Hoja ya Kitila Mkumbo kuhusu mapambano ya Katiba Mpya

Hoja ya Kitila Mkumbo kuhusu mapambano ya Katiba Mpya

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Mwalimu Kitila Anasema Kwamba

Mapambano ya katiba mpya hayapaswi kuongozwa na wanasiasa, yanapaswa kuongozwa na Civil societies.

Ikitokea mfano mchakato ukiwa umeshikiliwa na ChademaTz,mimi kama mwana CCM siwezi kuunga mkono kwa sababu intially ntakuwa suspicious kwamba wanataka kunitoa madarakani.

Nadhani Hoja ya KITILA IPO SAHIHI KABISA LAKINI HAINA APPLICABILITY KWA SASA.
 
Civil society zipo chini ya wizara ya GWAJIMA.
.
Sidhani kama kuna civil society kwa sasa inanguvu ya kuongelea mambo kama hayo japo kuwa ni moja ya theme ya GOOD GOVERNANCE

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hata hizo Civil Societies zenyewe baadhi zina mafungamano na baadhi ya vyama vya siasa!

Kinachotakiwa ni kutanguliza tu mbele maslahi ya Taifa, kama walivyofanya akina Jaji Warioba kwenye ile Tume yao ya kukusanya maoni ya Katiba.
Anaweza tofautisha civil societies from politicians!?

Civil societies ni akina nani!?

Politicians hawawezi kuwa sehemu ya Civil Societies!?

Mapambano ya kudai katiba Mpya since 1991 under NCCR- kama wanaharakati iliyozaa NCCR-MAGEUZI na baadae Sheria ya kwanza ya vyama vya Siasa ni zao la hizo Civil Societies.

Yeye mwenyewe pale UDSM kwenye kongamano la Katiba Mpya akitoa maoni yake juu ya Muundo wa Serikali ilikuwa ni zao la Civil Societies kama Redet, Jukwaa la Katiba, TEC etc.

Huwezi tenganisha Civil Societies na Politicians katika mapambano ya haki na utawala wa Sheria.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu Kitila Anasema Kwamb
.
Mapambano ya katiba mpya hayapaswi kuongozwa na wanasiasa,yanapaswa kuongozwa na Civil societies.
.
Ikitokea mfano mchakato ukiwa umeshikiliwa na ChademaTz,mimi kama mwana CCM siwezi kuunga mkono kwa sababu intially ntakuwa suspicious kwamba wanataka kunitoa madarakani.
.
Nadhani Hoja ya KITILA IPO SAHIHI KABISA LAKINI HAINA APPLICABILITY KWA SASA.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kitila ni kichaa maana Civil societies zenyewe zimejaa UVCCM tupu
 
kama raia wanaounda Civil Societies wana vyama wanavyoviunga mkono na kufanya navyo kazi ni ngumu sana kupata neutral agents!

iko wazi kama hauko sisiem uko upinzani, huu ni mchakato wa kisiasa unawezaje kuwaweka pembeni wanasiasa?

Yaani unataka wachezaji wa kigeni kina Mayele wapunguzwe ili George Mpole awe mfungaji bora na wananchi wasiteteme maana wanakukera halafu kikao cha maamuzi kisiwahusishe wajumbe toka Yanga,Simba na TFF.

Huu usomi wa kukariri ni shida sana!mbona kama ameongelea jalalani bila kufikiria kiprofessa? Ametuaibisha UDSM Nkrumah hall where revolutionary ideas are born!
 
KUNA CIVIL SOCIETY MOJA MIAKA KAMA SITA NYUMA ILIKUWA INAJIHUSISHA NA MASUALA YA KISIASA.

Nafikiri mnaelewa kilicho wakuta na walikuwa mfano kwa civil society nyingine.

Kazi ya civil society ni kutoa tu elimu sahihi kwa jamii au huduma Fulani kwa jamii na haitakiwi kuwa upande wowote ule wa kisiasa na hazitakiwi kunihusisha na siasa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu Kitila Anasema Kwamb
.
Mapambano ya katiba mpya hayapaswi kuongozwa na wanasiasa,yanapaswa kuongozwa na Civil societies.
.
Ikitokea mfano mchakato ukiwa umeshikiliwa na ChademaTz,mimi kama mwana CCM siwezi kuunga mkono kwa sababu intially ntakuwa suspicious kwamba wanataka kunitoa madarakani.
.
Nadhani Hoja ya KITILA IPO SAHIHI KABISA LAKINI HAINA APPLICABILITY KWA SASA.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
MKUMBO ni TIMU MAGUFULI aka SUKUMA GANG

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Unachotakiwa kujua ni kwamba hata hivyo vyama vya wafanyakazi vina Uccm na UCHADEMA, Ni sawa kabisa na jinsi Simba na Yanga zilivyoigawa jamii ya wanamichezo!

Ukienda Mbeya City au Kagera Sugar utakuta kuna viongozi na wachezaji wengine ni wafuasi wa Simba na wengine Yanga! Vivyo ndani ya TFF kwenyewe wapo Simba na Yanga, Hivyo wakati mwingine hata maamuzi yao yanaathiriwa na hiyo kitu!

Kwa hiyo hata hivyo vyama kuna watu wana mtazamo na mrengo wa CHADEMA huku wengine wanaskilizia CCM inasemaje?

Pia tangu asili watumishi wamefanywa na katiba kuwa waoga sana wa kufanya siasa au harakati zozote zenye kutishia maslahi ya chama tawala, Hivyo ni ngumu sana kwa mazingira ya Tanzania harakati kama hizo ziongozwe na taasisi kama hizo!
 
Ni vizuri Msomi anapoongea anatolea na mfano nchi ambazo zilifanikiwa kupata katiba mpya kupitia civil sociaety Visa vis nchi ambazo zimefanikiwa kwa kutumia vyama vya siasa.

Huyu Nkumbo akubali wakati wake umeshapita, Alipata bahati kwa Magufuli kwahiyo arudishe shukrani kwa Mungu maisha yaendelee kama siasa aje kivingine hakuna teuzi tena ndani ya ccm. CCM INA WENYEWE NA WENYEWE NDIO SISI
 
ipi hiyo?
KUNA CIVIL SOCIETY MOJA MIAKA KAMA SITA NYUMA ILIKUWA INAJIHUSISHA NA MASUALA YA KISIASA.

Nafikiri mnaelewa kilicho wakuta na walikuwa mfano kwa civil society nyingine.

Kazi ya civil society ni kutoa tu elimu sahihi kwa jamii au huduma Fulani kwa jamii na haitakiwi kuwa upande wowote ule wa kisiasa na hazitakiwi kunihusisha na siasa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu Kitila Anasema Kwamba

Mapambano ya katiba mpya hayapaswi kuongozwa na wanasiasa,yanapaswa kuongozwa na Civil societies.

Ikitokea mfano mchakato ukiwa umeshikiliwa na ChademaTz,mimi kama mwana CCM siwezi kuunga mkono kwa sababu intially ntakuwa suspicious kwamba wanataka kunitoa madarakani.

Nadhani Hoja ya KITILA IPO SAHIHI KABISA LAKINI HAINA APPLICABILITY KWA SASA.
I don't know how that'll work. Kuna wakati serikali ililalamika kuwa baadhi ya NGOs/CSOs zinajihusisha na mambo ya siasa na kutishia kuzifuta zikiendelea na mwelekeo huo. Nafikiri mojawapo ni LHRC. Zamani zaidi ilikuwa BAWATA ya mama Tibaijuka kabla hajaenda UN na yenyewe ikafa.

Serikali haitaki katiba ya maana, hilo ndilo tatizo kubwa. Hiyo suspicion ya kutolewa madarakani haina maana wakati uwanja wa kujadili mambo yote ya msingi upo wazi kwa wadau wote. Ni yule tu anayetaka kubaki madarakani by hooks and crooks ndiye atatoa kisingizio cha ovyo namna hiyo.

Halafu sidhani kama ni sahihi kusema vyama vya siasa vinaongoza mapambano ya katiba. Hiyo inaonekana kwa vile CCM wanataka kuzuia hitaji kubwa la wananchi bila sababu za msingi. Vinachofanya ni kupambania ajenda ya katiba mpya IWEKWE MEZANI na mchakato ufanyike. How? ni suala la muafaka wa nchi nzima kwa namna itakayokubalika na wadau wote. Kitila aache uzuzu.
 
Back
Top Bottom