Hoja kuwa Yanga hawawezi mechi za kimataifa imekufa kifo che mende, wamebaki na kauli ya Yanga kucheza kombe la loser!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kabla ya Yanga kutinga hatua ya makundi na sasa kutinga robo fainali, hoja kuu ya makolo ilikuwa ni Yanga hawawezi kimataifa isipokuwa wao tu.

Sasa baada ya Yanga kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Shirikisho, hoja yao kubwa imekuwa hilo ni kombe la loser kanakwamba hiyo sio michuano ya kimataifa ambayo walidai Yanga haiwezi huku wao wenyewe wameshiriki mara kadhaa kwenye hiyo Michuano ya Shirkisho na safari yao kuishi njiani pamoja na kuloga (ushirikina).

Hofu yao kubwa kwa sasa ni iwapo Yanga ataingia nusu fainali wakati wao wameishia robo fainali kwani tutakuwa tumewaziba midomo ingawa hawatakosa cha kusema (watakuja na habari za mwaka 93 na nyingine za aina hiyo).

Tutarajjie hoja ya kombe la loser kushika kasi wakati wao wenyewe hawajawahi kulibeba na zaidi wanalitamani na ndio maana hata kule Bondeni walitia Taifa doa wakitafuta hilo kombe la loser.
 
Nasikia jezi za kuingia robo fainali za utopolo zipo sokoni na zinaelekea kwisha
 
Yanga inabeba kombe la ligi second time,

Yanga inabeba kombe la Azam Federation second time,

Yanga inajipigia Simba kama Ngoma April mikia hawatoki,

Yanga Iko Robo fainali Shirikisho ambapo Simba waliita Yanga wa matopeni wao wa kimataifa,

Yanga imeongeza wawiwandi hatari wawili , Natural strikers Musonda na Mzize kumsaidia Mayele, wanapiga magoli tu! Simba Kuna Boko! Yanga imeongeza beki mkali Baka, Simba haina mbadala wa Inonga , Onyango, Kapombe na Zimbwe wakiumia au kucheza chini ya Kiwango Simba Chali!! Moloko ni Winga na anafunga, Feisal hahitajiki Tena,

Sasa Yanga mwakani tunarudi kibabe kombe la Klabu bingwa Afrika huko Makolo wanakojisifia kushiriki wakati wao si mabingwa wa nchi yoyote, hii kanuni iliyowaingiza Simba michuano ya klabu bingwa ifutwe CAF , kama timu si bingwa nchini mwake icheze Shirikisho tuone Simba watacheza kombe Gani!
 
Unajua kimataifa kweli ww Caf champions league ndio kimataifa sio Caf confederation cup.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…