Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Hizi ni hoja kumi alizozitoa Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima akihoji na kushauri.
1.Kuna wimbi la utekaji, na uvamizi wa kikatili wa raia pasipo hatia wala utaratibu wa kueleweka.
2.Vyombo vya ulinzi nchini havijaeleza kushindwa kushughulikia matukio ya utekaji wa raia kwanini hatua hazichukuliwi mpaka sasa zaidi ya raia 80 wamepotea na hawajulikani walipo.
3.Je Viongozi wakuu wa serikali wangekaa kimya au wangejisiakiaje endapo wangepoteza watoto wao kwa kutekwa au kujeruhiwa kwa kutobolewa macho?
4.Kuna mabadiliko ya Mara kwa Mara ya Viongozi wakuu wa Idara ya usalama wa taifa bila kuwa na sababu za kueleweka jambo ambalo linatia mashaka utendaji wa idara hii nyeti nchini.
5.Wanasiasa wasitumie vyombo vya ulinzi na usalama kwa manufaa yao ya kisiasa vyombo viwe huru vifanye kazi zake kwa maslahi ya taifa na kwa haki.
6.Mifumo ya upatikanaji wa uongozi wa vyombo vya usalama ifanyiwe marekebisho ili kuwalinda wanapofanya vizuri na kuongeza ufanisi wa vyombo hivyo kiutendaji.
7.Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakishindwa kutekeleza majukumu yao wawajibishwe ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
8.Huenda Kuna genge la utekaji linaloundwa na Watu fulani ambo sio vyombo vya ulinzi linateka na kuumiza watu.
9.Vyombo vya ulinzi na usalama viboreshewe kimaslahi ili kuongeza ufanisi na hamasa ya kufanya kazi, vianzishiwe mifumo thabiti ya kuviwezesha kukua kiuchumi.
10.Kwanini matukio ya raia kupotea na kuumizwa hayachukuliwi kwa uzito kiasi kwamba sio binadamu ni mbuzi au kondoo?