N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Kumekuwa na hoja miongoni mwetu Watanzania kuhusu matumizi ya lugha za kigeni hasa Kiingereza kutumika kama kipimo cha mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili. Je, hoja hii ikoje? na ina ukweli kiasi gani?
HOJA NAZOWAZA ZITHIBITISHE KWAMBA KUJUA KIINGEREZA SIO KUWA NA AKILI NI KAMA IFUATAVO:
- Lugha ya Kiingereza ni njia tu ya mazungumzo kama lugha nyingine yoyote ya hapa nyumbani au ya kimataifa.
SASA NI BAHATI MBAYA HAPA KWETU TANZANIA
- Watu wanaozungumza Kiingereza wanachukuliwa kama wajanja,na wenye uwezo wa akili kiasi kwamba wanapewa kipaumbele kwenye mambo mengi hata ajira lakini ukweli ni kwamba umahiri katika Kiingereza au Lugha yoyote anuai hakumaanishi kwamba wewe una akili sana kuwazidi wasiomudu kuzungumza lugha hiyo unayoiwezea kwa ufasaha.
TUKILINDE KISWAHILI ila pia TUSIKIBEZE KIINGEREZA maana tayari kina nguvu na ishakuwa lugha ya dunia.

- Lugha unayoimudu haifasili usomi wako.
- Bila shaka mtu anaezungumza lugha nyingi anachukuliwa kama mwerevu na anayeweza kwa sababu anaweza kuwasiliana na watu wengi lakini hicho sio kipimo kwamba maudhui ya anachowasiliana nao kinaakisi uwezo wake wa akili.
- Hata katika historia wafalme walikuwa na maafisa ambao walijua kuzungumza zaidi ya lugha moja lakini hawakuwa watu wenye akili kuwazidi wengine.