Hoja nzito: Sumaye asema CHADEMA badala ya kupambana na CCM kwa Hoja wao wanashindana na polisi ambao hawatawaweza

Hoja nzito: Sumaye asema CHADEMA badala ya kupambana na CCM kwa Hoja wao wanashindana na polisi ambao hawatawaweza

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Aliyekuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA mzee Sumaye amesema mara kadhaa aliwashauri viongozi wenzake wapambane na CCM kwa hoja lakini walimpuuza.

Sumaye anasema CHADEMA wamejikita kushindana na polisi ambao kamwe hawatawaweza kwa kuwa askari wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Unapojikita kushughulika na polisi maana yake unawaachia CCM wafanye siasa ndio maana nimerudi kwenye chama changu ili nifanye siasa amemaliza mzee Sumaye.

Maendeleo hayana vyama!
 
Alipoondoka CCM alidai hakuna demokrasia. Kaondoka CHADEMA eti nako hakuna demokrasia.
Eventually karudi CCM. Vicious cycle. Vyama tofauti, mtu ni yule yule mmoja.

Hapa hata mtoto wa shule ya vidudu atajua tatizo liko wapi!
 
Kipindi chote akiwa CHADEMA alipambana na nani? Atuelewa CHADEMA wanapambana vipi na polisi badala ya CCM.
 
Hivi CCM inayakumbuka maneno aliyoyasema Sumaye wakati anatoka ccm na kwenda chadema? Sumaye alisema hata rudi ccm kwani ccm sio mama yake akamnukuu na Hayati baba wa Taifa kuwa ccm sio mama yake,nilitarajia jana wakati wa kumpokea Sumaye ,CCM inge mwuuliza juu ya hiyo kauli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamuulize wa nini na njaa imemrudisha, akae atulie ashibishe tumbo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anazungumzia hawa Polisi wanaotembea na Ilani ya CCM!! Haha..

Yeye atapambana vipi na CCM wakati yuko ndani?

Kwanini hakujiunga na wanaokubali hoja yake?!!!
 
Huyo Mzee kachanganyikiwa baada ya kunyang'anywa mashamba yake na hao hao serikali anayoiabudu sasa!Tuliwaambia kuwa kudumu upinzani lazima muwe mmejitoa muhanga!
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mzee Sumaye amesema mara kadhaa aliwashauri viongozi wenzake wapambane na CCM kwa hoja lakini walimpuuza.

Sumaye anasema Chadema wamejikita kushindana na polisi ambao kamwe hawatawaweza kwa kuwa askari wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Unapojikita kushughulika na polisi maana yake unawaachia CCM wafanye siasa ndio maana nimerudi kwenye chama changu ili nifanye siasa amemaliza mzee Sumaye.

Maendeleo hayana vyama!
Aliyekuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mzee Sumaye amesema mara kadhaa aliwashauri viongozi wenzake wapambane na CCM kwa hoja lakini walimpuuza.

Sumaye anasema Chadema wamejikita kushindana na polisi ambao kamwe hawatawaweza kwa kuwa askari wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Unapojikita kushughulika na polisi maana yake unawaachia CCM wafanye siasa ndio maana nimerudi kwenye chama changu ili nifanye siasa amemaliza mzee Sumaye.

Maendeleo hayana vyama!
FB_IMG_1581414222882.jpg


Tuendelee au tusiendelee ?
 
Hahah...

Sasa Sumaye anataka kufanya siasa gani tena kwa umri alionao, au kapewa ahadi za jimbo la Kibamba!!!
 
Back
Top Bottom