HOJA: Mbunge awe Mkuu wa Serikali katika Wilaya

Yeriko ameharibika kabisa siku hizi! Ujinga gani huu unapendekeza?
Lengo kubwa la kuwa na Bunge, serikali na Mahakama ni CHECKS AND BALANCE.

Sasa ukishakuwa na Mbunge halafu ndio huyo huyo Serikali, hiyo checks and balances itafanyikaje.

Na kiuhalisia siku zote, serikali ni SHETANI takataka linaloumiza wananchi, ni lazima kuwe na namna ya kuli-hold accountable hasa kupitia Bunge
 
Hii italeta ukabila. Iwapo akija hata Askofu, au Captain wa Yanga, au Mganga Mkuu, au hata Bwana Shamba, lazima tu asiye wa pale ataitwa mgeni au atadharaulika, watu kama Wasukuma na Wanyakyusa lugha yao ndiyo itakuwa lugha rasmi. Wakati mimi niko Middle School darasa la 6, Headmaster alikuwa Mchagga, Askofu alikuwa Mzungu, Bwana Shamba alikuwa Mhaya na Captain wa timu ya Mwadui alikuwa Mjaluo. Baadaye nikarnda Tanga kwa Wazigua na Waislamu, huku wakiniita Mnyamwezi. Nikaajiriwa Mamlaka ya Korosho Newala baada ya kupita JKT Mlalo. Hiyo Tanzania, wanachotaka CHADEMA wajitawale Kikabila kwa sababu wanajiona ni bora na wanatengwa na Waranzania. Tusikubali.
 
Mkuu LGF wewe ni GT humu JF na kutokana na historia yake unafahamu fika kuwa leo ukabila umepungua kwa asilimia 90 ukilinganisha na wakati huo. Wakati huo Newala wamakonde walikuwa asilimia 99. 9 na hao waliobaki ni wafanyakazi. Kwa hiyo usiogope, maana utaratibu huo utaleta maendeleo ya uhakika, kwani kila wilaya inapata bajeti yake kutoka Serikali Kuu, hivyo kwa kuwa Serikali ipo kwa wananchi sehemu husika hakuna fedha itatoka kwenda nje ya Wilaya hiyo. Mkuu tumeona na tunashuhudia fedha za miradi za wilaya husika zinapigwa panga na kwenda kuendeleza kwa wahusika wa wilaya ingine wanakotoka. Mkuu mjenga Nchi ni Wananchi ; na hivyo hivyo kwa wilaya - mjenga wilaya ni wananchi wa Wilaya husika.
 
Big-up Mkuu, huwa napenda kusoma watu wenye uchambuzi hai kama huu. Ahsante
 
Hilo nalo mkalitizame katika Katiba Mpya badala ya kulihamishia hadi chini kwenye Wilaya na Halmashauri.
Rais ni mkuu wa Executive lakini ni mbunge, na ni sehemu ya mahakama....[emoji1787]
 
Iko vizuri hiyo hoja, haina maana kuwa na kiongozi wa kuteuliwa.
 
Yeriko unafirisika kifkra vibaya sana..

Uharisho gani unaandika.. Shida ya wachambuzi wasiasa kutokusoma siasa
 
Jua kwanza maana ya SERIKALI ndo utafakari kama unayemnyenyekea akupe KURA kama unaweza kumuwajibisha!!
 
Sasa ndugu hapa ni sawa na Nchi kuingia katika mfumo wa jimbo??, Hivi Zitto awe mkuu wa serikali hawezi kutangazia umma kuwa kasulu ni Nchi inayojitegemea?.
 
Sio kila mwanasiasa ni kiongozi tambua hilo!
Ikiwa hivyo wilaya nyingi zitakuwa na viongozi manunda haswaaaa!
 
ni hoja nzuri, lakini chawa wataku

Ni hoja nzuri, lakini chawa watakula wapi?
 
Kwenye hili umechemka. Lazima tutofautishe kati ya serikali na wawakilishi wa wananchi.
 
Rais sio mbunge ila nisehemu ya bunge
 
Uko sahihi yaani 50 to 60% ya Kodi ibaki kuendeleza sehemu kodi ilipokusanywa! Juzi karibu nitoe machozi eti hospitali ya mkoa Geita haina dawa kabisa halafu ina wafanyakazi 12 tu wakati mkoa huu hutoa 60% dhahabu exports jumla 2022 ni zaidi ya tripni 6! Kwa nini hata trioni 1 isibaki Geita? Ni akili kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…