PreGE2025 Hoja 6 za kwanini No Election lazima itekelezwe ikiwa Reforms hizi hazijafanyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dp800

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
2,310
Reaction score
4,714

View: https://youtu.be/--J45XU5LAs?si=_xbKbAZN1lVA2KpD

Mh. Tundu Lisu ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema ameeleza kwa undani na urahisi sana mabadiliko 6 ambayo Chadema inadai, Katika mkutano wa leo wa uliofanyika Nachingwea.

Sikliza kwenye link hiyo kuanzia dakika ya 27
Naomba CHADEMA Media mturahishie kupata nakala ya hoja hizi muhimu na ikiwezekana zitolewe nakala nyingi zisambazwe kila mahali makanisani, misikitini na maeneo yote ya wazi zibandikwe ili watu wote watambue Chadema inapigania jambo gani.

Wengi wanawasiwasi NO ELECTION ni ngumu kutekelezwa kwa sababu hawajui uzito na umuhimu wa REFORMS zinazohitajika au kudaiwa na Chadema

Kwa Muhtasari Reforms hizo ni
1. Tume Huru ya Uchaguzi
Chadema inataka Tume Huru ya Uchaguzi ambayo viongozi wake wakuu na watendaji wake wote hawateuliwi na Raisi wa Tanzania ambaye pia ni mgombea kwa tiketi ya CCM (wawe watu huru na wasiteuliwa na upande wowote unaoshindana katika uchaguzi)

2. Kura Feki
Chadema inataka utaratibu utakao ondoa kura Feki kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura. Utaratibu huo utapatikana ikiwa Vyama na Wagombea wataruhusiwa kuthibitisha taarifa za tume (database) inayobeba taarifa za wapiga kura na uhalali wa wapiga kura walioandikishwa Katika daftati la Tume. Kwa utaratibu wa sasa ni tume pekee ndio inajua wapiga kura walioandikishwa. Udhaifu huu unapelekea watumishi wa tume, Polisi au CCM kuingiza kura feki kwenye vituo vya kura maana hata wafu au watu hewa wamo kwenye daftari la Tume.
Lakini kingine Mh. Tundu Lisu ametaka sheria iseme ni marufuku mtu kuingia na kitu/vitu vinavyowezesha kura feki kuingizwa kituoni

3. Wagombea Kuenguliwa
Chadema inataka wagombea kutokuenguliwa kwa sababu zozote zile iwapo mtu huyo amekidhi sifa zilizoainishwa katika katiba za mtu kuwa kiongozi. Sambamba na hilo Mh. Lisu amekazia kwamba Sheria iseme ikiwa hakuna mgombea kinzani katika nafasi husika basi uchaguzi wa eneo hilo usimame hadi pale wagombea zaidi ya mmoja wamepatikana. Hii ni kuhakikisha hakuna mgombea anapita bila kupingwa ambayo ilikuwa janga kubwa uchaguzi wa 2020.

4. Fujo kutoka katika Vyombo vya Dola (Polisi, RC, DC, Usalama wa Taifa, Jeshi, Migambo n.k)
Chadema na wapinzani wanafanyiwa fujo na vurugu sana wakati wa kampeni (kupigwa mabomu, kuzuiliwa fomu n.k) Hii inaathiri ufanisi wa kampeni zao na michakato mingine katika uchaguzi. Sheria ikataze Polisi kuingilia kampeni na kuwa vikwazo kupata fomu na nyaraka nyingine muhimu za uchaguzi. Hapa Lisu alitoa mfano namna FFU walivyozuia wagombea wa upinzani kuchukua fomu katika Jimbo la Ruangwa kwa kuwapiga mabomu na virungu hadi kupelekea Waziri mkuu Kasimu Majaliwa kupita bila kupingwa.

5. Kanuni za Mawakala wa Uchaguzi
Chadema inasema kanuni za kuwasimamia mawakala wa wagombea zimewekwa kama mtego wa kuangusha vyama vya upinzani. Mfano sheria ya sasa inataka mawakala waapishwe na Wakurugenzi. Mazingira wanayo kutana nayo mawakala wa upinzani ni magumu hivyo yanapelekea wengi kutokutimiza wajibu wao na kutoa mwanya kwa CCM na serikali kuiba kura za wananchi. Sheria iondoe na kuzuia vikwazo vyovyote vinavyosababisha mawakala kushindwa kutimiza wajibu wako kabla, wakati na baada ya kupiga kura.

6. Mauaji ya Viongozi wa Upinzani.
Tundu lisu amehoji matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa viongozi wa Upinzani. Akitolea mfano Mauaji mgombea wa Manyoni, watu waliouliwa Pemba kisa uchaguzi na maeneo mengine mengi ya nchi hii.
Chadema inataka Mauaji ya viongozi na wanachama wa upinzani yakomeshwe kwa kuweka sheria zinazozuia vyombo vya dola kuingilia uchaguzi. Pia Chadema haiko tayari kuingia katika Uchaguzi ambao ni kama Kafara kwa wanachama wake ili kuifanya CCM iendelee kuwa madarakani.

Mwisho Tundu Lisu amehoji
1. Hizi hoja chadema inazozipigani ni mbaya namna gani hata zisitekelezwe?
2. Nani anachukizwa na hoja hizo na kwanini mambo haya yasifanyiwe kazi?
3. Nani huyo anayefurahishwa na mauaji ya watanzania au kura feki katika chaguzi zetu?

Zaidi sana Tundu Lisu amesema hoja hizo sio za Chadema Pekee yake.
Tume mbalimbali zimeundwa na maraisi mbalimbali wa Tanzania nao pia waliyaona haya na kutaka mambo haya yafanyiwe kazi.

Hivyo basi Chadema imedhamiria kuzuia uchaguzi wa 2025 ikiwa mambo hayo hayatafanyiwa kazi.
 
..Reforms ni moja nguzo za 4R za Rais Samia, sasa kwanini kuna shida kutekeleza Reforms ktk mifumo yetu ya uchaguzi?
 
Hizi hoja zikizingatiwa, Tutakuwa na The best uchaguzi.
 
Umesahau utekwaji,
Wakurugenzi kufunga ofisi
Upinduaji wa matokeo
 
Watu wengi waliotimamu kichwani hawashiriki uchaguzi kwa sababu ya kasoro hizo.Zikifanyiwa kazi idadi kubwa watajitokeza kupiga kura.
 
Back
Top Bottom