HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Napenda kuwaasa watanzania kuwa ni muhimu kujiamini...Health System yetu inatarajiwa kuonesha resilience ya hali ya juu katika hili.tusimbeze Rais na vyombo vyake...tuendelee kuisupport serikali kukabiliana na janga hili
 
Waebrania 5:14
"Lakini Chakula Kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya".

Asomaye na Afahamu.

Asante Mleta uzi.
 
Vipi Bahati Nasibu inalipa? Mtanzania 1 keshatangazwa kupoteza Maisha. Huyo ndiye aliyetangazwa, kuna kadhaa wengine wamezikwa kimya kimya.
Mnageuza maisha ya Watanzania kuwa Bahati Nasibu, ama kweli KUA UYAONE
 
Jambo la msingi ambalo ulitakiwa ufahamu kuwa huu ugonjwa ni very complex. Na kwa mazingira ya nchi za kiafrica total lockdown na kufunga mipaka ni suala gumu sana. Angalia tu kwa mtu ambaye ni mama lishe anaekaa uswahilini,anapikia nyumbani chakula chake na kukiuzia kariakoo umwambie kwa siku thelathini usitoke ndani,ataishi vipi? Mimi nafikiri pamoja na kuwa ulitaka kuleta ujumbe mzuri lakini kutumia neno bahati nasibu haijakaa vizuri. Tumeona kenya pamoja na kuchukua hatua za kuzuia watu kutoka majumbani,kwa sababu ya umaskini wetu waafrika watu waliingia kwa nguvu ili wapate hata mkate. Matokeo yake ni wananchi na waandishi wa habari kuchapwa virungu.
Mimi nafikiri Rais kama kiongozi wa nchi yetu aliangalia mazingira yalivyo kimaisha na kupima na kuona kuwa kuzuia watu kutoka na kufunga mipaka ni ngumu.
Pia umegusia kuhusu idadi ya wagonjwa kuwa unahisi kwamba huenda kuna udanganyifu sababu tu haiwezekani kuwe na idadi ndogo ya wagonjwa.Sasa serikali ifiche ili ifaidike nini? Sababu hili ni janga la dunia. Hata hao wamarekani ambao waliwakebehi wachina kuna kirusi toka china wanaona aibu sasa hivi. Hili ni janga la kidunia hata WHO lazima wafuatilie data za kila nchi sidhani kama kuna udanganyifu.
 
Wewe mwendawazimu acha kuidharirisha serikali yetu.serikali hii ya awamu ya tano pesa ipo.Wewe mwendawazimu na rais Magufuli nananajua pesa ipo au haipo?nakuonya usirudie tena ujinga huu

Sijijui, upo!???

Wewe kweli ni likely HUJIJUI....!!

Kwani mwenzio kakukosea nini hata kumporomoshea matusi kiasi hicho?

Kwa sababu ya kutoa maoni yake, au siyo? Kwani lazima kila mtu atoe positive opinion dhidi ya Rais wako Magufuli ndiyo aonekane wa maana kwako?

Kama ndivyo unavyoamini, basi nina hakika upstairs hauko sawa wewe......!!!
 
Mkuu huo ndio ukweli, ila hawataki kuukubali, jamaa kaangalia Hali ya kipato Cha mtanzania na halingumu ya maisha akaona nibora ajifunge bomu shingoni likilipuka kilamtu atajuwa Ni jinsigani ya kujiokoa
Mkuu kwa hali kama hiyo tutamkimbilia nani?
Mimi nimejifunza kitu,kiongozi au mtawala mahili nchini kwetu atajulikana jinsi alivyopambana na Corona akaishinda au akashindwa.
 
Amenikosea sana kwa kuidharirisha nchi yangu,nchi hii ni tajiri sana,why aiite masikini?Kama anatumiwa na mabeberu aende huko huko na kutumika kwake
 
Mkuu usilinganishe nchi za dunia ya kwanza ambazo watu wake wanao uwezo wa kuweka akiba na wakakaa majumbani mwao hata miezi miwili na hizi za dunia inayopambana iweze kusimama.

Kuna kina mama wauza chapati na vitumbua hawa ukiwaambia wakae majumbani watakufa njaa, kuna wengi wamechukua mikopo ya vicoba wanadaiwa marejesho hawa wakishinda ndani watakufa na njaa.

Kufungia mipaka sio jambo rahisi na linakuwa ni chaguo la mwisho kwa kiongozi wa nchi kama hizi za afrika, afya ni muhimu lakini na uhalisia wa uduni wa maisha unapaswa kuangaliwa.
 
Makala ya mleta Mada ni ndefu, nzuri na imeeleweka mno, wewe ndo una matatizo makubwa, umesoma kwa kukurupuka na unajibu kwa kukurupuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mimi nashindwa kuelewa mna - argue kitu gani kwa sababu;

1. Haiwezekani uwafungie watu ndani halafu usiwape chakula na maji ya kutosha kutumia kwa muda wote utakaokuwa umewafungia...!!

2. Kama serikali ya Tanzania imeshindwa ama inasita sita kuchukua hatua hizo kwa sababu ya kukosa uwezo wa kuwahudumia watu watakapokuwa ndani (locked down), then huo ni uamuzi sahihi....!!

3. Kwa uamuzi huu ni wazi kuwa Tanzania itakuwa imeamua kuiachia "nature" iamue hatima ya wananchi wake pasipo kuhusisha hatua zote za kibinadamu

Mungu anasema; "....nimewapa AKILI ili muweze kutambua MEMA na MABAYA...."

Hapo ndipo tumeshatumia uwezo wetu wa kuamua. Hilo ndilo jema tulilochagua...
 
Tunaongea nadharia nyingi lakini ukweli kuhusu pato la mtanzania wa kawaida linajulikana.
 
Vipi Bahati Nasibu inalipa? Mtanzania 1 keshatangazwa kupoteza Maisha. Huyo ndiye aliyetangazwa, kuna kadhaa wengine wamezikwa kimya kimya.
Mnageuza maisha ya Watanzania kuwa Bahati Nasibu, ama kweli KUA UYAONE

..hii siyo bahati nasibu.

..kilichofanyika ni KAMARI.

..na maisha yetu wanayachezea kila siku.
 
Kwa uamuzi huu ni wazi kuwa Tanzania itakuwa imeamua kuiachia "nature" iamue hatima ya wananchi wake pasipo kuhusisha hatua zote za kibinadamu
Mkuu mbona kuna hatua nyigine zimechuliwa kama kudhibiti wanaosafiri kuingia nchini, kusimamisha shule na vyuo, kuhimiza kunawa, watu kutoshikana mikono.....kwa hiyo haijaachiwa "nature".
 
Vipi Bahati Nasibu inalipa? Mtanzania 1 keshatangazwa kupoteza Maisha. Huyo ndiye aliyetangazwa, kuna kadhaa wengine wamezikwa kimya kimya.
Mnageuza maisha ya Watanzania kuwa Bahati Nasibu, ama kweli KUA UYAONE
Hili mbona lilitarajiwa? korona inakuja na vifo. Suala kubwa ni kasi ya maambukizi na idadi ya wagonjwa wanaoishia ICU. Kama una ushahidi wa mtu yeyote aliyeugua korona (sijui utakuwa umeujaje) na amekufa na kuzikwa kimya kimya ni vizuri uweke ushahidi huo hadharani. Sidhani kama kuna Watanzania wenye kuuguza ndugu zao sirini hadi wanakufa bila kupiga kelele kuwa ndugu zao wanakufa. Kama kuna mtu binafsi unamjua kuwa ametaka kutibiwa au kupimwa na amekataliwa akiwa anaumwa akionesha dalili za korona na mtu huyo akafa na kuzikwa kimya kimya ni vizuri kuweka wazi. Nasimama kusahihishwa.
 

..South Sudan na wenyewe wamecheza kamari kama sisi na hawana mgonjwa hata mmoja.

..natamani tumuazime Raisi wa South Sudan aje atuongoze.
 
Nasikia ukijipaka kwa kujisugua pilipili za kutosha sehemu za siri haupatwi na Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…