HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Wewe mwendawazimu acha kuidharirisha serikali yetu.serikali hii ya awamu ya tano pesa ipo.Wewe mwendawazimu na rais Magufuli nani anajua pesa ipo au haipo?nakuonya usirudie tena ujinga huu
 
Hopeless comment ever!
 
Kiufupi sisi wa hali ya chini tuko pamoja na rais Magufuli.

Kwa hio watu wachache wakimlaumu Magu kwa sababu hajafungia watu ndani basi isionekane kwamba ni watu wote.

Wengi wetu tusipotoka hatuli.
Iweje tuache kuwa upande nmoja na Rais magufuli?
Kwani rais ndo alikutuma umasikini au ndiye alikuketea umasikini?wewe kazurule huko eti unatafuta riziki uki coronwa huko watu wanaochapa kazi za kutengeneza majeneza lazima wakupige hela
 
Acha uongo na propaganda Mzee. Marekani kama nchi haijaamua ni lini wananchi watarudi makazini wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka. Huo uliousema ni uongo. In fact Wamarekani wengi, kwa mujibu wa polls/surveys wanapinga kuruhusu watu kuchangamana sasahivi wakati maambukizi yakiendelea kukua. True, ni Trump ndiye aliyeleta hadharani pendekezo lake kuwa watu warudi kazini mapema kuliko Wanasayasi wake wanavyoshauri. Kwahiyo acha kupotosha kwamba eti "hata Marekani" wanafikiria ... In fact, hata mjumbe wa "task force" ya Coronavirus ya serikali ya Marekani Dr. Fauci amesema kitakachoamua ni lini utaondolewa mwongozo na sharti la "social distance" ni Coronavirus yenyewe, na siyo mtu mwingine yeyote kwa hisia zake. Acha uongo Mzee.
 
Kiufupi sisi wa hali ya chini tuko pamoja na rais Magufuli.

Kwa hio watu wachache wakimlaumu Magu kwa sababu hajafungia watu ndani basi isionekane kwamba ni watu wote.

Wengi wetu tusipotoka hatuli.
Iweje tuache kuwa upande nmoja na Rais magufuli?
Umesema kweli mkuu, yani ufungwe usife kwa corona lakini familia nzima ife kwa njaa?
Watanzania wengi tunatafuta pesa ya leo tukalipie deni la jana ili tukope tena kwa mangi kwa ajili ya kula leo. Ukitufungia tutakufa na watu wengine maji mpaka wakachote kwa jirani
 
Kama hutaki kutoka nje unaogopa corona si unaamua mwenyewe tu kwani mpaka uambiwe na raisi?
 
Yote tisa katika hatua na mikakati mbalimbali ya kuzuia kirusi cha korona kusambaa nchini, la kumi ni juhudi, dhamira na umakini wa kila mwananchi kufuata ushauri wa wataalamu. Si Rais, au mtu yeyote yule atakusimamia ili ujiweke katika hali ya kinga.
 
Ndugu Watanzania, Mungu apewe sifa, Matangazo yoyote Yale hayatasaidia kabisa ikiwa Mungu muumba mbingu na Dunia hatakuwa pamoja nasi kama watanzania, kama kuna Mtanzania aliweka mgomo wa kumwombea Raisi basi muda huu asiweke mgomo wa kuombea Tanzania yetu, Kwa msaada wa Mungu tutamshinda Corona
 
Kweli kabisa ujue hata nch za dunia ya kwanza zilifunga nchi zao baada ya kuona ugonjwa umesha ingia ndani na umekua mkubwa Sasa fikiria Kama unajua kabisa ndan huna mripuko kwann ufunge mipaka unachotakiwa ni kuakikisha mgonjwa haingii ndani kwa kuweka ulinz imara mipakan wanao ingia wanapimwa na kukaa karantin siku kum na nne baada ya Apo wanaenda mitaan il huu ugonjwa soon utasambaaa Mana juzi MBOWE kajua kabisa mwanae anaumwa korona na mtoto alikaa nae kwa muda wa siku kumi na tano lakin yeye na upumbafu Wake kaenda kuita press conference kaongea kamaliza et ndo anasema anaenda kukaa karantin huo si ujinga wa makusud
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu wakati mwengine mambo unayotetea ni magumu sana.
Kwanza eleza kwanini baadhi ya nchi umeweka idadi ya watu na baadhi ya nchi hujaweka idadi ya watu wa nchi hiyo.

Kuchagua Nigeria and Ethiopia and DRC kuweka idadi ya wagonjwa na idadi ya watu inaonyesha upo DISHONEST. Ungeweka nchi zote na Idadi ya watu na idadi ya wagonjwa. Halafu umeona South Africa? Idadi ya watu? Idadi ya wagonjwa?

Kaka sayansi inataka objectivity.
Kiufupi ni kuwa Tanzania INAFICHA takwimu za Watu wenye Corona waliopimwa. Lakini pia Tanzania hakuna vipimo mpaka juzi tulipopata vya Jack Ma. Huwezi kujua idadi kama hupimi.

Mwisho kauli ya Rais kanisani jumapili iliyopita ni kauli mbaya Sana kwa Kiongozi na imeaminiwa na baadhi ya watu. Watu watakufa sana
 
Tuonyeshe wagonjwa wako wap CHADEMA wa ufipa naona mnalazimisha kila Kiki iwe upande wenu IV Kat ya maguful na mwenyekit wenu Nan mjinga Zaid MBOWE kakaa na mwanae siku kum na tano nyumbani mtoto anaumwa wameenda kumpima wamemkuta na korona MBOWE badala ya kukaa ndani katoka kwenda kufanya press conference na waandish wa habari kazunguka kasalimiana na watu alafu ndio anakuja kutangaza et anakaa karantin huu si umaku huu au aliamua kusambaza makusudi Yani CHADEMA wanafanya kila kitu ili wapate attention hawajali afya za watanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi huu. Mungu ametupa akili za kukabili mazingira. Fuata masharti ya madaktari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…