KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,250
- 5,509
Ninatambua uthubutu na uimara wa serikali ya CCM ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli katika kulinda maslahi ya umma hasa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma zinazotokana na kodi zetu. Juzi, wakati Rais alipokuwa anawahutubia wakazi wa Geita alisikitishwa na kitendo cha baraza la madiwani kupitisha bajeti ya shilingi za kitanzania bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa mitaro na wanaomba kiasi hicho kutoka serikali kuu. Hakika kitendo hicho kilikusikitisha sana Mhe.Rais kwa matumizi hayo yasiyo ya msingi yasiyojali maslahi ya umma ambayo daima umekuwa ukiyapa kipaumbele.
Nilipokuwa natafakari kitendo hicho cha Mhe.Rais kinachoonesha kujali watu na kuheshimu kodi za watanzania hasa nidhamu ya fedha za umma na matumizi yanayojali, nikapata wazo la serikali kuliangalia suala la utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa vinavyopokea ruzuku na kusitisha au serikali isitishe ruzuku kwa vyama vyote vinavyopewa ruzuku lakini vinasusa kushiri uchaguzi. Kwa nini ‘option’ mojawapo kati ya hizo?
Ruzuku si ahsante ya serikali kwa chama kilichoshinda, ahsante/pongezi inatolewa mara moja na ni wakati uliposhinda. Ruzuku ni fedha za kukisaidia chama katika ujenzi wa siasa bora za kidemokrasia na ni endelevu. Sasa kama serikali inatoa ruzuku kwa vyama kwa nini wasusie uchaguzi wakati ruzuku inatolewa ili kuimarisha siasa safi?
Kwa mantiki hii, serikali haina budi kutekeleza hoja mojawapo kati ya hizo mbili ambazo ni: kusitisha ruzuku kwa vyama vyote vyenye kupokea ruzuku au kusitisha ruzuku kwa vyama vinavyopokea ruzuku lakini wanasusia kushiriki uchaguzi. Kwa nini ruzuku isitishwe?
Kama nilivyokwisha sema, maslahi ya umma yanalindwa kwa nidhamu nzuri na matumizi sahihi ya kodi zetu na ruzuku si gawio la kampuni binafsi kwa vyama vya siasa ila ni kodi zetu. Kama vyama vyama vinapokea ruzuku lakini hawashiriki uchaguzi, nidhamu na matumizi mazuri ya kodi zetu inatoka wapi hapo? Je, ruzuku inatumika kufanyia nini ?
Serikali ya JPM imejipambanua katika nidhamu ya kodi zetu ikiwepo ruzuku, Mhe. Rais tunaomba suala la ruzuku liangaliwe kwa jicho la tatu.