Hoja nzito: Sumaye asema CHADEMA badala ya kupambana na CCM kwa Hoja wao wanashindana na polisi ambao hawatawaweza

hebu jamani mrudishieni Sumaye mashamba yake ya Morogoro ili atulie kwa amani asizidi kujizalilisha.
 
Sasa polisi si ndio hao wanaotumiwa na CCM kuzuia kusiwe na uwanja fair? Sumaye ina maana haelewi hili? Uelewa wake ni finyu sana.
 
Alipoondoka CCM alidai hakuna demokrasia.
Kaondoka CDM eti nako hakuna demokrasia.
Eventually karudi CCM. Vicious cycle.
Vyama tofauti, mtu ni yule yule mmoja.
Hapa hata mtoto wa shule ya vidudu atajua tatizo liko wapi!
Tamaa ya madaraka tu hawa wazee.
Wapumzike wengine nao wapate nafasi ya kuongoza.
 
johnthebaptist,
CHADEMA haijawahi kupambana na polisi, siku zote polisi inapambana na Chadema kuwalinda CCM, ni polisi inayopeleka askari naagsri kurandaranda kwenye ofisi za CHADEMA kuhakikisha hawatoki nje kumwaga taka!
 
Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, Sumaye bila shaka amesoma lakwanza mpaka form four na akaenda mpaka chuo kikuu, Dah ndio maana USA na Europe zipo hapo zilipo
 
johnthebaptist, Mzee kaa kimya unajidharaulisha tu,mtu umekuwa waziri mkuu wa JMT kwa miaka kumi kwenda kugombea uenyekiti wa kanda huoni ilikuwa kitendo cha kijuha? Hata hao wanaokupigia makofi hapo walikuwa wanakunanga ila kwa vile CCM ni genge la wanafiki basi wanakuchulia poa ili muendelee kuganga njaa na matamanio yenu ya kutaka madaraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni siasa ipi ambayo bado anataka kufanya huyu mzee? Sumaye angetulia tu ale pension yake taratibu na alee wajukuu
Huyu mzee atakuwa anawashwa washwa ndiyo sababu ya yeye kukosa maneno ya busara.

Hata hao wajukuu sijui kama anao.

Mzee Nkapa aliwahi kuwaita yeye na yule mmasai kuwa ni malofa, bila shaka ni malofa kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshakuwa PM miaka 10 halafu unaanza kuhangaika na siasa za upinzani,angalau basi uwe na ushawishi,Sasa unakuta ushawishi wenyewe upoupo tu.
Nyumbani kumenoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…