Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Hoja: Mbunge awe Mkuu wa Serikali katika Wilaya.
Katika Katiba Mpya, Nafikiri kuna umuhimu kufanya mageuzi ya muundo wa utawala na uongozi wa kisiasa nchini. Mbunge wa kuchaguliwa, awe ni Mkuu wa serikali katika Wilaya, aongoze kuanzia baraza la Usalama Wilaya, (Kamati ya ulinzi na Usalama). Vichache hivyo mkuu wa Mkoa apatikane kwa kuchaguliwa na ndie awe mkuu wa serikali ya mkoa. Hili litaondoa mkanganyiko ulipo sasa katika nchi yetu kutumik miundo miwili ya kutawala.
Mfano, Kuna miundo miwili inaongoza serikali katika nchi moja. Kwanza ni kuanzia Mwenyekiti wa Mtaa/Kitongoji ni Mkuu wa serikali ya Kitongoji/Mtaa, Diwani wa Kata ni Mkuu wa Serikali ya kata. Pili ni kuanzia kwa Mkuu wa Wilaya ambae si wa kuchaguliwa anakuwa ndie mkuu wa serikali, wakato huo katika Wilaya hiyo hiyo kuna kuwa na Mbunge ambae ni waluchaguliwa akiongoza watu na kuwakilisha matatizo/mahitaji ya watu lakini hana uwakilishi wa moja kwa moja kwa mkuu wa nchi ambae watu wamemchagua (rais). Badala yake Rais anawakilishwa na Mku wa Wilaya/Mkoa ambae hana uhusiano wa moja kwa moja na wananchi.
Hili linaleta pengo la Wananchi kumfikia Rais wao. Lakini pia linaongeza gharama ya uendeshaji wa serikali kwakuwa kuna serikali mbili ndani ya nchi moja. Yaani kuanzia Mtaa hadi kata kuna serikali y kuchaguliwa na wananchi ambayo inafanya kazi moja kwa moja na Wananchi hao. Pili kuanzia Wilaya kuna serikali mbili moja imechaguliwa na wananchi na inawakilisha wananchi, lakini inakatika uwakilishi wake kwakuwa haimfikii Rais kama mwakili wa wananchi waliomchagua rais, inamegeka na kuelekea Bungeni. Badala yake Rais ametuma mwakilishi wake (kisiasa tu) ambae hana mizizi kwa wananchi na hawafiii wananchi walipo, ana udola tu anaitwa Mkuu wa Wilaya/Mkoa, Kama ni uwakilishi wa rais kiserikali ulitakiwa kukomea kwa Mkurugenzi. Cheo hiki cha udola wa DC na RC kilitakiwa kubebwa na kutumikiwa na Mbunge wa kuchaguliwa kama nchi zingine wanamuita Gavana. Anakuwa na full control ya Polisi Wilaya, chini yake anakuwepo mtendaji ambae ni Mkurugenzi atakayepatikana kwa kuomba kazi hiyo kupitia mchakato wa kiutumishi katika Wilaya/Mkoa.
Kwamantiki ya mabadiliko hayo, Majimbo yatafutwa na badala yake tutakuwa na Mbunge wa Wilaya, Nafasi za DAS na RAS ambazo leo ni za kisiasa tu, zinafutwa. Kazi zao atazifanya Mkurugenzi. Vigezo vya ubunge vitabadilika, viwe kuanzia shahada moja na kuendelea, kuliko iliyo sasa ambapo sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika kiswahili tu, Yaani mtu yoyote anaweza kuwa Mbunge, kisha anakwenda kutunga sheria bungeni ambazo sheria hizo, zinataka Mtu anayetakiwa kwenda kuzitumia yaani mwanasheria, lazima asome shahada ya kwanza ya sheria miaka mitatu/minne, kisha aende kusoma shule ya sheria miaka mitatu, akafanye mazoezi kwa vitendo mwaka mmoja ndipo atunukiwe leseni ya kuzutumikia sheria zilizotungwa na mambumbu wanaojua kusoma na kuandika tu kisha wakawa Wabunge wa Tanzania.
Naleta hoja.
Na Yericko Nyerere