Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Katika maisha kuna hali tofauti tofauti. Hali zingine ni kutokamilika kwetu, au kujisahau kwetu.
Kwa tulipofikia sasa si kila mtu anastahili kuonewa huruma na kusaidiwa na jamii. Wakati mwingine ni mavuno ya alichopanda. Hebu fikiria hii;
1. UHALIFU
Ulikuwa mwizi, umewaibia watu sana, umewapa hasara sana, sasa ukakamatwa na kuvunjwa mguu au mkono. Ama umelogwa, unateseka, sasa unarudi mtaani kutafuta huruma za jamii(kuomba omba), nani akusaidie sasa, unalaumu jamii kwa kukutenga?!
2. KWENYE JAMII
Ulikuwa unaringa kipindi una mafanikio, labda kazi nzuri, kipato cha uhakika, marafiki wa level zako. Sasa maisha yamebadilika umerudi chini, unataka wale uliowadharau wawe pamoja na wewe. Wanapo kukataa unawalaumu hawana upendo, wanafiki. Mbona mwanzo hukuwaona hivyo?
3. STAREHE
wewe ulikuwa mla bata, pedeshee, mutu ya watoto, umewagonga wewe mpaka wamekuachia magonjwa ya zinaa. Sasa umeanza kunyauka wamekukimbia, umefilisika sababu ya matibabu sasa unataka uende sawa na wastaarabu nani akukubali? Kula mavuno yako mwenyewe.
4. SIASA
Mnafanya uchaguzi, wananchi mmechuja sera, mmeambiwa chama hiki hakifai, sera zao zile zile, tabia zao zile zile, mkachagua hivyo hivyo. Sasa mavuno yenu ni tozo ya miamala sa simu, miamala ya benki, kodi ya jengo kupitia LUKU n.k
Mifano ni mingi, ukitafakari makosa mengi ya mwanadamu zaidi ya 60% mengine yana epukika. Kabla ya kufanya jambo lolote fikiria na matokeo yake au mwishowe.
Kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Ndio maana siamini kabisa kuhusu kila jambo ni mipango ya Mungu, au baada ya kukosa unasingizia ni shetani kanipitia kumbe ni mavuno yako tu.