Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.
Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama
Ni wazi nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji taasisi imara. Sema usiruke kitu kimoja ni kwamba taasisi imara zinaongozwa na viongozi imara, rais ni taasisi, bunge ni taasisi na hata wananchi nao naomba tuwataasisishe kwa ajili ya hoja hii nao ni taasisi.
Utofauti wa mfumo wowote tutakaouchagua utaletwa na asili ya watu wanaoushikilia huo mfumo. Kama
watu hao wataongozwa mioyoni mwao na matakwa binafsi na si maslahi mapana ya taifa basi tegemea nchi kuyumba maana rais mwenye matakwa binafsi atashauriwa na mshauri ambaye kipaumbele chake ni kubakia katika nafasi husika [binafsi]. Haya taasisi ni imara lakini watu wake ni wabinafsi tatizo linabaki palepale
Ndio maana uwe ni ubepari au ujamaa, uwe ni udikteta au demokrasia kama watu hawataamua kuwa na mfumo unaowapa sifa wanaofanya ya maana kwa jamii bado tu tutayumba. Tuige mfano Japan, vitu kama kamikaze ndio vinavyosifiwa huko hata muvi zao unakuta yule mtu anaona ni heshima kujitoa kwa taifa lake. Mtu akilipa kodi kubwa kule ni heshima akiibia wananchi ni aibu kubwa anaweza hata kujiua kabla hajahukumiwa. Kwa hiyo jamii husika itakipata kile kitu inachoamua kukisifia na kukipa airtime zaidi. When you exalt goodness goodness overflows, the same when you exalt shit -shit overflows.
Nawiwwa kuamininkwamba tatizo letu lipo kisaikolojia zaidi kama taifa. Habari zetu ziangaliwe, hata vile viscreenshot vya habari mbovumbovu naona vinaleta madhara zaidi kuliko faida.
Kama labda wenzangu hamjagundua kuwa kipindi kile hatupati habari mbovumbovu, kile cha JPM ile ari ya taifa kiujumla ilianza kuinuka. Sijui kwa wengine. Watu wakaanza kuwa na mawazo ya kujenga zaidi viwanda. Kulipa kodi. Mkuu
Yoda kuna element moja muhimu sana kwenye kujenga taifa nayo ni Trust, TRUST. Sasa watu walio wengi uelewa wao wa mifumo ni duni, na usichokielewa/jua kukiamini inakuwa ngumu. Ndio maana tukipata mtu anayeonekana na akaaminika ni kichocheo kizuri sana cha maendeleo. Ndiyo sababu baadhi ya watu bila kijisanamu hawezi kumuomba Mungu, usimlaumu maana akili yake inahitaji kakitu kanakoshikika mtu anayeonekana ili kuamini.
Nahisi nimeandika sana, na ni kweli nimeandika sana wacha nisumarize; Mifumo imara inajengwa na watu imara, udhaifu tunaouona kwenye mifumo ndio kioo cha kuonesha sisi wenyewe watu tu dhaifu kiasi gani. Hatua zianzie binafsi, kupenda kuwa mtu wa kujitoa, na kusifia matukio ya kujitoa ili hata kama aiai hatutafika hatua za mbali. Watoto na wajukuu wetu watakutana na mazingira yatakayowajenga hivyo