Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulimalizika mjini Beijing wiki iliyopita, ambapo wakuu zaidi ya 50 wa nchi au serikali za Afrika walihudhuria mkutano huo, na kuonyesha kuwa nchi za Afrika zinaupa umuhimu mkubwa mkutano huo na matarajio makubwa ya kuendeleza uhusiano na China.
Hata hivyo, wakati mkutano huu ukibainisha "mapendekezo makuu sita" kwa China na Afrika kuendeleza kwa pamoja mambo ya kisasa na kuandaa mwongozo wa ushirikiano katika hatua zinazofuata, hoja kama "China inamwaga pesa barani Afrika" na "China kutumia fedha kununua kura za nchi maskini" zinaibuka katika vyombo vya habari vya magharibi.
Hivi sasa, "dunia ya kusini", ikiwa ni pamoja na China na nchi za Afrika, inazidi kupaza sauti, kuandika upya mazingira ya kisiasa na kiuchumi ya dunia, na kukuza utaratibu wa kimataifa katika mwelekeo wa haki na wa kuridhisha zaidi. Huu umekuwa ukweli usiopingika na mwelekeo usiozuilika. Baadhi ya nchi za Magharibi zinahofu kwamba nguvu zao zitadhoofika, hivyo zinachochea hatua za "vita baridi vipya" katika maeneo ambayo yamejaa nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na kuendelea kupaka matopo na kuharibu ushirikiano kati ya China na Afrika.
Kutokana na hali hiyo, wakati wa mkutano huu wa kilele, China na nchi za Afrika ambazo zina uhusiano wa kibalozi zimefikia ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati, na China na Afrika pia zimekubaliana kuboresha uhusiano wao kuwa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya. Hii sio tu inaweka wazi umuhimu wa kimkakati wa China na Afrika kwa upande mwingine, bali pia inabeba matumaini makubwa ya viongozi wa China na Afrika kwa urafiki wa kudumu kati ya China na Afrika.
Katika jukwaa la kimataifa, China daima imekuwa ikitetea maslahi ya Afrika, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20 na upanuzi wa "BRICS" kwa nchi za Afrika, na vilevile Afrika pia "imeiunga mkono China" katika masuala mengi ya kimataifa, sababu ni kuwa matakwa ya kisiasa ya China na Afrika yanafanana kiasili, na kuna maelewano ya kina juu ya uingiliaji kati wa nchi za Magharibi na umwamba wa Magharibi.
China na Afrika kuhitajiana sio tu kunabaki katika mambo ya siasa. Kutokana na msaada wa China, nchi nyingi za Afrika zimepata ufadhili wa kujenga miundombinu inayohitajika zaidi kwa ajili ya maendeleo yao.
Katika Mkutano huo wa kilele, viongozi wa China, Tanzania na Zambia kwa pamoja walishuhudia utiaji saini wa "Mkataba wa Makubaliano ya Kufufua Reli ya TAZARA" ili kuwezesha mradi huo wenye ishara kati ya China na Afrika uoneshe ufanisi wake katika enzi mpya haswa kusaidia usafirishaji nje wa maliasili yaliyomo katika Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tanzania, hii itawapa faida nyingi wananchi wa Tanzania. Taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Samia anatarajia kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China hususan katika uwekezaji wa miundombinu na kujenga kwa pamoja pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".
Wakati huo huo, Afrika pia ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya China. Ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Afrika unaendelea kwa kasi, na katika siku zijazo, bara hilo linatarajiwa kuwa soko kubwa linalojumuisha watu bilioni 1.3 na Pato la Dola za Marekani trilioni 3.4, na hii itakuwa ni fursa kubwa kwa China kuuza nje bidhaa, teknolojia na mitaji. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika zimekabiliana na shinikizo kubwa kutoka nchi za Magharibi, hasa Marekani, na kufanya ushirikiano wa karibu na China katika masuala kama vile TEHAMA, uchumi wa kidijitali na nishati safi. Biashara ya makampuni ya mawasiliano ya simu ya China
Barani Ulaya na Marekani imeshuka sana, lakini wamefanikiwa kuchukua sehemu kubwa ya soko barani Afrika, na Afrika imekuwa sehemu muhimu ya vigezo na teknolojia ya China "kutoka nje". Kwa hivyo, Afrika ina jukumu muhimu zaidi katika maendeleo ya uchumi wa China kuliko watu wengi wanavyofikiria, na umuhimu wa Afrika utakuwa mkubwa zaidi.
Kama methali ya Kiafrika inavyosema, “Marafiki wa kweli ni wale wanaosafiri pamoja.” Hivi sasa, China inajiendeleza kuwa nchi ya kisasa kwa mtindo wa kichina huku nchi za Afrika pia zinapata mwamko mpya na kupiga hatua thabiti kuelekea malengo ya kujiamulia mambo ya kisiasa, kujipatia maendeleo, na kujitegemea kupitia umoja.
Kwenye mazingira haya, Mkutano huu wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umeleta zama mpya ambapo China na Afrika zinakwenda sambamba katika kuendeleza mambo ya kisasa, jambo ambalo bila shaka litaanzisha wimbi kubwa la maendeleo ya kisasa katika "dunia ya kusini" na kuandika sura mpya katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.