informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), leo Julai 20, 2024 kimeendesha mdahalo wa wagombea urais wa chama hicho pamoja na wagombea wa Chama cha Mawakili Vijana (TYL).
Katika mdahalo huo ambao umeendeshwa na Mwandishi wa Habari wa muda mrefu, Jenerali Ulimwengu, wagombea wamepata fursa ya kunadi sera zao licha ya maudhurio ya wafuatiliaji kwenye ukumbi wa Wakili house kutokuwa ya kulidhisha.
Kufuatia changamoto hiyo mgombea urais wa TYL, Wakili Denis Bwana amesema kuwa uchache wa maudhurio kwenye mjadala huo ni matokeo ya mwenendo wa TLS kwa siku za hivi karibuni, amesema kuwa cha hicho kwa siku za karibuni kimeonekana kusuasua kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kukemea baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki kwenye jamii, kupigania haki za wanachama wanapopata changamoto zinazohitaji utetezi na kushindwa kuwa na sauti kuishauri Serikali kwenye baadhi ya mambo.
Wakili huyo amedai kuwa taasisi nyingi zisizo za kiserikali pamoja na wadau wengine wasio na nguvu kubwa wamekuwa wakujitokeza wazi kukemea mara kwa mara vitendo visivyo vya haki ambayo vimekuwa vikitokea kwenye jamii, lakini amedai kuwa TLS ambayo ni taasisi kubwa ambayo msingi wa kuundwa kwake umepitia Bungeni imeshindwa kusimama kidete kuonesha msimamo wake.
Anadai kuwa kauli hiyo imechangia kupunguza ushawishi wa TLS, huku akisema kuwa hiyo ndio sababu ambayo imechangia watu kushindwa kushiriki moja kwa moja mdahalo kama ilivyozoeleka. Kufuatia hali hiyo amesema zinahitajika jitahada kwa kupata viongozi bora ambao watarejesha ushawishi na desturi ya chama hicho.
Aidha mgombea Urais wa TLS, Wakili Revocatus Rubigili Kuuli akizungumza katika mdahalo huo amesema kuwa Chama hicho kimekosa makali ya kukemea masuala ambayo yanaenda kinyume na Sheria pamoja na haki.
"Kuna wasiwasi kwamba Chama hiki siku hizi kimekuwa legevu, lakini ni wajibu wetu kuhakikisha chama chetu kinarudi kuwa na nguvu, na namna pekee ya kufanya ni kuhakikisha tunatmiza malengo ya Chama hiki kuanzishwa"amesema
Lakini amesema kuwa ni vigumu kuwa na Chama chenye nguvu kama huna Watu kwenye Chama hicho ambao wanaweza kutoka hadharani kukemea kwa sauti kuu vitendo vinavyokiuka haki na kuvunja sheria
Ambapo ametolea mfano "Nilisikia juzi kauli za kiongozi mmoja mkubwa anasema uchaguzi sio lazima Mtu ashinde kwa kula. Ni wajibu wetu kama wanachama kuona namna ya kukemea matendo kama haya kwa sababu ni kauli hatari kwa Nchi inayoendeshwa kwa Demokrasia
Pia wagombea wengine katika nafasi hiyo nao wanakili kupungua kwa makali ya chama hicho huku wakiomba ridhaa kuwa wakichaguliwa kupitia mikakati mbalimbali watarejesha makali ya chama hivyo kutokana na misingi yake
Itakumbukwa baadhi ya masuala muhimu ambayo yamebainishwa kama wajibu wa TLS ni pamoja na kulinda hadhi na taaluma ya Sheria, kushauri Serikali katika mchakato wa kutunga Sheria, wajibu wa kulinda haki na kutetea haki za wananchi katika jamii.
Wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa TLS ni Wakili Emmanuel Augustino Muga, CAPT. Ibrahim Mbiu Bendera, Wakili Paul Revocatus Kaunda na Wakili Sweetbert Nkuba, pia nafasi wagombea vijana mgombea mwingine ni Wakili Emmanuel Phalet Ukashu ambaye anafanya kinyanganyiro kuwa na wagombea wawili.
Uchaguzi wa Chama hicho unatarajiwa kufanyika August 2, 2024 ukitanguliwa na shughuli nyingine za mkutano mkuu wa mwaka.
Hata hivyo wakati michakato hiyo ikiendelea Mahakama imempa kibali Wakili Boniface Mwambukusi kufungua kesi dhidi ya TLS, hatua hiyo imekuja baada Mwambukusi kuenguliwa kwenye kinyanganyiro.