Hoja nzito: Sumaye asema CHADEMA badala ya kupambana na CCM kwa Hoja wao wanashindana na polisi ambao hawatawaweza

Hivi kwa mfano unawezaje kuitofautisha CCM na Polisi kwa sasa?
 
Sumaye laiti angejua kuwa huko CCM kwenyewe haitajiki, haaminiki na wala hakubaliki basi angejifunza kukaa kimya au kujifunza cha kusema.

Sumaye ni sawa na mkimbizi aliyerejea nchini kwake lakini bado nchi yenyewe haijatulia, ipo siku atakimbia au kukimbizwa.
 
We msukule!
Kinachoshangaza ni kipi kati ya MAFISADI kwenda CCM na MAFISADI kuchukuliwa na CHADEMA.
Tena sio kuchukuliwa tu!
Wanagombea na URAIS na kupewa UNEC.
CHADEMA ya siku hizi inaji-equate na CCM. ndo imefikia level hiyo?
Kumbe unatambua CDM ni level za juu kuliko CCM eeh!Hahaahaaaa,basi ngoja nijibu,CDM haijafikia level hizo!
 
Wahenga walisema Uzee dawa!! Sidhani kama walikuwa sahihi 100% sababu hasa wasio na busara huzeeka pia.
 
Mbowe na wenzake lazima waache kabisa mtindo wa kupokea "Makapi ya Kisiasa, Political Rejects" kutoka ccm.

Hii kitu imeigharimu sana hiki chama kuliko kitu kingine chochote toka kianzishwe zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Hakuna value yoyote iliyoongezwa na watu hawa kwa kuhamia Chadema ila wamekuwa kama waliokuwa wanakuja kuwachora tu yaani (Moles). Lazima tukubali huu mkakati ni wa hovyo kabisa na is a big wash out.
 
Mimi Huwa nashangaa Hivi hawa Wana Siasa wanavyohama vyama Hawawezi kuhama kimya kimya bila kuongea Sababu zao za kitoto za kuhama Chama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…