KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,250
- 5,509
Wafute Leo hii. Wasikawie.Huu ni ufujaji wa kodi zetu mkuu, vyama vinapewa fedha badala ya kutimiza majukumu yao ya kisiasa wanatumbua tu, na chaguzi hawashiriki.
Hivi ndivyo vyama hewa mkuu, fedha zinatoka,hazitumiki kwa malengo husika. Msajili awalime barua wajieleze kwanini wasinyimwe ruzuku, kwani hawatimizi malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao.Wafute Leo hii. Wasikawie.
Ingependeza zaidi tungewakumbusha waliozuia vyama kufanya harakati za kujitangaza, kwani kushiriki uchaguzi bila kujitangaza wakati chama tawala kinafanya hivyo, ni kuondoa mazingira ya ushindani halali.Kama vyama vyama vinapokea ruzuku lakini hawashiriki uchaguzi, nidhamu na matumizi mazuri ya kodi zetu inatoka wapi hapo? Je, ruzuku inatumika kufanyia nini ?
HakikaCcm ndio watakuwa wa kwanza kuumia ruzuku ikisitishwa.
Naunga mkono hoja, vyama susa susa na vyama zira zira, visipewe ruzuku!, tena mimi nilishauri ruzuku kwa vyama vya siasa ifutwe kabisa Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadiRuzuku si ahsante ya serikali kwa chama kilichoshinda, ahsante/pongezi inatolewa mara moja na ni wakati uliposhinda. Ruzuku ni fedha za kukisaidia chama katika ujenzi wa siasa bora za kidemokrasia na ni endelevu. Sasa kama serikali inatoa ruzuku kwa vyama kwa nini wasusie uchaguzi wakati ruzuku inatolewa ili kuimarisha siasa safi?
Kwa mantiki hii, serikali haina budi kutekeleza hoja mojawapo kati ya hizo mbili ambazo ni: kusitisha ruzuku kwa vyama vyote vyenye kupokea ruzuku au kusitisha ruzuku kwa vyama vinavyopokea ruzuku lakini wanasusia kushiriki uchaguzi. Kwa nini ruzuku isitishwe?
Kama nilivyokwisha sema, maslahi ya umma yanalindwa kwa nidhamu nzuri na matumizi sahihi ya kodi zetu na ruzuku si gawio la kampuni binafsi kwa vyama vya siasa ila ni kodi zetu. Kama vyama vyama vinapokea ruzuku lakini hawashiriki uchaguzi, nidhamu na matumizi mazuri ya kodi zetu inatoka wapi hapo? Je, ruzuku inatumika kufanyia nini ?