa lazima kwa wakimbizi wa Burundi kutoka Tanzania, huku wengi wao wakisema hawataki kurudi nyumbani kutokana na hofu ya usalama na mateso ya kisiasa.

Manyanyaso hayo yanaripotiwa wakati Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za wakimbizi zikizuia wakimbizi kurejeshwa katika maeneo ambayo maisha au uhuru wao uko hatarini.

Hadi mwisho wa Novemba 2025, zaidi ya wakimbizi 140,000 wa Burundi walikuwa wanaishi Tanzania baada ya kukimbia machafuko ya muda mrefu nchini mwao.

Taarifa za manyanyaso ya wakimbizi wanaotoka Burundi zimeripotiwa wakati kuwakiwa na taarifa za kufungwa kwa kambi ya Nyarugusu ifikapi Juni mwaka huu, huku kambi ya Nduta iikitakiwa kufungwa ifikapo Machi 2026.

Juhudi za kuupata uongozi wa Idara ya Wakimbizi ya Tanzania, kuzungumzia suala hilo, hazijafanikiwa.

Mmoja wa wakimbizi anayeishi ndani ya kambi ya Nduta amesema, amesema kumekuwa kuwa unyanyasaji katika kambi hiyo na kambi ya Nyarugusu, ambapo baadhi ya wakimbizi wamebomolewa nyumba.

“Kuna unyanyasaji wa aina mbalimbali! Wengi wanatumia njia mbadala ya kuondoka hapa na kwenda nchi zingine hususa kwa wale wenye usalama mdogo. Huu unyama unafanyika kwa wakimbizi wa Kirundi tu. Wanaopatikana kwenye kambi za wakimbizi wa Kigoma,” amesema.

Amesema katika kambi ya Nyarugusu kati ya kanda sita zilizopo baadhi zimebomolewa makazi ya wakimbizi.

“Walianza kubomoa zone ya 13 na 12. Hizi zone zingine bado zipo Ila watu wengi wako wanatumia huu usafiri wa UNHCR na kufika mpakani na badaye wakijaliwa, kusafiri kwenda nchi zingine ambazo ni salama na zinazoweza kuwapokea.

“Hii kitu inafanywa kwa siasa kali ili ionekane kwamba watu wanaondoka kwa hiari yao wenyewe kama ilivyofanyika kwenye kambi za Warundi za zamani kwa mfano kambi ya Mtabila,” amesema.




Ameongeza, “Wakimbizi wanafanyiwa vituko, unyanyasaji wa kila aina, na kuibiwa mali zao ili kwa vyovyote waondoke wenyewe wakiona maisha ni magumu. Jinsi inavyofanyika ni kubomoa nyumba ya mkimbizi na kunembia hutakiwi kwenda kuishi pengine! Nenda ujiandikishe urudi kwenu!”

UNHCR
Ingawa maelfu wanaendelea kurejea kwa hiari, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, inasema maelfu bado wanahitaji ulinzi wa kimataifa. Takribani watu 17,000 wamesema hawawezi kurudi kwa sababu ya hofu ya usalama wao, wakiwemo wanachama wa upinzani na wanajeshi wa zamani.

Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Umoja wa Mataifa wa habari Februari 24, 2026 imemnukuu mmoja wa maofisa wake anayefanya kazi Tanzania, Bahia Egeh, akisema kuna ongezeko la malalamiko kuhusu kurejeshwa kwa lazima na hatua za shinikizo dhidi ya wakimbizi kambini.

Aidha, kumekuwapo ripoti za kubomolewa kwa makazi ya wakimbizi wakati wa mchakato wa urejeshaji na madai ya baadhi yao kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji.

Kwa sasa kuna kambi mbili za wakimbizi katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania, ambazo ni Nduta na Nyarugusu, ambapo Nyarugusu ndiyo kubwa zaidi. Wakimbizi wengi wanataka kuhamia Nyarugusu kufuatia tangazo la kufungwa kwa kambi ya Nduta mwezi Machi. Hata hivyo, hali kambini inaelezwa kuwa ngumu kutokana na kupungua kwa ufadhili wa UNHCR, jambo lililoathiri huduma muhimu kama afya.

Juhudi za kuwarejesha wakimbizi
Mwaka 2017 ilitangazwa kuwa ni salama kwa wakimbizi wa Burundi kurejea nyumbani, na makubaliano ya pande tatu yakafikiwa kati ya UNHCR na serikali za Tanzania na Burundi ili kuwezesha urejeshaji wa hiari. Hivi karibuni, juhudi zimeongezwa baada ya kukubaliwa lengo la kurejesha wakimbizi 3,000 kwa wiki mwishoni mwa 2025.

Katika miezi miwili ya kwanza ya 2026, zaidi ya wakimbizi 28,000 wamerudi Burundi kutoka Tanzania, huku 8,000 wakirejea katika wiki moja pekee—idadi inayozidi lengo la wiki. Tangu 2017, zaidi ya wakimbizi 180,000 wamesharejeshwa.

Hata hivyo, UNHCR imeeleza wasiwasi kuwa katika juhudi hizi za kasi, makazi ya wakimbizi yamebomolewa na kuwalazimisha baadhi yao kukaa katika vituo vya muda vilivyojaa kupita kiasi, huku pia kukiwa na madai ya unyanyasaji.

UNHCR imesisitiza kuwa urejeshaji unapaswa kufanyika kwa hiari, kwa usalama na kwa heshima, bila shinikizo. Shirika hilo lina dawati maalum la ulinzi kwa ajili ya kuchunguza iwapo wakimbizi wako tayari kurejea, ili kuhakikisha wanaohitaji ulinzi wa kimataifa wanaendelea kubaki Tanzania.

Kupungua kwa ufadhili pia kumeathiri huduma kambini. Kwa mfano, katika kambi ya Nyarugusu, vituo vya afya vimepungua kutoka 10 hadi viwili tu vinavyofanya kazi. Aidha, vituo vya mapokezi nchini Burundi navyo vinakabiliwa na msongamano na uhaba wa rasilimali.

UNHCR imesema itaendelea kushirikiana na serikali za Burundi na Tanzania kuhakikisha makubaliano ya urejeshaji wa hiari yanaheshimiwa, huku ikilinda haki na mahitaji ya wakimbizi katika kila hatua ya mchakato huo.

Pia soma ~ Wakimbizi 4,200 kutoka Burundi waliokuwa wakiishi nchini Tanzania wamerejeshwa nchini kwao kwa hiyari
 
tatizo hao ndugu zetu huwa wanajihusisha na ujambazi na uvunjifu wa amani kwa baadhi ya maeneo...
 
Back
Top Bottom