Hoja ya kwanini Fred akubalike zaidi Isimani badala ya alipozaliwa ni ya kipuuzi iliyojaa ukabila, ukanda na ubaguzi

Hoja ya kwanini Fred akubalike zaidi Isimani badala ya alipozaliwa ni ya kipuuzi iliyojaa ukabila, ukanda na ubaguzi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Inashangaza sana leo karne ya 21 iliyo kasi zaidi kiteknolojia kuna watu hasa wa upinzani wanaojenga hoja kwanini Fred Vunjabei akubalike zaidi Isimani kuliko Kalenga alipozaliwa mara baada ya kushinda kura za maoni hatua ya kwanza. Haya ni mawazo ya hovyo yaliyojaa ubaguzi wa kijinga kupitiliza. Nimeshtushwa mno na hizi fikra za kijima.

Wakati tunawalaumu wazungu kwa ubaguzi ninadhani TUJISAHIHISHE kwanza sisi wenyewe. Vinginevyo tutaendelea kuwa nyuma sana kidemokrasia, kimaendeleo na kisiasa. Kinachosikitisha zaidi ni hizi fikra kusambazwa na watu wa vyama vya upinzani ambao tulitegemea ndo wawe mstari wa mbele kutokuwa na fikra kama hizi.

Tuige Zambia iliyowahi kuwa na makamu wa Rais mzungu kwa jina Guy Scott. Je, sisi hapa kama Fred tu tunambagua vipi kuhusu mtanzania mwenye asili ya Ulaya au Asia kuwa kiongozi?

Pongezi kwa watu wa mkoa wa Arusha wasioangalia mgombea ubunge ni mzaliwa wa wapi ili mradi ni mtanzania. Mwaka 1995 mzaliwa wa wilaya ya Mbulu Padri aliyeasi Wilbroad Slaa alichaguliwa kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha. Mwaka huohuo Makongoro Nyerere akawa mbunge wa Arusha mjini.
 
Sema ni vizuri watu kuhoji ila isiwe kwa nia mbaya, kilichobaki tusubirie maaamuzi kutoka kwa mafisadi papa wa Lumumba waamue nani awe mbunge wa Isimani.
 
Back
Top Bottom