Hoja ya kuwa Rais Magufuli anapendelea Chato haina mashiko

Hoja ya kuwa Rais Magufuli anapendelea Chato haina mashiko

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
Hoja ya kuwa Mgombea Wetu Rais Magufuli anapendelea Chato hazina Mashiko :-
1.-1.jpg

1. Ikulu ya Chamwino -ni Chato?

2. Hospital za Rufaa za Kanda Mtwara na Mara ni Chato?

3. Reli SGR-inafika Chato?

4.Bwawa Kubwa la Kuzalisha Umeme liko Chato?

5. Flyover -Ziko Chato?

6. Cherezo za Meli-ziko Chato?

7. Hifadhi ya Wanyama ya Chato eneo kubwa lipo Kagera -Nayo ni Chato?

8. Meli ya MV Victoria na vivuko ziwa Nyasa -Vinafika Chato?

9. Elimu bure -ni kwa Chato tu?

10. Mama Ntilie, Machinga na bodaboda wasiosumbuliwa ni wa Chato tu?

11. Umeme wa REA ni vijiji vya Chato tu?

12. Rada za kuongoza ndege zipo Dar,Mwanza na Mbeya -Nazo ni Chato?

13. Ndege mpya 11 nazo ni za Watu wa Chato?

14. Mradi wa Barabara za Kuzunguka Mji Dodoma (Ring road) - Nayo ni Chato?

16. Ujenzi wa Mji wa kiserikali Dodoma -Nayo ni Chato?

17. Ujenzi wa hospital kila wilaya -nayo ni Chato?

18. Ujenzi wa Barabara kiwango cha Lami kuunganisha mikoa ya Katavi, Tabora na Rukwa -Nayo ni Chato?

19. Ujenzi wa flyover ya Salender -Coco beach -Nayo ni Chato?

20. Ujenzi wa Daraja la kigongo ferry -Nayo ni Chato?

21. Ufufuaji wa Reli kutoka Dar -Arusha na Moshi-Nayo ni Chato?

22. Ujenzi wa Barabara za lami ndani ya makao makuu za mikoa yote! Nayo ni Chato?

23. Mradi wa Uwanja mkubwa wa ndege Msalato Dodoma -Nayo ni Chato?

24. Mradi mkubwa wa Maji -Ruvu -Nayo ni Chato?

25. Daraja la mto Wami kwenda mikoa ya Kaskazini -Nayo ni Chato?

26. Upanuzi wa Bandari za DSM na Mtwara -Nayo ni Chato?

27. Ujenzi wa bomba la Mafuta ghafi -Hoima hadi Tanga -Nayo ni Chato?

Iko Miradi chungu nzima inayotekelezwa nje ya Wilaya ya Chato unaweza ongezea. Itoshe tu kusema Mheshimiwa Rais hana cha kulaumiwa. Hawa watu hawachelewi kuuliza mbona CORONA haiui watu wa Chato!!

Nitamsemea Rais wangu, Rais wetu mpendwa Dr JPM , nitamuombea usiku na mchana ili wenye wivu wasijinyonge bali waelewe.
Kura yangu nitampa.
 
-Kuna uhusiano wowote wa Rais kuwa mzawa wa Chato na uwanja kujengwa Chato?JPM asingekuwa mzawa wa Chato,uwanja ungejengwa huko kwa mazingira ya sasa?
Nashindwa kutenganisha uhusiano huo!
-Vipi kuhusu bandari?
-Vipi kuhusu hospitali ya rufaa ya kuhudumia kanda?

*Kuna miradi ambayo ikienda Chato wala hakuna anayeweza kushtuka!Miradi kama Umeme,maji,barabara,hospitali,zahanati,shule nk!
Lakini hii miradi ambayo haina tija,hapana kwakweli!Huu ni upendeleo wa wazi!
Hayo uliyotaja hata kama mtu hakubaliani na mojawapo lakini anaweza akaona kuna logic kuitekeleza!
Lakini hili la uwanja Chato,hapana,hapana hapana!
Ni matumizi mabaya ya kodi za watanzania!
Tuwe wakweli,mteja wa uwanja huo ni JPM mwenyewe!
 
Ngoja tumwambie Lissu apige zaidi spana aisee...... Watu wanaweweseka tu kwa sasa
Kila anayejaribu kujibu anaonekana hajajibu kisawasawa,warudi chemba waje na majibu ya pamoja maana kwasasa kila mtu anasema lake!Mwingine anasema haendi na uwanja kaburini,wengine ndio kama hivi,wengine ni mkakati wa miaka 50 ijayo!Yaani majibu yao vichekesho tu!😁😁!Lissu apige spana nyingine hapo hapo,kuna watu watavaa boxer kichwani!
 
Mkuu ,Miradi mingi uliyo itaja ipo au ilijengwa huko ilipo kwa Sababu za kimazingira/kibiashara kimahitaji na kiusalama zaidi.

Nilicho kiona hapa ni wewe kujing'ata Mkia wako mwenyewe ,kajipangeni tena mje na Majibu sahihi.
 
Watu wanapasema sana chato,natamani nipatembelee Na hasa nikauone huo uwanja wa chato.nitaenda kwa ndege ya ATCL bila Shaka wana route ya huko
 
-Kuna uhusiano wowote wa Rais kuwa mzawa wa Chato na uwanja kujengwa Chato?JPM asingekuwa mzawa wa Chato,uwanja ungejengwa huko kwa mazingira ya sasa?
Nashindwa kutenganisha uhusiano huo!
-Vipi kuhusu bandari?
-Vipi kuhusu hospitali ya rufaa ya kuhudumia kanda?

*Kuna miradi ambayo ikienda Chato wala hakuna anayeweza kushtuka!Miradi kama Umeme,maji,barabara,hospitali,zahanati,shule nk!
Lakini hii miradi ambayo haina tija,hapana kwakweli!Huu ni upendeleo wa wazi!
Hayo uliyotaja hata kama mtu hakubaliani na mojawapo lakini anaweza akaona kuna logic kuitekeleza!
Lakini hili la uwanja Chato,hapana,hapana hapana!
Ni matumizi mabaya ya kodi za watanzania!
Tuwe wakweli,mteja wa uwanja huo ni JPM mwenyewe!
Nasikia wanajenga na uwanja mkubwa wa mpira ili wavutie watalii.
 
Nyie jamaa ni shida sana, kajipange tena, Mh Lissu piga spana nyingine hawa vilaza wazidi kupoteana
 
Back
Top Bottom