#COVID19 Hoja ya Humphrey Polepole kuhusu thamani ya fedha manunuzi ya chanjo ya COVID-19 ni mfupa mgumu kwa wanasiasa wachumia tumbo

Hakuna msaada wa trilioni 2!! Nani atakupa msaada wa trilioni 2?? Weka ushahidi hapa kama tumepewa msaada wa trilioni 2!! Hivi wewe unawajua mabeberu au unawasikia tu!! Watoto wanahitaji kuchanjwa japo hawapo hatarini kwa sababu usipowachanja wataendelea kuwaambukiza watu wazima!! Ujue chanjo ya corona haizuii maambukizi!!
 

Sasa wanaosemaga ni biashara nashindwa kuelewa, yaani mtu akuuzie chanjo za Trillion 2 alafu muda huo huo anakupa trillion 1.2 za mkopo? Sasa ni biashara au hasara? Mind you uchumi wake nao umepungua sababu uzalishaji umeshuka so hasara ni nyingi kuliko faida ya kuuza chanjo. Reasoning ya polepole ina walakini ama anapotosha maksudi tu akijua waTZ hawana elimu ya kutosha.

Unadai chanjo ya corona haizuii maambukizi ila unasahau tatizo ni delta variant.... Chanjo ilitengenezwa kwa zile conditions za mwanzo hawa kupredicy variant zingine ambazo hata hazihisi chanjom mfano israel 90% ya walioambukizwa baada ya chanjo ni delta variant but hizi boosters zimeonyesha mafanikio dhidi ya Delta. Mind you hta waliolazwa na mitungi ya gesi kwa waliochanjwa wengi ni above 60 ambao wana underlying diseases kibao delta ikiwashika inawapeleka mputa.
 
Wewe ndio unadhihirisha ujinga wako wala hoja yake haija base kwenye gharama tu maana tatizo sio gharama ila inadumu kwa muda gani?
Haingii akilini kila baada ya mwaka tutumie zaidi ya trillion kwenye huduma ambayo madhara yake ni pungufu ya 1%
Lazima tufikiri kwa namna yetu na njia yetu kujiondoa kwenye mtego wa kuwa watumwa wa mabeberu
 

Acha ujinga wewe izo pesa tulizopewa ni za mkopo fuatilia zaidi acha kuwa mjinga izi zama
 
Acha ujinga wewe izo pesa tulizopewa ni za mkopo fuatilia zaidi acha kuwa mjinga izi zama
Twende taratibu haina haja ya matusi.... Mtu anakwambia chanjo ni trillion 1 alafu akukopeshe trillion 1 sasa anafikiaje lengo lake la kuingiza faida ilihali faida anayotaka anakupa tena ww kwa mkopo? Ambao kwa risk yake unaweza usilipwe wote? Or rather ukalipa kwa miaka hata 20!! Faida anai realise vipi?

Kingine pia Nimehoji hasara walizopata kwenye uchumi wao zinaweza kuwa recouped kwa mauzo ya chanjo? Yaani pato la taifa liporomoke, ajira zipotee alafu biashara ya chanjo ndio irejeshe hizo hasara? Yaani mtuelezee faida wanaingizaje ilihali loss za pandemic ni zaidi ya Mamia ya Trillion?
 
Title inasema value for money and hoja yangu imejikita hapo sasa ujinga unatka wapi?

Unasema madhara ni below 1% nimekuuliza unajua value for money inayopotea hta kwa hyo 1% wanaofariki au kuugua?? Unajua biashara ngapi zimekufa tokea Covid 19 iwepo hta kma waliougua Tz ni below 1%? Unajua export/import value ngapi zimepotea??

Unasema tufikiri kwa namna yetu? Unadhani suluhu ni ipi kwa mfano? Maana naona lawama tu kwa mzungu ila ukiulizwa chanjo ngapi mmeshatengeneza hapa TZ kumaliza Covid 19 hauna jibu? Mbona china na russia wana zao? Umeona wananunua za mabeberu??

Tusijione tuna akili sana kuliko hta WHO!! ilihali unaowaita mabeberu ndio wamekupa hta hyo smartphone unayotumia kukashifu.
 
Bado kuna watu wanaamini hesabu za pole pole.

Toka avuruge zile za CAG alizihoji 1.5 trillion amekuwa hana maana
 

Hii akili angeitumia wakati wa Mwendazake pia, mshenzy tu anamhujumu rais kwa sababu Hakuna maslahi.
 
Na cha kusikitisha zaidi ni rahisi vilevile kupenyeza magonjwa/ madhara mengine kwetu kupitia chanjo! Namkumbuka sana genius wetu, the late mzee baba.
 
Watoto hawachanjwi muwe mnafanya tafiti kabla ya kuja huku. Na kila chanjo ina umri elekezi
 
Ukisema almost 40% ni watoto, unasahau hii nchi population kubwa ni vijana ambao survival rate ni 98%.

Kama ni hivyo kuna haja gani ya kupambana na ugonjwa huu ambao kwa nchi yetu bado mortality rate ni ndogo kulinganisha na malaria.
 
Corona inalazimishwa tu Tanzania hata yenyewe haitaki, angalia mikusanyiko ya watu kila mahali,ingekuwa Corona ile inayovuna Ulaya na Marekani robo ya Watanzania wangekuwa hawapo.

Ajabu zaidi wanaopona ni wengi zaidi,hawataki kuusema ukweli huu,wanataka kutuaminisha ukipata tu Corona utakufa.
Wanataka nchi ziogope ili ziendelee kukopa.

Wananchi ndiyo maana wamepuuza chanjo na barakoa.Viongozi wanaolazimisha Delta ya India ije na imegoma watajiju wenyewe.
Maamuzi ya hovyo kabisa.
 
Mzee polepole ulishashuhudia lini ngozi nyeusi ikasumbuliwa na mafua ya msimu......huo ni ugonjwa wa mabeberu, lakini wanataka kuchezesha ngoma dunia nzima, naunga mkono hoja hakuna value for money wala dharura yoyote ya kiafya...........
 

Hizi ni hoja mfu, potofu kabisa, purely theoretical..

Hadi sasa ni watu karibu laki 4 tu wamechanjwa.. Mostly, serikali ikijitahidi, watachanjwa watu mil 1 au 1.5 tu haiwezi zidi hapo, sbb kuna hiari, hiari hii inamfanya mtu yeyote asichanje au achanje, yaani ni uhuru wako tu.

So haiwezi fikia milele hiyo idadi Polepole anayosema. Huyo polepole naona anatafuta kufukuzwa CCM haraka sana.

Naona anazidi kuichonoa serikali ya Mama Samia, ila naamini, 2025 asahau ubunge au nafasi yoyote, his time in CCM or Government was over, ila naona hataki kukubali au kuelewa hilo, anapambana tu. Bahati mbaya, huwezi shindana na Mh. Rais.
 
Kwa hesabu za ROBOT, Polepole, wakiugua watu million kumi halafu wakafa watu laki mbili basi sikitu! (... yaani hata kuwakumbuka wahanga wa MV BUKOBA kwa Polepole ni upuuzi!)
... HALAFU ROBOT HILI LINAFUNDISHA UONGOZI WA BINAADAM! ... ONLY IN TZ!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…