-- Kilichojificha nyuma ya pazia katika hili: Hoteli nyingi zenye hadhi ya kitalii jijini Nairobi zinamilikiwa na Kampuni za KIjerumani na Kiisrael sasa wegeni wengi wanafikia hoteli hizo wakidanganywa kuwa Tanzania hamna miundo mbinu bora ikiwemo hoteli na barabara viwanja vya ndege.
-- Ujenzi huu wa barabara utaendana na ujenzi wa hotels na viwanja vya ndege vya kisasa, kwa mantiki hii, hii ni threat kwa mahotel haya makubwa pale Nairobi kwani italazimika watalii waje moja kwa moja Tanzania.
-- Wakenya kwa kudhaminiwa na hayo mataifa ya nje wanajidai kupinga ujenzi huo wa barabara wakati wenyewe barabara ya lami ninakatiza mbuga ya masai mara.
-- Hata mlima Kilimanjaro wanautangaza kama ni wao, watalii wengi wa kuja mlima KIlimanjaro wanafikia Nairobi, hela kubwa wanaacha kule hapa kwetu wanakuja kumalizia chenchi, hata pembezoni mwa barabara ya Namanga kwenda Nairobi kuna shule nyingi, mahospitali, maduka na hata kile chuo kikuu cha waislam vyote vinaitwa kilimanjaro kuonyesha kwamba ni mlima wao
-- Kuna chama fulani cha siasa hapa nchini kishapata fedha kutoka Ujerumani ili kutetea kutojengwa kwa barabara hiyo ya Musoma - Arusha, hakuna uzalendo ulafi na uchu wa madaraka tu!
-- Tunapaswa kuwa wazalendo kwa kuipenda nchi yetu, ikijengwa barabara, hoteli nzuri na viwanja vya ndege pato letu litaongezeka, shida tunashabikia hata hatujui kinachendelea nyuma ya pazia.
Karibuni tujenge uzalendo!