Wanabodi,
Kila nipatapo nafasi, huja na hoja za " Kwa Maslahi ya Taifa" zenye lengo la kuhamasisha uzalendo kwa nchi yetu, Mada ya leo, naizungumzia idadi ya kweli ya waliokufa kwa Corona Tanzania mpaka hapa ninapo andika bandiko hili, Tanzania wamekufa watu 16 tuu kwa ugonjwa wa Corona!, Kubali, Kataa, lakini huo ndio ukweli mpaka pale itakapo tangazwa tena update nyingine ambayo itatolewa leo na hoja kuu ya bandiko la leo hizi hoja na tuhuma za kuwa serikali yetu inaficha idadi halisi ya vifo vya watu wanakufa kwa Corona, wanaokufa ni wengi, lakini idadi inayotangazwa na serikali ni idadi ndogo, hivyo taarifa ya serikali ni taarifa ya uongo, idadi inayotangazwa na serikali ni idadi ya uongo!, jee rais wa JMT ni muongo?!, jee Waziri Mkuu wa JMT ni muongo?!, Jee Waziri wa Afya ni muongo?, Jee wataalamu waliochunguza na kutoa taarifa hiyo ni waongo?. Jibu ni hapana, data za idadi ya vifo inayotokewa na serikali ni data za ukweli.
Natoa wito nawaomba Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo wa ukweli wa nchi yetu, tuiaminie taarifa ya serikali yetu, kuwa idadi vifo 16 iliyotolewa na serikali kuwa ndio pekee waliokufa kwa Corona mpaka sasa nchini Tanzania, ni idadi ya ukweli wenyewe kabisa na halisi, ambayo ndio ya watu waliopimwa na kuthibitishwa wamekufa kwa ugonjwa wa Corona, ila pia kuna watu wengine wengi tuu na wanakufa kwa magonjwa mengine, na inawezekana miongoni mwa hao wanaokufa kwa magonjwa mengine ikiwemo haya ya matatizo ya kupumua, pia Corona imechangia, ila hawaja pimwa na kutthibitishwa kuwa ni Corona, hivyo mpaka sasa ninapoandika bandiko hili asubuhi hii, idadi rasmi ya vifo vilivyotokana na Corona na kuthibitishwa na serikali yetu ni watu 16 tuu na huu ndio ukweli wenyewe halisi, kubali, kataa, ndio ukweli.
naomba uandamane nami.
A Way Forward ya Nini Kifanyike
Korona ni Janga, Ni Vita, Vita Ikiisha Tangazwa, Amri ni Moja, Umoja, Mshikamano, Ushirikiano Ndio Siri ya Ushindi!-Korona ni janga, ni vita, vita ikiishatangazwa, ili tushinde vita hii ni lazima viongozi wetu wa serikali, wanasiasa, wapinzani, wataalamu, wote tuzungumze kwa kauli moja, Amiri Jeshi Mkuu akiishasema waliokufa ni 16, sheria ya kivita inatumika, walikufa ni 16!, hata kama umeona na kushuhudia miili 100 inazikwa!, bado utasema ni waliokufa ni 16 tuu!. Leo Waziri Mkuu wtu katangaza idadi ya 16, halafu kesho anaibuka mtu mwingine kuleta idadi ya vifo vya mitandaoni!, what does this mean?. Tutawachanganya Watanzania!, hizi idadi za kwenye mitandao, tuachieni sisi watu wa mitandaoni, kwenye hili lazima serikali, wapinzani mzungumze kwa kauli moja kwa maslahi ya taifa!
Serikali Isijimilkishe Vita Hii ya Corona Kuifanya ni Vita Yake!, Vita Hii ni ya Watanzania Wote, Serikali Ifanye Ushirikishwaji!- Tangu janga hili limeanza, serikali ndio imehodhi ukamanda na wapiganaji wa vita hii, kwa kuunda kamati 3 za kiserekali za kushughulikia, 1 Mawaziri, 2. Wakatibu Wakuu 3. Wataalamu. Mawaziri ni ya serikali, Makatibu Wakuu ni wa Serikali, hao wataalamu ni kina nani?, hakuna ushirikishwaji umma, hivyo sasa uindwe kamati ya kitaifa, kwa serikali kuomba ushirikishwa wa Watanzania wote wenye mawazo yoyote chanya ya kusaidia, wakiwemo wa Diaspora, wayalete on line, out of mawazo hayo, inaundwa kamati shirikishi ya kitaifa ambayo itajumuisha sekta zote, sio hali ilivyo sasa, vita hii inaweza kuwa inaongozwa na Goliati, kumbe kina Daudi wapo na wamejinyamazia kwa sababu hawajashirikishwa!. Haiwezekani Waziri Mkuu ataje idadi ya vifo 16, halafu kesho yake waziri mkuu kivuli kuibuka na kusema serikali inasema uongo. Ile kanuni ya a collective responsibility inakuwa applicable kwenye hili la Corona tuongee kwa sauti moja na kupigana kwa nguvu moja.
Uwezo wa Serikali yetu kutoa elimu kwa umma ni mdogo, kama zilivyo vita nyingine zote, ma verenani huitwa kwenye kupanga mikakati, sisi ma veterani kwenye sekta ya media tupo, tuitwe, tushirikishwe, miongoni mwetu kuna mabingwa wa utoaji elimu kwa umma, tuwe recalled turudi newsrooms tukawasaidie hawa vijana wa sasa suala zima la utoaji wa elimu ya umma, hili lingefanyika tangu mwanzo, tungewasaidia sana Watanzania, ila hadi hapa tulipo, hatujachelewa!. Media zetu hazina uwezo wa utoaji elimu, hivyo media ziwezeshwe, maveterani tuitwe turudi newsroom tusaidie.
Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakaini kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote, kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Rais wetu asiwabeze viongozi wa dini kwa kutumia maneno ya ushetani, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani.
Kwa vile mpaka sasa Corona haina kinga wala tiba, naunga mkono juhuzi zote zinazochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na janga hili, tuendelee kufuata ushauri wote wa kitaalamu unaotolewa katika kukabiliana na janga hili, na kwa vile Corona ni adui asiyejulikana, tutumie silaha zote za ki hospitali za kiimali. tiba asili, tiba mbadala, na hata akitokea mtu akaotoshwa chochote, tusidharau, na hata kama ni kweli uchawi upo, na wachawi wapo, waruhusiwe kuiloga Corona ife iishe tuendelee na maisha yetu.
Hitimisho.
Watanzania Tuiaminie Serikali Yetu, Serikali ni Wakweli, Data za Serikali ni za Kweli.
Namalizia kwa ule wito wa mwanzo wa bandiko hili, nawaomba Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo wa ukweli wa nchi yetu, tuiaminie taarifa ya serikali yetu, kuwa idadi vifo 16 iliyotolewa na serikali kuwa ndio pekee waliokufa kwa Corona mpaka sasa nchini Tanzania, ni idadi ya ukweli wenyewe kabisa na halisi, ambayo ndio ya watu waliopimwa na kuthibitishwa wamekufa kwa ugonjwa wa Corona, ila pia kuna watu wengine wengi tuu na wanakufa kwa magonjwa mengine, na inawezekana miongoni mwa hao wanaokufa kwa magonjwa mengine ikiwemo haya ya matatizo ya kupumua, pia Corona imechangia, ila hawaja pimwa na kutthibitishwa kuwa ni Corona, hivyo mpaka sasa ninapoandika bandiko hili asubuhi hii, idadi rasmi ya vifo vilivyotokana na Corona na kuthibitishwa na serikali yetu ni watu 16 tuu na huu ndio ukweli wenyewe halisi, kubali, kataa, ndio ukweli.
Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali