Hoja 10 za Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu kuhusu Rais kutoshtakiwa mahakamani

Hoja 10 za Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu kuhusu Rais kutoshtakiwa mahakamani

RAKI BIG

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
394
Reaction score
459
Ado Shaibu: ACT Wazalendo tumekuwa mstari wa mbele kuiwajibisha Serikali Mahakamani. Rais alipomwondosha CAG Prof. Assad kinyume na Katiba, Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe alimpeleka Mahakamani. Pia, Rais alipomteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali asiye na vigezo vya kikatiba, nilimpeleka mahakamani.

Ado Shaibu: Kwenye kesi zote hizi, licha ya mapingamizi ya Serikali, iliwekwa bayana kuwa RAIS ANAWEZA KUSHTAKIWA akivunja katiba

Ado Shaibu: Ili kunivunja moyo, Serikali imeomba fidia kubwa ya gharama ya kesi yangu dhidi ya Rais iliyofutwa kwa sababu za kiufundi (Tsh.123,500,000). Tarehe 03 Juni 2020,

Mahakama imeniamuru kumlipa Rais Magufuli fidia ya Tsh. 445,000.

Ado Shaibu: Hata hivyo, binafsi sioni sababu ya kumlipa Rais Magufuli fidia. Kwenye kesi Rais alitetewa na mawakili wa Serikali wanaolipwa kwa kodi zetu. Hakuna haja ya mawakili hao kulipwa tena hasa kwenye kesi ya kulinda na kutetea katiba kama niliyoifungua.

Ado Shaibu: Baada ya kutushindwa mahakamani, Serikali sasa inakimbilia Bungeni kutunga sheria ya kutuzuia tusimshtaki Rais, Makamu wa Rais, Spika na Jaji Mkuu kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa 2020.

Ado Shaibu: Hawataki pia NGOs na wanaharakati wapeleke kesi za kulinda Katiba mahakamani. Wanataka wawe huru kuvunja Katiba wapendavyo.

Ado Shaibu: jambo hili halikubaliki. Hii sio nchi ya kifalme. Kila mtu yupo chini ya sheria. Kuwa Rais, Spika au Jaji sio tiketi ya kuvunja katiba halafu usiguswe.

Ado Shaibu: Kama alivyosema Mwanasheria Mkuu wa Chama chetu, ingawa CCM watatumia wingi wao Bungeni, tutaupinga Muswada huo ndani ya Bunge.

Ado Shaibu: Ni Muswada ambao, kama ukipitishwa na kuwa Sheria, utaturudisha nyuma sana kwenye mapambano ya kupigania uwajibikaji, utawala wa sheria na haki za binadamu.

Ado Shaibu: Ujumbe wetu kwa Watanzania ni kuwa hatua hii iwape sababu nyingine ya kuiadhibu CCM kwenye Uchaguzi Mkuu 2020. Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imevuruga kupindukia uchumi na haki. Zawadi pekee kwao ni kuiondosha madarakani 2020.

Imeandaliwa na:
Janeth Rithe, Naibu Katibu, Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.
07 Juni 2020.

103077166_3324151564275071_4520194417115499530_o.jpg
 
Kutoka mahakama ya mafisadi mpaka kwenye sheria za kutetea uvunjivu wa sheria na katiba ya nchi!!
 
Back
Top Bottom