HOJA: World Cup 2030 -EAC2030?

HOJA: World Cup 2030 -EAC2030?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Natoa hoja kuwa Vyama vya mpira vya nchi za East African Community vipeleke bid yao ya kuandaa mashindano ya FIFA World Cup 2030. Hiyo ni miaka 12 ijayo, ikiwa ni miaka 20 baada ya mashindano hayo kufanyika Afrika; hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa vile mabara yote mengine yatakuwa yameshaandaa mashindano hayo. Iwapo nchi kubwa kubwa kama Tanzania, Kenya na Uganda vitaandaa viwanja vitatu vitatu, na nchi ndogo za Rwanda na Burundi zikaandaa viwanja viwili viliwi, kutakuwa na viwanja 13 vinavyotosha sana kuandaa mashindano hayo. Afrika ya kusini ilikuwa na viwanja 10 wakati Urusi na Brazili waliandaa kwa viwanja 12.

FAIDA za kuandaa mashindano hayo katika ukanda huu zitakuwa ni nyingi sana na zitadumu muda mrefu sana hasa ukizigantia uzuri wa vivutio vyetu vya utalii!
 
Mawazo ya namna yako hayana mashiko kwa utawala wa CCM. Watu wenyewe akili kama Kenya na Rwanda kwao ni bonge la Wazo, Ila hapa Mchafukoge utaonekana takataka tu
Tuwaelimishe basi
 
Mkuu,Kama 2030 fainali zitarudi Africa,Morocco wana nafasi kubwa ya kuandaa ukizingatia walitoswa kwa 2026.Pia tayari wana miundombinu Kama;viwanja bora vya kuchezea na mazoezi,barabara za viwango,hoteli za madaraja ya juu,viwanja bora vya ndege,pamoja na usalama wa uhakika.Vyote hivyo kwa ukanda wetu bado sana.Fikiria leo jiji kama Dar es salaam lipokee wageni laki tano kwa muda wa mwezi mmoja tu,miundombinu inaruhusu?.Labda tuanze kwa kuandaa AFCON kwa pamoja.
 
sipati picha hao wazungu watakavyojazana gesti hausi
 
Tihefu hefu wameshauona Uzi huyu au wamevaa miwani ya jiwe.
 
Natoa hoja kuwa Vyama vya mpira vya nchi za East African Community vipeleke bid yao ya kuandaa mashindano ya FIFA World Cup 2030. Hiyo ni miaka 12 ijayo, ikiwa ni miaka 20 baada ya mashindano hayo kufanyika Afrika; hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa vile mabara yote mengine yatakuwa yameshaandaa mashindano hayo. Iwapo nchi kubwa kubwa kama Tanzania, Kenya na Uganda vitaandaa viwanja vitatu vitatu, na nchi ndogo za Rwanda na Burundi zikaandaa viwanja viwili viliwi, kutakuwa na viwanja 13 vinavyotosha sana kuandaa mashindano hayo. Afrika ya kusini ilikuwa na viwanja 10 wakati Urusi na Brazili waliandaa kwa viwanja 12.

FAIDA za kuandaa mashindano hayo katika ukanda huu zitakuwa ni nyingi sana na zitadumu muda mrefu sana hasa ukizigantia uzuri wa vivutio vyetu vya utalii!
kuandaa kombe la dunia si suala la kuwa na viwanja tu mkuu,
labda useme kombe la Africa
 
Back
Top Bottom