Hoja ya Makamba kuwa maboresho ya sheria ya uchaguzi yamefanyika ni dhaifu

Hoja ya Makamba kuwa maboresho ya sheria ya uchaguzi yamefanyika ni dhaifu

Mwana kondoo 2025

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2025
Posts
495
Reaction score
580
Nimefuatilia hoja za mbuge wa Chadema covi 19 kuhusu hoja zake kinzani na No reforms No Election kwamba Chadema wamejishauri vibaya kwa kukataa kusaini kanuni na kwamba muda uliobaki wa kufanya mabadiliko yoyote ni mfupi mno kwa Mchakato wa kibunge.

Nadhani ameshindwa kujua sababu kubwa wananchi na viongozi wa dini kudai kwa nguvu maboresho yafanyike ya msingi kwenye katiba ili kuruhusu uchaguzi huru na wa haki. Majaribio ya mabadiliko ya sheria hiyo yameonyesha mapungufu makubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na hapo ndipo matumaini ya wananchi yalipo fail.

Makosa yale yale ya uchaguzi wa 2019, 2020 yalijirudia je impact ya mabadiliko ya sheria hizo ni nini? Msimamo wa No reform No Election unaanzia hapo. Kama yote hayo yalifanyika kuiokomoa Chadema au upinzani, hatua hiyo haitafika mbali sana wananchi wameelewa na wanayaona kwa macho. Wacha tuone mwisho wake.
 
Back
Top Bottom