HOJA: Je, umahiri wa lugha ya kigeni ni kipimo cha akili?

Waambie waelewe.
 
Twende mbele turudi nyuma jamani kujua lugha ya kigeni ni raha ila kuhusiana na uwezo wa akili hii haikubaliani moja kwa moja ila ina uhusiano flani
 
Kumekuwa na hoja miongoni mwetu Watanzania kuhusu matumizi ya lugha za kigeni hasa Kiingereza kutumika kama kipimo cha mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili. Je, hoja hii ikoje? na ina ukweli kiasi gani?
Kama sio akili kwa nini vipanga wa darasani ndio waliokuwa wanakuwa mahiri pia kwenye somo la Kiingererza?

Sijaona mtu anapata 15% somo la Biology, History au Geograpghy, halafu 95% kwenye English.
 
Ndiyo maana kunakuwa na si ntofahamu pale MTU anapofundishwa kwa Kiingereza miaka mingi tu mpaka akapata PHD halafu asijue Kiingereza.....
 
Mimi Kingereza sijui, lakini kiakili nina uwezo mkubwa sana.
Sasa hiyo ndo hoja niliyoibua hapa mkuu...ukweli ni kwamba kumekuwa na upotoshaji miongoni mwetu kwamba mtu asipofahamu kuzungumza au kuandika vema kiingereza basi eti hana akili kamili. Huu ni 'upopoma' (samahani kwa hilo neno mapopoma) kudhani kwamba kiingereza ndio kipimio cha akili ya mtu.
 
Nikipata sababu ya Kisayansi zaidi juu ya hili naweza Kukuelewa ila kwa sasa na ulichokiandika hapa sijakuelewa japo nina wajibu wa Kuheshimu mtizamo na mchango wako huu pia.
 
Hivi ukijua kiingereza.. unapokuwa unawaza kimoyo moyo .. huwa unawaza kwa kiingereza!? Au unawaza kwa Kiswahili.. πŸ™‚??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…