jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Kuna mdau amenihoji nini msimamo wangu kuhusu hizi tozo au tuseme sakata la Tozo. Nitamjibu bila unafiki...
Mimi ni muumini wa nchi kujitegemea na kujiendesha kikamilifu kwani hiyo ndio maana kamili ya uhuru. Haiwezekani kwa miaka yote hiyo tangu uhuru tuendelee kusomeshewa,kuuguziwa,kustareheshwa na kulishwa kwa HISANI YA WATU WA MAREKANI /SWEDEN/UK/CHINA n.k.
Lazima ifike mahali tujisimamie na kujiendesha kwa asilimia 100. Utamu na uchungu wa kodi ni lazima uwe shared ....Hii ni dhana muhimu sana tunapoenda kutekeleza suala hili la ulipaji wa kodi bila kushikana shati.
Kila mmoja alipe kodi yaani tukianzia ACCASIA ,DANGOTE hadi raia wa kawaida bila the so called TAX HOLIDAYS ,sijui kuvutia wawekezaji na blah blah nyingine.
Matumizi ya kodi
Hapa ndio penye hoja muhimu la sivyo tutatovugana vidole vya macho. Kodi au tozo hii ielekezwe moja kwa moja kwenye kujenga miundombinu ya huduma za jamii NOT LESS NOT MUCH yaani ikiingia B 800 mwezi huo huo mzigo unatawanywa kwenda kujenga barabara na shule na hospitali na visima vya maji....Yaani sio zile issue za upembuzi yakinifu na uchakataji...Hapo TUTAMTOVUGA MTU!
Zaidi Huduma hii ya uhamishaji fedha iruhusiwe kwa upana katika muktadha wa ICT ....Yaani tuachane na monopoly ya makampuni ya simu tu.Turuhusu Apps mbalimbali za kukusanya ,kutunza na kusafirisha fedha.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!!!!