SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Unasikia mwamba anaitwa Rodri baasi. Unajua hii mashine, jina tu linambeba. Mara unasikia Zico, Pele, Garincha, Kaka, Socrates, Romario, Ronaldinho, Bebeto. Jina moja tu umemaliza kazi, unajua unazungumzia nani. Unaweza ukaishi maisha yako yote haujui jina lao lingine na hautakutana na mwingine mwenye jina kama lake.
Sisi sasa, star kabisa ila utasikia Bakari Nondo Mwamnyeto! Utasikia Kibu Denis Prosper, whhhy? Eti Fiston Kalala Mayele! Mara Clatous Chota Chama! Chota ya nini sasa? Kuna Mayele wangapi tunaowajua hadi uone ulazima wa kuongeza Kalala?
Hivi kwa nini tunapenda kuita watu majina matatu ilhali hakuna ulazima wa kufanya hivyo?
Nashauri wachezaji wa kibongo wakishajipata na nyota ikaanza kuwawakia, wasipunguze tu umri, waende pia kwa babu na bibi zao wapewe jina tofauti kabisa la "kilugha". Itawasaidia sana katika branding.