Hoja wanazotumia kumwandamana Dotto Biteko hazina mashiko

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Waziri Dotto Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri mMkuu ameituliza sana Wizara ya Nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na Wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na “amewagawia bandari zote za Tanganyika”.

Kwa hiyo hoja kwamba siyo raia wa Tanzania ni upuuzi mtupu na ni mbinu za mafisadi kumchafua.
 
Kuwa na ndugu nje ya nchi si kosa. Hata Lissu ana ndugu Wamarekani.

Kwani uraia wa Biteko ukoje? Wa kuzaliwa au wa "kununua"?
 
Kweni Uchaguzi Mkuu umekaribia hadi kuanza kuvuana Uraia?!
Siyo mimi mkuu! Nataka nijue pa kusimamia, kumkosoa au kumtetea. Mimi sina shida na uraia wake kwa sababu siyo Mbunge wa Jimbo langu.

Isitoshe, Dotto anaonekana ni mchapa kazi. Maadam ni mchapa kazi, hata kama uraia wake ni wa nchi nyingine, bado tunaweza kumwazima kwa muda kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanganyika.
 
Dotto ni Mtanzania na ni mchapakazi mimi ningependa aje huku CHADEMA huko CCM ataambukizwa Ufisadi.
 
Dotto Biteko ameituliza sana wizara ya nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na amewagawia bandari zote za Tanganyika.
Hizi hoja , ukifiria kwa undani sana, unajua tu kuwa, zinatoka kwa kipara. Inaonekana kipara kwa, sasa ana muogopa, sana Doto kwenye ushindani anaoufikiria.

Kwanza kipara, hana uwezo mkubwa wa kufikiri. Uwezo wake ni kama wa mzee wake mmoja ambaye alishawahi kuwa, Rais.Mzee Tabasamu.

Nimemuhusisha kipara na huu mchezo wa kumchafua Doto kwa kwa sababu hizi:Moja Doto alifanya kazi nzuri sana ya bwawa na kipara alifeli.Na ameendelea kuwa bora kwenye utendaji wake,akiwa naibu wazir mkuu.

Pili,Doto kuwa naibu wazir mkuu, hilo kipara, hakulitaka kwa kuwa aliutaka sana uwazir mkuu.Na kuna muda hapa katikati,Kassim alichafuliwa sana. Ila,mama alikuwa na misimamo.

Tatu:Tabia ya kuchafua watu, pia anayo Mr tabasamu ambaye , ndiye mshauri mkuu wa, kipara. Tuliona hiyo mwaka 2005 akimchafua Dr Salim Ahmed Salim kuwa sio raia.

Aidha, uchambuzi wangu , unanionyesha kuwa, msingi wa matamshi ya mkuu wa, majeshi kuhusu uraia wa viongoz ulitoka kwa Mr Tabasamu. Kwani Mr Tabasamu pia hakupendezwa na uteuzi wa Doto kuwa naibu wazir mkuu kwani inatishia nafasi ya kipara , kule anapofikiria.

Duru za kumbukumbu za, hotuba ya mwalimu zinaonyesha kuwa mwalimu hakupenda wala kupendezwa kuwaita baadhi ya watu kuwa sio raia. Mwalimu alisema, wananchi wote, wa Tanzania wametoka sehemu mbalimbali, akiwemo yeye mwalimu ambaye kabira yake ina asili ya Rwanda. Na wao kuitwa wazanaki, waliitwa na wajita, wakimaanisha waliokuja na nn. Watu wenye asili ya Tanzania kabisa ni wagogo.Wengi wametoka sehemu nyingi za Africa.

Mwisho, Kipara na Tabasamu watafute hoja nyingine, hii wamekosea.
 
Waziri Dotto Biteko ambaye pia ni naibu waziri mkuu ameituliza sana wizara ya nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na amewagawia bandari zote za Tanganyika.

Kwa hiyo hoja kwamba siyo raia wa Tanzania ni upuuzi mtupu na ni mbinu za mafisadi kumchafua.
Hata makamba anawajomba nje
 
Jiwe la gizani limempata mtu. Ifahamike kwamba kama siku ile CDF anaongelea tishio la kiusalama la wahamiaji haramu kushika nyadhfa za maamuzi na huyo bwana alikuwepo kwenye list basi lazima ataondolewa tu.
 
Kuwa na ndugu nje ya nchi si kosa. Hata Lissu ana ndugu Wamarekani.

Kwani uraia wa Biteko ukoje? Wa kuzaliwa au wa "kununua"?

Mhamiaji haramu kwa sababu hakuwahi kufuata taratibu za kuupata uraia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria. Yeye ajiuzulu nafasi zote, kisha afuate tu taratibu za kurasimisha uraia wake kwa kuukana uraia wa nchi yake asilia.
 
Kama kuwa na wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na amewagawia bandari zote za Tanganyika.
Kama kuwa na wajomba nje wanaoweza kufanya haya nini cha kujivunia, au huelewi unacho andika hapa?
Inaonyesha unao uhusiano na huyo mtu wako, hii siyo bure.

Ni hivi. Kama mnataka kuwa waTanzania na msiwekewe mashaka yoyote, kubalini Tanzania ndiyo nchi yenu, achaneni na maslahi ya huko kwenu, huku mkijifanya nyinyi ni wenzetu.

WaTanzania hawawezi kuwabagua kwa misingi ya huko mnakotokea, bali kwa matendo yenu yanapoonyesha mpo hapa kuendeleza maslahi ya huko mlikotokea.
 
Mhamiaji haramu kwa sababu hakuwahi kufuata taratibu za kuupata uraia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria. Yeye ajiuzulu nafasi zote, kisha afuate tu taratibu za kurasimisha uraia wake kwa kuukana uraia wa nchi yake asilia.
Na inasikitisha na kushangaza sana hawa watu wanawezaje kujipenyeza miongoni mwetu hadi kufika huko juu bila kugundulika.
Hili linatia hofu sana kuhusu usalama wetu.

Lakini, ni kama nikijijibu mwenyewe swali hilo; jibu ni CCM yenyewe. Uozo ulioingia ndani ya chama hicho unahatarisha sana usalama wa nchi hii.
Hawa wakimbizi wanapojipenyeza ndani ya chama hicho, toka huko vijijini, hakuna tena anayefuatilia kujuwa ni watu wa aina gani hawa.
 
Jiwe la gizani limempata mtu. Ifahamike kwamba kama siku ile CDF anaongelea tishio la kiusalama la wahamiaji haramu kushika nyadhfa za maamuzi na huyo bwana alikuwepo kwenye list basi lazima ataondolewa tu.
Huyo aliye mteua katika nafasi hizo, hata yeye licha ya kushika wadhifa wa juu kabisa, haieleweki baba yake mzazi ni nani na anaishi/aliishi wapi?
Kuna ujinga wa kutisha sana ndani ya nchi hii.
 
Huyu ndiye mmoja wa wale aliowataja Mkuu wa Majeshi " kuna wahamiaji haramu wameteuliwa kwenye nafasi nyeti" huyu ni mmoja wapo.
Tunatawaliwa na wageni
 
Hakuna mgeni mwanye Huruma na nchi hii.

Wageni kwanza wana hasira ya kuacha makwao na kukosa heshima kwao.
Wageni wanashukuru kuona shamba la bibi lisilo na wenyewe . Na wenyewe hawapo macho wamelala usingizi Fofofo.

Inaelekea humjui vizuri na hujui ufisadi waliofanya . Ni bora hata January.
Januari wanamchafua mana anaonekana ana kawazo ka kushindana na Lisu . Na amini usiamini kuna vitalu Makamba na JPM waligoma kuwanyanganya wachimbaji wadogo lakini mtu wenu alichofanya kinajulikana wakati ni ukuta.

Ni nchi ya waliolala tu ndiyo Panakua na Cheo kikubwa kisicho kuwepo Kikatiba na kinapewa heshima na kupiguwa makofi badala ya kupugwa makofi.

Kumtaja tu kwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu ni kuendesha nchi Kinyume na Katiba. Katiba ni kijitabu tu kilichowaweka madarakani alisikika Mama mmoja akisema kule Manzese.

Tanzania watawala wasipobadilika upepo unaovuma ukanda huu wa Afrika mashariki utavuma kuelekea Tanganyika . Zanzibar ukishavuma na miti sisiyokuwa na mizizi ikanyooka wakawa na katiba yao na nchi yao.

Tanganyika ,Tanganyika nakuoenda kwa Moyo wote. Shoka limekwisha kuwekwa shinani ,na kila mti usiozaa matunda utakatwa na kutupwa motoni.
Matunda ni matendo mema na sio kujikusanyia mali na kugawana mabilioni ya kuza vitalu kwa wazungu.

Na PM asingewekewa breki pale angeibua uozo mwingi.
Majaliwa hoyeeeee!!
Mtangayika mwenzetu hoyeeee.
Msukuma Magumashi na dalali wa wageni ashindwe na alegee .
Hatutaki kuuza mali na ardhi ya wasukuma na watanganyika kwa sababu ya vyeo . Watoto na wajukuu wetu hatutaki waje kuvuta bangi na mabomu ya moshi kama Wakenya, Gen Z. 😂😂😂😂
Mkiendelea kuwasifia hawa wahalifu mtatuudhi watoto wa Mungu na Mungu atashusha adhabu kwenye Taifa hili.

Kumbuka Shoka limekwisha kuwekwa shinani . Na kila mti usiozaa matunda utakatwa na kutupwa motoni.

Sifieni tu majizi .
Bil.40 zitarudi kwa wenyewe.
 
Huyu ndiye mmoja wa wale aliowataja Mkuu wa Majeshi " kuna wahamiaji haramu wameteuliwa kwenye nafasi nyeti" huyu ni mmoja wapo.
Tunatawaliwa na wageni
Ni fisadi wa hatari kabisa. Na machoni pa watu ni kama Bashe.
Hata wayahudi walipokua ugenini kila pahali walichuma mali nyingi sana kwa ajili ya kujenga kwao.

Hakuna mgeni asiyependa kwao alikotoka.
Siwabagui kwa sababu ya asili yao lakini ni wazi kuwa Hawa wanaojulikana kabisa ndugu zao ,shangazi zao ,wajomba zao,babu zao na binamu zao walipo hawafai kupewa vyeo vya juu na kwenye maamuzi ya mustakabali wa rasilimali zetu . Wafanye kazi kama wataalamu kwenye maeneo mengine.

Mgeni nchi ikinuka kwa ufisadi alioufanya atakimbia nchi ndio maana kwa sasa wanawekeza sana Dubai na kwingineko. Wale ni wapitaji na wasaka fursa. Ukifuatilia hata Paroko muuza viungo vya watu sio Mtanganyika. Hakuna muhaya katili kiasi kile.

Kwa sasa hawa wageni hawakomeshi ufisadi zaidi ya kulinda kamba za watu zisikatike ili wale kwa urefu wa kamba yake.

Mleta mada anamsifia huyo mtu wakati tangu amewekwa kwenye nafasi ya unaibu Kaka mkuu ufisadi umepanda kwa kasi kubwa kama vile amekuja kuweka beria ya kumzuia Kaka mkuu asifanye kazi yake.

Yeye pamoja na Kamati ya Nishati walifanya ziara ya Kukagua Mabwawa ya maji mwaka jana na Januari lakini ulikua ni usanii. Kila walikokagua palitengenezwa usanii wa kufungulia maji ili mapendekezo ya serikali kutenga bajeti ya ruzuku ikubalike.
Tukajiuloza ina maana intelijensia yao haiwaambii yanayotendeka au wako bize kumuandama baba Lisu na Msigwa na Sugu na Mbowe!!

Yaani yupo Kaka mkuu na naibu kaka mkuu anayesifiwa kuwa ni kijana machchari haafu Meli ya Sukari irudi na mzigo wake bila kupakuliwa halafu Intelijensia yao isijue huo mchongo na pesa ikatolewa bil.500 kwa mujibu wa taarifa ya mpina na wazalendo wengine walioshuhudia meli ikitinga na sukari magumashi kisha ikaondoka na mzigo wake kama unifomu zilizomng'oa Kangi Lugola (Japo yeye aliingizwa mkenge) ,kosa lake likawa kulidanganya bunge kumbe hana taarifa za uhakika .Bashe amelidanganya Bunge halafu Spika ameridhia wizi wa bil.500 uwe ni halali bila kujiuliza tu kweli Sukari Tani Elfu 60 zisizolipiwa kodi ziingizwe kwenye soko halafu sukari isiuzwe hata Sh.1800?? Inaingia akilini kweli au ni mkakati kamili. ? Nimeichomekea hii mana kila anapotajwa na kutukuzwa Mungu lazima Shetani naye alaaniwe.
 
Umeongea kwa uchungu sana
 
Waziri Dotto Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri mMkuu ameituliza sana Wizara ya Nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na Wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na “amewagawia bandari zote za Tanganyika”.

Kwa hiyo hoja kwamba siyo raia wa Tanzania ni upuuzi mtupu na ni mbinu za mafisadi kumchafua.
Umenena vyema sana. Hoja zao za kijinga tunawaachia wao.
 
Waziri Dotto Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri mMkuu ameituliza sana Wizara ya Nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na Wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na “amewagawia bandari zote za Tanganyika”.

Kwa hiyo hoja kwamba siyo raia wa Tanzania ni upuuzi mtupu na ni mbinu za mafisadi kumchafua.
Mtetea mafisadi na uovu kwenye ubora wako
 
Back
Top Bottom