#COVID19 Hoja ya Humphrey Polepole kuhusu thamani ya fedha manunuzi ya chanjo ya COVID-19 ni mfupa mgumu kwa wanasiasa wachumia tumbo

#COVID19 Hoja ya Humphrey Polepole kuhusu thamani ya fedha manunuzi ya chanjo ya COVID-19 ni mfupa mgumu kwa wanasiasa wachumia tumbo

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Polepole kasema haoni thamani ya fedhha (value for money) kwenye pesa ya kununulia chanjo. Hakuna aliyejitokeza kutetea thamani ya fecha inayonunulia chanjo ya corona isiyo na uwezo wa kumlinda mtu hata kwa miezi 6 tu

Hoja ya Polepole ni hii; Bei ya chanjo ni Tsh 51,000/=. Watanzania tuko milioni 60. Kwa sasa watalaam wanasema herd immunity inafikiwa iwapk asilimia 70 watachanjwa!

Kwa hiyo lazima watanzania 42,000,000 wachanjwe!! Kwa hiho pesa inayohitajika ni sn 51,000/= × 42,000,000 = 2,142,000,000,000/= yaani trilioni 2.142.

Lakini hakuna mtu antakayewsza kjkuambia kwa uhakika hiyo iliyotugharimu trilioni mbili na ushee itatukinga kwa muda gani?

Waliotangulia kuchomwa hiyo chanjo haikuweza kuwakinga hata kwa miezi sita na wakachomwa nyingine!! Pia hiyo ya pili haikuwakinga na sasa Marekani wanaambiwa wachomwe ya tatu!

Baada ya hapo wawe wanachomwa boosters!! Hapo thamani ya fedha iko wapi?

Halafu unaingia gharama yote hiyo kwa ugonjwa wa mafua ambao wanaougua hupona kwa asilimia 98%!
 
Kama issue ni value for money ntamjibu ifuatavyo.

Kwanza hauhitaji kuchanja watu million 60 maana zaidi ya 40% hapo ni watoto below 18 years ambao risk ya kupata ni ndogo kuliko adults. So usipige hesabu za jumla hivyo.

Kuna misaada ya zaidi ya trillion 2 inapatikana kwa ajili ya covid relief so inaweza kufund. Yaani hela ya beberu unatumia hyo hyo kununua dawa ya beberu sasa tunapata hasara gani kama taifa?

3. Ukipiga hesabu za Trillion 2 sasa anaweza piga thamani ambayo labor inayoumwa/kufariki sababu ya corona ingezalisha kwa muda ambao wanaugua? Kama engineer anazalisha million 200 ya thamani ya kazi zake kwa mwaka, akifariki kwa Covid je unapigaje hesabu ya Value for money iliyopotea sababu ya kifo chake??

Kama issue ni gharama hata mashine na vifaa/skilled manpower za kufanya chemotherapy au radio therapy kwa wagonjwa wa kansa ni bei juu sana ila mbona hawajawahi isitisha licha ya kwamba wanaotumia tiba hyo 80% huishia kufariki tu ma hta wakipona wana long term effects?

Hizi double standards huwa kwa faida ya nani?
 
Unamaanisha tumepigwa tena mchana kweupe?
Tumepigwa mchana kweupe huku tumefumbua macho. Leo tumeambiwa tumepewa mkopo na IMF wa matrilioni ya shilingi, ili kupambana na corona!

Can you imagine!! Ugonjwa ambao asilimia kubwa ya wanaoambukizwa hupona bila hata kujua kuwa walishawahi kuambukizwa!!

Wengi pia huugua kidogo mafua na kikohozi!! Wachache sana wanaoelemewa na corona ni wale ambao tayari ni waathirika wa magonjwa mengine kama vile pumu, kisukari, mago jwa ya moyo, presha ya kupanda na kushuka nk. Corona haijawahi kumdhoofisha mtu mwenye afya njema!! Huo ndio ugonjwa wa kuhalalisha Taifa liingie kwenye madeni makubwa halafu na kinga yenyewe haipatikani!!

Njooni hapa mawakala na wapiga debe wote wa chanjo mtuoneshe thamani ya pesa inayonunua chanjo isiyoweza kumkinga mtu hata kwa miezi 6, dhidi ya ugonjwa unaoua kwa asilimia pungufu ya 2%.
 
Kuna wakati inafaa hoja ijibiwe kwa hoja mkuu wangu.
Wasiokuwa na hoja au jibu kama mimi naishia kusoma koments
Kuna majitu mapumbavu mengi sana Jamii forums, hawaangalii hoja iliyoletwa wanaangalia nani kaongea, ikiletwa thread ya mtu wanayemkubali hata Kama ni pumba na mashudu wanasapoti tu. Ingawa wapo baadhi wanaotumia common sense. Wengine wengi upeo wa kufikiri upo chini sana.
 
Kuna majitu mapumbavu mengi sana Jamii forums, hawaangalii hoja iliyoletwa wanaangalia nani kaongea, ikiletwa thread ya mtu wanayemkubali hata Kama ni pumba na mashudu wanasapoti tu. Ingawa wapo baadhi wanaotumia common sense. Wengine wengi upeo wa kufikiri upo chini sana.
Too much politiks and ushabiki jombaa,...hii inazaa taifa zembe kufikiri
 
Hadi leo tarehe 8/9/2021 kwa mujibu wa takwimu rasmi jumla ya waliowahi kuambukizwa virusi vya corona ni 222,812,592. Waliodaiwa kufa kwa corona ni 4,601,142. Kwa hiyo waliodaiwa kufa kwa corona ni asilimia 2.065% tu. Kwa takwimu hizo covid 19 haimo katika orodha ya magonjwa 10 yanayoongoza kwa kuua hata huko marekani inakopigiwa debe sana corona!

Kitakachotokea mabeberu wanatufanya tena watumwa!! Hata tukifanya kazi kwa bidii namna gani, kipato chote kitaenda kwao kwa kugharimia "mapambano" dhidi ya ugonjwa hewa!!! Fikiri kidogo tu.

Watanzania tunavyobanana kwenye dala dala bila barakoa!! Tumekimbiza mwenge na mikesha ya mwenge wengi hawana barakoa!! Kwenye mipira tunabanana bila barakoa,, ingekuwa covid 19 ni ugonjwa halisi si tungekwisha!! Inauma sana!!
 
Back
Top Bottom