HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Kufunga mipaka sio kujikinga na korona ingekua ivyo mpaka sasahivi urus isingekuwa na mgonjwa Mana waligunga mapema Sana Yan kabla hata haujasambaa Sana kutoka China
I'm too young to understand. Kwa nini mheshimiwa afanye Bahati nasibu na uhai wa raia wake wapendwa? Kitu kinachofanywa na Rais wetu mpendwa ni mikakati ya kuua ndege wawili kwa jiwe moja na inabidi tusuport na kufuata kile wizara ya afya inachoelekeza.. Na soon tu tutaanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi mwaka 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmk tatizo kubwa ni uwaxi

Nilipoandika makala yangu ya ILIYOPITA kuhusiana na ugonjwa utokanao na virusi vya korona (COVID-19) Tanzania ilikuwa haijtangaza kuwepo kwa mgonjwa yeyote nchini na kuwa makala ile ililenga katika kutoa shime ya kuwahi ugonjwa huo. Nchi zote zilizowahi kuutangaulia ugonjwa huo na kuchukua hatua kali mapema wameweza kudhibiti kusambaa kwake na hata kupunguza kasi ya maambukizi (rate of infections). Nchi zilizochelewa kuchukua hatua hizo au zimechukua hatua ambazo ni za taratibu sana zimejikuta leo hii zikihangaika kuokoa na kulinda maisha ya wananchi wao. Italia, Ufaransa na Uingereza kama ilivyo Marekani na Irani ni nchi ambazo zote leo zinajikuta zinakimbizana na muda. Muda hauko upande wao.

Kwa Tanzania hadi hivi sasa kuna kitu kinachoonekana si cha kawaida (an anomaly). Nchi zote ambazo zimepata wagonjwa wa kwanza tumeona idadi ya wanaoambukizwa ikiongezeka kwa kasi kubwa (exponentially). Karibu mwezi mmoja nyuma (Februari 15) Marekani ilikuwa na wagonjwa 15; leo hii Machi 26 Marekani ina wagonjwa karibu 70,000. Hii ni nyuma ya China tu na Italia. Kasi hiyo ya kusambaa kwa ugonjwa huu imeonekana karibu nchi zote ambazo ugonjwa huu umejikita. Kwa Afrika ni Afrika ya Kusini ambayo inaonekana ugonjwa huu kusambaa kwa kasi (sasa hivi wao wana kesi zaidi ya 900)

Je, namba zetu zinaweza kuaminika?
Nimesema hapo juu kuwa hali katika Tanzania inaonekana si ya kawaida (an anomaly). Kwamba, kweli nchi yetu inaweza kuwa na wagonjwa 13 tu wakati watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida? Je inawezekana serikali inaficha hali halisi na kuwa labda Rais Magufuli hataki watu waone kuwa Tanzania ina wagonjwa wengi? Ukifuatilia mitandao ya kijamii unaweza ukaamini hili. Lakini hiki “kinachoonekana” ni lazima tukipime (kwa tulio pembeni) kwa kulinganisha na nchi nyingine kama za kwetu. Hadi hivi sasa inaonekana ugonjwa wa COVID-19 haujalipuka kwa kasi kubwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Kufikia leo kwa baadhi ya nchi za Afrika hali ya wagonjwa (na namba za wagonjwa wapya kwenye mabano) ni kama ifuatavyo:

Nigeria (yenye watu milioni 190) - 51

Rwanda – 41

Kenya 31 (3)

Madagascar (4)

Zambia – 16 (4)

Uganda - 14

Ethiopia (yenye watu milioni 105) - 12

Congo DR (yenye watu milioni 81) – 4

Hivyo, tukiangalia takwimu hata za majirani zetu na nchi nyingine tunazoshabihiana nazo kwa mambo mengi utaona kuwa kasi ya maambukizi bado si kubwa na kama alivyosema Waziri Ummy Mwalimu leo ni kuwa wengi wa wagonjwa hawa ni wale waliopata COVID-19 wakitokea nje. Kwa hiyo, hatuna budi kukubaliana na kile tunachokiona; ugonjwa huu ni tishio lakini kwa nchi hizi za kwetu haujaweza kusambaa kwa haraka katika jamii (community spread). Hofu ya ugonjwa huu kusambaa kwa haraka ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu.

Hatua Zilizochukuliwa Zinatosha?
Hadi hivi sasa serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa haya maambukizi ya ndani kwa ndani kwenye jamii hayatokei. Kufungwa kwa shule, vyuo na kutoa elimu ya usafi na kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima ni njia sahihi. Katika mazingira ya kawaida tulitarajia baada ya Isabela kugundulika kule Arusha tungeona mlipuko Arusha lakini hilo halijatokea. Katika mazingira tunayoyaona kwenye nchi za wenzetu mgonjwa wa kwanza anapopatikana tu basi kuna uwezekano wa kuibuka kwa wagonjwa wengi zaidi.

Na namna pekee ya kuwapata wagonjwa hao ni kuchukua vipimo kwa watu wengi kwa kadiri inavyowezekana. Hili nalo Waziri Mwalimu amelielezea leo vizuri. Kwamba serikali inafanya vipimo na kuongeza uwezo wa kupima kwa haraka. Hii yote inasaidia kuweza kujua ni sehemu gani ya watu katika nchi wanaweza kuwa wameupata ugonjwa huu.

Bahati Nasibu ya Magufuli
Ni kutokana na hili Rais Magufuli – ambaye ni mwanasayansi ameona kuwa kwa sasa nchi nzima si lazima ifungwe kama walivyofanya nchi nyingine. Amewataka Watanzania kuzingatia kanuni za usafi na kupunguza migusano isiyo ya lazima lakini wakati huo huo kuendelea na shughuli zao. Hoja hii si kwa Magufuli peke yake; tumeona hata Marekani kuna mjadala mkubwa wa kutaka watu waanze kurudi makazini ifikapo Pasaka kwani uchumi wao hauwezi kwenda bila watu kurudi makazini. Hili nalo tumelisikia kwa Rais Bosanaro wa Brazili na baadhi ya wataalamu ambao wanataka kuona jamii inatengeneza kinga ya jamii (herd immunity) ambayo inatokea endapo watu wengi wanapata maambukizi na kupona na hivyo kupunguza mahali virusi hivyo vinaweza kuambukiza zaidi.

Endapo kasi hii ya maambukizi Tanzania itaendelea kuwa ndogo namna hii mambo mawili yanaweza kutokea. Kwanza, tunaweza kujikuta hatuna wagonjwa wapya ndani ya wiki chache zijazo kwa sababu tumeweza kuzuia maambukizi ya ndani kwa ndani kwenye jamii na pili tunaweza kuonesha kuwa hofu ya kuwa Afrika itakuwa ni kiini cha mlipuko haina msingi kwani nchi zetu katika umaskini wao wote wameweza kudhibiti ugonjwa huu kwa haraka bila kulazimika kufunga nchi. Hii itaokoa uchumi wetu na watu wataendelea na maisha yao kama kawaida na kutumia fursa mbalimbali ambazo zitakuwa zimejitokeza kiuchumi.

Bahati Nasibu Ikilipa

Huku kutakuwa ni kulipa kwa bahati nasibu ya korona ambacho Magufuli ameicheza. Na ikitokea hivyo, Rais Magufuli atakuwa ameonesha namna nyingine ya kukabiliana na tishio hili kinyume na viongozi wenzake wa Afrika kama Uhuru Kenyatta, Cyril Ramaphosa na Paul Kagame. Mabezo yote ambayo baadhi ya watu wameyarusha kwa Rais Magufuli kwenye mitandao yatawarudia kwani Watanzania kwa fahari wataanza kuyarudisha mabezo hayo. Magufuli atajionesha bado ni kiongozi wa aina yake katika Afrika; umpende au usimpende. Kwamba, siyo kiongozi wa kufuata mkumbo au upepo.

Na inawezekana tukashuhudia kuwa kudhibitiwa kwa ugonjwa huu Tanzania kunaweza kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa viwanda vyetu na wajasiriamali mbalimbali. Baadhi ya nafasi zinazoweza au kupaswa kutumika mara ugonjwa huu ukidhibitiwa:

  • Utengenezaji wa vitakasa mikono (hand sanitizers)
  • Utengenezaji wa vifaa vya mtu kujikinga (PPEs) kama magauni, glovu, maski na vilemba. Viwanda vyetu vya nguo vinaweza kuchangamkia fursa hii
  • Utengenezaji wa vitanda na vifaa mbalimbali vya kitabibu (Kama dawa, maji ya wagonjwa n.k) ambavyo vinaweza kutoa nafasi kwa viwanda vyetu.
  • Kutoa mchango katika utafiti wa chanjo ya ugonjwa huu kwa wataalamu wetu (hatuwezi kuwa watu tunaosubiri wengine tu watuletee chanjo!)
Bahati Nasibu Isipolipa

Hata hivyo, bahati nasibu hii inaweza isilipe. Hili litatokea endapo vitu viwili vitatokea. Kwanza, endapo idadi ya wagonjwa wapya itaanza kuongezeka kwa kasi kama ilivyotokea nchi nyingine na kusababisha mfumo wetu wa tiba (healthcare system) kushindwa kuhimili na kubomoka (collapse). Pili, endapo itagundulika kuwa kwa makusudi serikali na taasisi zake wamekuwa hawaripoti kwa usahihi idadi ya wagonjwa na matokeo yake na hivyo kuwaacha watu wenye maambuziki kuendelea kuzurura mitaani na kusababisha hilo jambo la kwanza. Kwa vile hadi hivi sasa idadi yetu ya wagonjwa haina tofauti sana na baadhi ya nchi kama za wetu; suala la kuficha namba (under reporting) ni vigumu sana kuaminika isipokuwa kama kweli nchi nyingine zote kama za kwetu zingekuwa zinaripoti namba kubwa zaidi kulinganisha na za kwetu. Kwa nchi zetu za Afrika utaona kuwa tuoka katika wastani ukiondoa Afrika ya Kusini ambayo iko pembezoni kweli kweli (outlier).

Lakini endapo jambo la kwanza likitokea na Tanzania ikajikuta kwenye mlipuko mkubwa wa korona baadhi ya mambo ambayo yanaweza kutokea ni haya:

  • Magufuli atabebeshwa lawama binafsi za kusababisha hilo. Sidhani kama ataeleweka kama atakuja kuwalaumu Watanzania kuwa hawakumsikiliza.
  • Tanzania na Watanzania wote wanaweza kujikuta wanapigwa marufuku kwenda nchi nyingine hadi hali itakapotengemaa. Endapo mlipuko wa korona ukatokea wakati nchi nyingine zimedhibiti basi viongozi wa Tanzania watanyoshewa vidole na dunia nzima kwani wenzao walipokuwa wananyolewa wao walikuwa wanaweka kalikiti!
  • Mfumo wa afya wa Tanzania unaweza kujikuta ukiporomoka kuliko tunavyoweza kudhania. Tumeona jinsi nchi za daraja la kwanza (Italia, Ufaransa, Marekani na China) zikipata shida kukabiliana na ugonjwa huu. Imefikia mahali serikali za nchi hizo zimeomba na zinategemea misaada kutoka makampuni binafsi kupata dawa na vitendea kazi mbalimbali. Kuna hospitali Marekani manesi wake walijikuta wakitumia mifuko ya plastiki ya takataka kama mavazi ya kujikina! Marekani hiyo! Tumeona Hispania, wazee wakiachwa wajifie wenyewe kwani manesi na wahudumu wengine wamekimbia! Tumeona Italia madaktari na manesi wakifa kutokana na ugonjwa huu. Kama hili linatokea kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu! Kama limetokea kwa chuma cha pua, itakuwaje kwa chuma chakavu!
  • Kama hali itakuwa mbaya zaidi ya nchi hizo basi mtafaruku wa kijamii (social unrest) unaoweza kutokea utatisha. Huko Marekani sasa hivi watu pamoja na utulivu unaoonekana kwa nje lakini watu wako katika hali ya msongo mkubwa wa mawazo. Tayari takwimu zinaonesha kuwa Wamarekani wananunua bunduki na silaha ndogondogo kwa kiasi kikubwa ili kujilinda endapo utatokea mtafaruku. Ununuzi wa bunduki umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 300 nchini Marekani kutokana na hofu ya kuvunjika kwa utawala wa sheria sababu ya korona.
Yapo na mengine ambayo yanaweza kusemwa. Lakini vyovyote vile ilivyo, swali kubwa ni je hii ni bahati nasibu holela au ni bahati nasibu inayotokana na fikra za kisayansi. Kwamba, Rais Magufuli badala ya kuangalia mambo kijamii anaongozwa na ujuzi wake wa kisayansi na hivyo anapima mambo kwa uzito wa ushahidi ulio mbele yake (empirical evidence). Kwamba, Rais Magufuli ameona kuwa uwezekano (chance) ya Tanzania kupata mlipuko mkubwa endapo tunaweza kudhibiti maambukizi yaliyopo hadi hivi sasa ni mdogo sana. Na hii ndio sababu amewataka Watanzania kutotishika na kuendelea na shughuli zao. Siyo kwamba, anapuuzia au hajali kinachotokea duniani bali hataki watu wake wajifungie ndani, waache kazi, na kuombea “siku ya mwisho ifike”. Magufuli anasema “tusitishane”. Kwamba, tunaweza kudhibiti hali iliyopo bila kulazimika kuifunga nchi nzima. Kiukweli, hayuko peke yake duniani.

Kama nilivyosema hapo mwanzoni, tayari nchi kama Marekani imeanza kufikiria namna gani ya kufungua nchi ili watu waanze kurudi makazini. Hata ndani ya Marekani yenyewe baadhi ya majimbo bado hayajatangaza kufunga shughuli zote kwa sababu hawajapata maambukizi mengi (kumbuka nusu ya kesi zote za korona Marekani zinatokea Jimbo la New York). Wenzetu Marekani kutokana na utajiri wao licha ya kuifunga nchi wameweza kutenga dola trilioni 2.2 kwa ajili ya kulinda ajira, wafanyakazi na kusaidia sekta mbalimbali ili zisilipe gharama kubwa kutokana na ugonjwa huu. Kiasi hicho ni sawa na bajeti ya sasa ya Tanzania kwa karibu miaka 75!

Ni wazi basi kila mmoja wetu afanye anachotakiwa kufanya kujikinga na ugonjwa huu. Serikali iendelee kuwa muwazi na kwa namna yeyote isiwafiche au kuonekana inawaficha Watanzania hali ilivyo. Wahenga waliposema “mficha maradhi kifo kitamfichua” walisema ukweli. Na kwa vile tumeona kuwa hadi hivi sasa hakuna sababu ya kudhania serikali haisemi ukweli ni muhimu basi Waziri Mwalimu na Waziri Mkuu kutoa taarifa za hali ilivyo kwa haraka na kwa uwazi. Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii, habari za uongo zinasambaa haraka na hatuwezi kuwafunga watu wote wenye kuandika au kuanzisha mijadala hiyo. La maana ni kuliwahi treni la uongo kabla yalijafika kituo cha kwanza.

Tukifanya hivyo, na kweli tukadhibiti maambukizi ya ugonjwa huu na kuhakikisha uchumi wetu hauyumbi kwa kiasi kikubwa basi bahati hii nasibu ya Magufuli; italipa na italipa na kulipa.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Unaweza kufuatilia takwimu za kasi ya uambukizaji wa virusi vya korona nchi mbalimbali duniani kwa KUBONYEZA HAPA
Mmk tatizo letu accurate information. Je data tunazopewa ni sahihi?
Mbeya, dom tayar kuna wagonjwa na hawajaripotiwa bado
 
Ni uchambuzi mzuri mno na wa kina.Uchambuzi kama huu ulifanywa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi na akaishia kufukuzwa kazi.
Mpaka sasa tunamshukuru Mungu kwa hali ilivyo,iwe ni kwa mkakati wa Rais wetu na wataalamu wake au ni "nature" imetuhifadhi yote kwa yote shukrani ni za Mwenyezi Mungu.
Uthubutu wa Raisi wetu hauna mfano bahati mbaya kubwa ni kuwa pale mambo yanapokwenda kombo uwazi unakuwa tatizo.Mimi naamini mfumo uliopo Tanzania wa serikali mpaka vitongojini ndio nguzo kubwa.Nipo kijijini kabisa lakini huwezi amini kuwa hata viduka mkoba vina ndooya maji na sabuni na watu wananawa kwelikweli.
Hata mikakati hii iki back fire bado Magufuli atasimama kama shujaa!!!!
 
Tupunguze hofu, tufuate maelekezo, tufanye kazi , Tumshirikishe Mungu.
Kwa akili zenu za kulala juu ya mawe,mnatoa idadi za uwongo tu.awamu hii ni uwongo na comedy
IMG_20200326_081617.jpeg

Mzee tunakushukuru kwa hii makala ndefu ya bahati nasibu ilipayo au itiayo hasara. Kiukweli alichofanya rais sio kucheza bahati nasibu, ila kiuhslisua ugonjwa huu hauna nguvu kwenye nchi zenye hali kama ya kwetu. Hakuna cha tahadhari wala nini, bali ni ugonjwa usioweza kujimwambafy kwenye hizi nchi zetu fullstop.
 
Ndugu yangu wakati mwengine mambo unayotetea ni magumu sana.
Kwanza eleza kwanini baadhi ya nchi umeweka idadi ya watu na baadhi ya nchi hujaweka idadi ya watu wa nchi hiyo. Kuchagua Nigeria and Ethiopia and DRC kuweka idadi ya wagonjwa na idadi ya watu inaonyesha upo DISHONEST. Ungeweka nchi zote na Idadi ya watu na idadi ya wagonjwa. Halafu umeona South Africa? Idadi ya watu? Idadi ya wagonjwa?
Kaka sayansi inataka objectivity.
Kiufupi ni kuwa Tanzania INAFICHA takwimu za Watu wenye Corona waliopimwa. Lakini pia Tanzania hakuna vipimo mpaka juzi tulipopata vya Jack Ma. Huwezi kujua idadi kama hupimi.
Mwisho kauli ya Rais kanisani jumapili iliyopita ni kauli mbaya Sana kwa Kiongozi na imeaminiwa na baadhi ya watu. Watu watakufa sana
watu watakufa Sana,???

hiyo tu, ndio imeondoa kabisa uzuri wote wa mawazo yako
 
Nimekusoma kamanda mwanzo mwisho,
Nachangia hivi
Wazungu pamoja na kuwa na madaktari wengi, vifaa tiba vya kutosha, Mapesa kibao kuna sehemu kidogo wameteleza katika kutoa elimu kwa wananchi wao

Kuhusu maambukizi ya corona
Sisi watanzania tumetulia kwanza tukausoma mchezo tukafanya sub

Elimu elimu elimu
Katazo,, hapa ndio wazungu na wachina walipofeli ndio maana maambukizi yakawa makubwa

Msivae mask kwa sababu zenyewe ndio chanzo cha maambukizi
nimeona wachina na wazungu wanavaa mask muda wote na kisha wanazishika shika mara wanashusha kidevuni, mara wanashika pale mbele bila kujua madhara yake

Mask wanatakiwa kuvaa wagonjwa na madaktari au wahudumu wa kuhudumia wagonjwa au zivaliwe kwenye mikusanyiko ya watu kisha ukitoka mahala hapo tupa mask yako kwenye dustbin

Wachina na wazungu walifundishwa kuvaa muda wote mask mbaka chumbani

Sisi watanzania baada ya kupata elimu ya madhara ya kuvaa mask tumepotezea kabisa kuzivaa hizo mask zenyewe na tunadunda tu,

Watanzania tumefundishwa kunawa na sabuni au kujipaka sanitizer tunanawa hatari mikono na kujipaka sanitizer kama tumevurugwa

Watanzania tumeondoa ile hofu ya corona baada ya kuambiwa corona ni mafua tu yanapona yenyewe na watanzania awana sifa ya kufa kwa mafua

Kifupi upo uwezekano mkubwa wa watanzania walio wengi mtaani wakawa na dalili za corona lakini wanameza tu panadol kisha wanachukulia poa kwa sababu historia ya kufa kwa mafua hatuna

Mfano dada isabela na mwana F A
Sio kwamba walizidiwa sanaa laah ila kwa sababu walitoka nje ya nchi na uko ndio kuna corona walijijengea hofu kutokana na kelele za mitandao na vyombo vya habari

Lakini kama isingekuwa kutoka huko nje ya nchi wangekula zao panadol na tungekuwa nao mtaani kama tulivyokuwa nao wengine

Kuna watu wengi sana mtaani wanaishi na dalili za corona lakini awaendi kupima
Na kama wataamua kwenda kupima Muhimbili Patakuwa apatoshi

Mwisho watanzania corona tunayo tunatembea nayo hao watu 13 wamejistukia wenyewe na kutokana na ile taharuki ya ugonjwa wamejipeleka wenyewe serikalini lakini wagonjwa mtaani awakosekani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hali hii utatumia kigezo gani kujua kama bahati nasibu ililipa au kutokulipa kama taarifa tunazopewa haziaminiki?!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona kaelezea vizuri viashiria tunvyotakiwa kutumia kujua kama Bahati nasibu imelipa ama kutolipa! Italipa pale janga hili litakapoisha bila ya kuwa na mlipuko kwenye nchi yetu kiasi cha kushindwa kuimudu, Haitalipa pale hali ya maambukizi itakapochukua kasi na kuwa na wagonjwa wengi kiasi cha vituo vya huduma kuzidiwa.

Hajasema haamini taarifa, lakini kaongelea dhana iliyojingeka miongoni mwetu kwamba kuna namna takwimu zinafichwa, ni dhana hatuna uhakika nayo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Serikali ipo vizuri, imeweka mikakati thabiti ya kuzuia kusambaa na kuingia ugonjwa huu. Sanitizers zipo zakutosha, mask zipo za kutosha, elimu imetolewa yakutosha.. Serikali ya awamu ya tano inawajali na kuwalinda sana wananchi wake..
 
Acha uongo na propaganda Mzee. Marekani kama nchi haijaamua ni lini wananchi watarudi makazini wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka. Huo uliousema ni uongo. True, ni Trump ndiye aliyeleta hadharani pendekezo lake kuwa watu warudi kazini mapema kuliko Wanasayasi wake wanavyoshauri. Acha uongo Mzee.

Marekani kama nchi utapataje statement yake? Amesema wanawaza kulift lock down, hajasema wametangaza tayari. Hata mmoja akitamka ambae anasauti kwenye maamuzi inatafsiriwa kwamba tayari wanawaza kuhusu hilo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mbeya, dom tayar kuna wagonjwa na hawajaripotiwa bado

Unaweza kutusaidia dondoo kuhusu wagonjwa hawa ili itusaidie kuishinikiza serikali kutoa taarifa sahihi, kama wamethibitika kwanini tunafichwa.
Tutajie angalau hospitali walipopatikana, najua kuna watu humu watatumia platforms zao kuhoji.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimekusoma kamanda mwanzo mwisho,
Nachangia hivi
Wazungu pamoja na kuwa na madaktari wengi, vifaa tiba vya kutosha, Mapesa kibao kuna sehemu kidogo wameteleza katika kutoa elimu kwa wananchi wao

Kuhusu maambukizi ya corona
Sisi watanzania tumetulia kwanza tukausoma mchezo tukafanya sub

Elimu elimu elimu
Katazo,, hapa ndio wazungu na wachina walipofeli ndio maana maambukizi yakawa makubwa

Msivae mask kwa sababu zenyewe ndio chanzo cha maambukizi
nimeona wachina na wazungu wanavaa mask muda wote na kisha wanazishika shika mara wanashusha kidevuni, mara wanashika pale mbele bila kujua madhara yake

Mask wanatakiwa kuvaa wagonjwa na madaktari au wahudumu wa kuhudumia wagonjwa au zivaliwe kwenye mikusanyiko ya watu kisha ukitoka mahala hapo tupa mask yako kwenye dustbin

Wachina na wazungu walifundishwa kuvaa muda wote mask mbaka chumbani

Sisi watanzania baada ya kupata elimu ya madhara ya kuvaa mask tumepotezea kabisa kuzivaa hizo mask zenyewe na tunadunda tu,

Watanzania tumefundishwa kunawa na sabuni au kujipaka sanitizer tunanawa hatari mikono na kujipaka sanitizer kama tumevurugwa

Watanzania tumeondoa ile hofu ya corona baada ya kuambiwa corona ni mafua tu yanapona yenyewe na watanzania awana sifa ya kufa kwa mafua

Kifupi upo uwezekano mkubwa wa watanzania walio wengi mtaani wakawa na dalili za corona lakini wanameza tu panadol kisha wanachukulia poa kwa sababu historia ya kufa kwa mafua hatuna

Mfano dada isabela na mwana F A
Sio kwamba walizidiwa sanaa laah ila kwa sababu walitoka nje ya nchi na uko ndio kuna corona walijijengea hofu kutokana na kelele za mitandao na vyombo vya habari
Unaweza kutusaidia dondoo kuhusu wagonjwa hawa ili itusaidie kuishinikiza serikali kutoa taarifa sahihi, kama wamethibitika kwanini tunafichwa.
Tutajie angalau hospitali walipopatikana, najua kuna watu humu watatumia platforms zao kuhoji.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu, huyo ni mpuuzi tu, na ndo waliokuwa wakiombea Corona ije, na sasa wanaombea kila siku wagonjwa waongezeke na kwamba selikari itangaze hata idadi isyokuwepo, lakini ni Watanzania wenzetu, hakuna namna tuishini nao tu
 
Covid-19 facts:
1.Corona Virus ni kirusi hatari kwa ustawi wa binadamu kokote duniani.
2.Mlipuko huo umesimamisha uchumi wa dunia mzima.
3.Social distancing ni mbinu rahisi ya kupunguza maambukizi mapya ya Corona virus.
4.Magufuli approach is hypotheses not a law,time will tell.
 
Nilipoandika makala yangu ya ILIYOPITA kuhusiana na ugonjwa utokanao na virusi vya korona (COVID-19) Tanzania ilikuwa haijtangaza kuwepo kwa mgonjwa yeyote nchini na kuwa makala ile ililenga katika kutoa shime ya kuwahi ugonjwa huo. Nchi zote zilizowahi kuutangaulia ugonjwa huo na kuchukua hatua kali mapema wameweza kudhibiti kusambaa kwake na hata kupunguza kasi ya maambukizi (rate of infections). Nchi zilizochelewa kuchukua hatua hizo au zimechukua hatua ambazo ni za taratibu sana zimejikuta leo hii zikihangaika kuokoa na kulinda maisha ya wananchi wao. Italia, Ufaransa na Uingereza kama ilivyo Marekani na Irani ni nchi ambazo zote leo zinajikuta zinakimbizana na muda. Muda hauko upande wao.

Kwa Tanzania hadi hivi sasa kuna kitu kinachoonekana si cha kawaida (an anomaly). Nchi zote ambazo zimepata wagonjwa wa kwanza tumeona idadi ya wanaoambukizwa ikiongezeka kwa kasi kubwa (exponentially). Karibu mwezi mmoja nyuma (Februari 15) Marekani ilikuwa na wagonjwa 15; leo hii Machi 26 Marekani ina wagonjwa karibu 70,000. Hii ni nyuma ya China tu na Italia. Kasi hiyo ya kusambaa kwa ugonjwa huu imeonekana karibu nchi zote ambazo ugonjwa huu umejikita. Kwa Afrika ni Afrika ya Kusini ambayo inaonekana ugonjwa huu kusambaa kwa kasi (sasa hivi wao wana kesi zaidi ya 900)

Je, namba zetu zinaweza kuaminika?
Nimesema hapo juu kuwa hali katika Tanzania inaonekana si ya kawaida (an anomaly). Kwamba, kweli nchi yetu inaweza kuwa na wagonjwa 13 tu wakati watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida? Je inawezekana serikali inaficha hali halisi na kuwa labda Rais Magufuli hataki watu waone kuwa Tanzania ina wagonjwa wengi? Ukifuatilia mitandao ya kijamii unaweza ukaamini hili. Lakini hiki “kinachoonekana” ni lazima tukipime (kwa tulio pembeni) kwa kulinganisha na nchi nyingine kama za kwetu. Hadi hivi sasa inaonekana ugonjwa wa COVID-19 haujalipuka kwa kasi kubwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Kufikia leo kwa baadhi ya nchi za Afrika hali ya wagonjwa (na namba za wagonjwa wapya kwenye mabano) ni kama ifuatavyo:

Nigeria (yenye watu milioni 190) - 51

Rwanda – 41

Kenya 31 (3)

Madagascar (4)

Zambia – 16 (4)

Uganda - 14

Ethiopia (yenye watu milioni 105) - 12

Congo DR (yenye watu milioni 81) – 4

Hivyo, tukiangalia takwimu hata za majirani zetu na nchi nyingine tunazoshabihiana nazo kwa mambo mengi utaona kuwa kasi ya maambukizi bado si kubwa na kama alivyosema Waziri Ummy Mwalimu leo ni kuwa wengi wa wagonjwa hawa ni wale waliopata COVID-19 wakitokea nje. Kwa hiyo, hatuna budi kukubaliana na kile tunachokiona; ugonjwa huu ni tishio lakini kwa nchi hizi za kwetu haujaweza kusambaa kwa haraka katika jamii (community spread). Hofu ya ugonjwa huu kusambaa kwa haraka ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu.

Hatua Zilizochukuliwa Zinatosha?
Hadi hivi sasa serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa haya maambukizi ya ndani kwa ndani kwenye jamii hayatokei. Kufungwa kwa shule, vyuo na kutoa elimu ya usafi na kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima ni njia sahihi. Katika mazingira ya kawaida tulitarajia baada ya Isabela kugundulika kule Arusha tungeona mlipuko Arusha lakini hilo halijatokea. Katika mazingira tunayoyaona kwenye nchi za wenzetu mgonjwa wa kwanza anapopatikana tu basi kuna uwezekano wa kuibuka kwa wagonjwa wengi zaidi.

Na namna pekee ya kuwapata wagonjwa hao ni kuchukua vipimo kwa watu wengi kwa kadiri inavyowezekana. Hili nalo Waziri Mwalimu amelielezea leo vizuri. Kwamba serikali inafanya vipimo na kuongeza uwezo wa kupima kwa haraka. Hii yote inasaidia kuweza kujua ni sehemu gani ya watu katika nchi wanaweza kuwa wameupata ugonjwa huu.

Bahati Nasibu ya Magufuli
Ni kutokana na hili Rais Magufuli – ambaye ni mwanasayansi ameona kuwa kwa sasa nchi nzima si lazima ifungwe kama walivyofanya nchi nyingine. Amewataka Watanzania kuzingatia kanuni za usafi na kupunguza migusano isiyo ya lazima lakini wakati huo huo kuendelea na shughuli zao. Hoja hii si kwa Magufuli peke yake; tumeona hata Marekani kuna mjadala mkubwa wa kutaka watu waanze kurudi makazini ifikapo Pasaka kwani uchumi wao hauwezi kwenda bila watu kurudi makazini. Hili nalo tumelisikia kwa Rais Bosanaro wa Brazili na baadhi ya wataalamu ambao wanataka kuona jamii inatengeneza kinga ya jamii (herd immunity) ambayo inatokea endapo watu wengi wanapata maambukizi na kupona na hivyo kupunguza mahali virusi hivyo vinaweza kuambukiza zaidi.

Endapo kasi hii ya maambukizi Tanzania itaendelea kuwa ndogo namna hii mambo mawili yanaweza kutokea. Kwanza, tunaweza kujikuta hatuna wagonjwa wapya ndani ya wiki chache zijazo kwa sababu tumeweza kuzuia maambukizi ya ndani kwa ndani kwenye jamii na pili tunaweza kuonesha kuwa hofu ya kuwa Afrika itakuwa ni kiini cha mlipuko haina msingi kwani nchi zetu katika umaskini wao wote wameweza kudhibiti ugonjwa huu kwa haraka bila kulazimika kufunga nchi. Hii itaokoa uchumi wetu na watu wataendelea na maisha yao kama kawaida na kutumia fursa mbalimbali ambazo zitakuwa zimejitokeza kiuchumi.

Bahati Nasibu Ikilipa

Huku kutakuwa ni kulipa kwa bahati nasibu ya korona ambacho Magufuli ameicheza. Na ikitokea hivyo, Rais Magufuli atakuwa ameonesha namna nyingine ya kukabiliana na tishio hili kinyume na viongozi wenzake wa Afrika kama Uhuru Kenyatta, Cyril Ramaphosa na Paul Kagame. Mabezo yote ambayo baadhi ya watu wameyarusha kwa Rais Magufuli kwenye mitandao yatawarudia kwani Watanzania kwa fahari wataanza kuyarudisha mabezo hayo. Magufuli atajionesha bado ni kiongozi wa aina yake katika Afrika; umpende au usimpende. Kwamba, siyo kiongozi wa kufuata mkumbo au upepo.

Na inawezekana tukashuhudia kuwa kudhibitiwa kwa ugonjwa huu Tanzania kunaweza kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa viwanda vyetu na wajasiriamali mbalimbali. Baadhi ya nafasi zinazoweza au kupaswa kutumika mara ugonjwa huu ukidhibitiwa:

  • Utengenezaji wa vitakasa mikono (hand sanitizers)
  • Utengenezaji wa vifaa vya mtu kujikinga (PPEs) kama magauni, glovu, maski na vilemba. Viwanda vyetu vya nguo vinaweza kuchangamkia fursa hii
  • Utengenezaji wa vitanda na vifaa mbalimbali vya kitabibu (Kama dawa, maji ya wagonjwa n.k) ambavyo vinaweza kutoa nafasi kwa viwanda vyetu.
  • Kutoa mchango katika utafiti wa chanjo ya ugonjwa huu kwa wataalamu wetu (hatuwezi kuwa watu tunaosubiri wengine tu watuletee chanjo!)
Bahati Nasibu Isipolipa

Hata hivyo, bahati nasibu hii inaweza isilipe. Hili litatokea endapo vitu viwili vitatokea. Kwanza, endapo idadi ya wagonjwa wapya itaanza kuongezeka kwa kasi kama ilivyotokea nchi nyingine na kusababisha mfumo wetu wa tiba (healthcare system) kushindwa kuhimili na kubomoka (collapse). Pili, endapo itagundulika kuwa kwa makusudi serikali na taasisi zake wamekuwa hawaripoti kwa usahihi idadi ya wagonjwa na matokeo yake na hivyo kuwaacha watu wenye maambuziki kuendelea kuzurura mitaani na kusababisha hilo jambo la kwanza. Kwa vile hadi hivi sasa idadi yetu ya wagonjwa haina tofauti sana na baadhi ya nchi kama za wetu; suala la kuficha namba (under reporting) ni vigumu sana kuaminika isipokuwa kama kweli nchi nyingine zote kama za kwetu zingekuwa zinaripoti namba kubwa zaidi kulinganisha na za kwetu. Kwa nchi zetu za Afrika utaona kuwa tuoka katika wastani ukiondoa Afrika ya Kusini ambayo iko pembezoni kweli kweli (outlier).

Lakini endapo jambo la kwanza likitokea na Tanzania ikajikuta kwenye mlipuko mkubwa wa korona baadhi ya mambo ambayo yanaweza kutokea ni haya:

  • Magufuli atabebeshwa lawama binafsi za kusababisha hilo. Sidhani kama ataeleweka kama atakuja kuwalaumu Watanzania kuwa hawakumsikiliza.
  • Tanzania na Watanzania wote wanaweza kujikuta wanapigwa marufuku kwenda nchi nyingine hadi hali itakapotengemaa. Endapo mlipuko wa korona ukatokea wakati nchi nyingine zimedhibiti basi viongozi wa Tanzania watanyoshewa vidole na dunia nzima kwani wenzao walipokuwa wananyolewa wao walikuwa wanaweka kalikiti!
  • Mfumo wa afya wa Tanzania unaweza kujikuta ukiporomoka kuliko tunavyoweza kudhania. Tumeona jinsi nchi za daraja la kwanza (Italia, Ufaransa, Marekani na China) zikipata shida kukabiliana na ugonjwa huu. Imefikia mahali serikali za nchi hizo zimeomba na zinategemea misaada kutoka makampuni binafsi kupata dawa na vitendea kazi mbalimbali. Kuna hospitali Marekani manesi wake walijikuta wakitumia mifuko ya plastiki ya takataka kama mavazi ya kujikina! Marekani hiyo! Tumeona Hispania, wazee wakiachwa wajifie wenyewe kwani manesi na wahudumu wengine wamekimbia! Tumeona Italia madaktari na manesi wakifa kutokana na ugonjwa huu. Kama hili linatokea kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu! Kama limetokea kwa chuma cha pua, itakuwaje kwa chuma chakavu!
  • Kama hali itakuwa mbaya zaidi ya nchi hizo basi mtafaruku wa kijamii (social unrest) unaoweza kutokea utatisha. Huko Marekani sasa hivi watu pamoja na utulivu unaoonekana kwa nje lakini watu wako katika hali ya msongo mkubwa wa mawazo. Tayari takwimu zinaonesha kuwa Wamarekani wananunua bunduki na silaha ndogondogo kwa kiasi kikubwa ili kujilinda endapo utatokea mtafaruku. Ununuzi wa bunduki umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 300 nchini Marekani kutokana na hofu ya kuvunjika kwa utawala wa sheria sababu ya korona.
Yapo na mengine ambayo yanaweza kusemwa. Lakini vyovyote vile ilivyo, swali kubwa ni je hii ni bahati nasibu holela au ni bahati nasibu inayotokana na fikra za kisayansi. Kwamba, Rais Magufuli badala ya kuangalia mambo kijamii anaongozwa na ujuzi wake wa kisayansi na hivyo anapima mambo kwa uzito wa ushahidi ulio mbele yake (empirical evidence). Kwamba, Rais Magufuli ameona kuwa uwezekano (chance) ya Tanzania kupata mlipuko mkubwa endapo tunaweza kudhibiti maambukizi yaliyopo hadi hivi sasa ni mdogo sana. Na hii ndio sababu amewataka Watanzania kutotishika na kuendelea na shughuli zao. Siyo kwamba, anapuuzia au hajali kinachotokea duniani bali hataki watu wake wajifungie ndani, waache kazi, na kuombea “siku ya mwisho ifike”. Magufuli anasema “tusitishane”. Kwamba, tunaweza kudhibiti hali iliyopo bila kulazimika kuifunga nchi nzima. Kiukweli, hayuko peke yake duniani.

Kama nilivyosema hapo mwanzoni, tayari nchi kama Marekani imeanza kufikiria namna gani ya kufungua nchi ili watu waanze kurudi makazini. Hata ndani ya Marekani yenyewe baadhi ya majimbo bado hayajatangaza kufunga shughuli zote kwa sababu hawajapata maambukizi mengi (kumbuka nusu ya kesi zote za korona Marekani zinatokea Jimbo la New York). Wenzetu Marekani kutokana na utajiri wao licha ya kuifunga nchi wameweza kutenga dola trilioni 2.2 kwa ajili ya kulinda ajira, wafanyakazi na kusaidia sekta mbalimbali ili zisilipe gharama kubwa kutokana na ugonjwa huu. Kiasi hicho ni sawa na bajeti ya sasa ya Tanzania kwa karibu miaka 75!

Ni wazi basi kila mmoja wetu afanye anachotakiwa kufanya kujikinga na ugonjwa huu. Serikali iendelee kuwa muwazi na kwa namna yeyote isiwafiche au kuonekana inawaficha Watanzania hali ilivyo. Wahenga waliposema “mficha maradhi kifo kitamfichua” walisema ukweli. Na kwa vile tumeona kuwa hadi hivi sasa hakuna sababu ya kudhania serikali haisemi ukweli ni muhimu basi Waziri Mwalimu na Waziri Mkuu kutoa taarifa za hali ilivyo kwa haraka na kwa uwazi. Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii, habari za uongo zinasambaa haraka na hatuwezi kuwafunga watu wote wenye kuandika au kuanzisha mijadala hiyo. La maana ni kuliwahi treni la uongo kabla yalijafika kituo cha kwanza.

Tukifanya hivyo, na kweli tukadhibiti maambukizi ya ugonjwa huu na kuhakikisha uchumi wetu hauyumbi kwa kiasi kikubwa basi bahati hii nasibu ya Magufuli; italipa na italipa na kulipa.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Unaweza kufuatilia takwimu za kasi ya uambukizaji wa virusi vya korona nchi mbalimbali duniani kwa KUBONYEZA HAPA

Mkuu unapokuwa kiongozi ni jukumu lako kuweka maono yako katika Imani ya kile unachokiamini. Sasa iwapo unachokiamini kikiwa vizuri na matarajio yako basi utakuwa umeponya wengi sana lakini pia kikiwa kunyume na ulivyotarajia pia wengi wataangamia kwa kuamini kwako lakini yote na yote utakuwa ni kiongozi uliye bora kwa sababu umesimamia ulichokiamini bila kuyumbishwa.
 
Back
Top Bottom