MwajabuOmary
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 384
- 418
Suala hili limekua likikejeliwa na ccm bila kuja na hoja zenye mashiko.
Hoja zangu ni hizi:-
1. Kwa upande wangu mimi, nikiangalia kwa upande wa vyama vya upinzani nabaini kwamba ni kichaa peke yake ndio anaweza kushiriki uchaguzi wa October, 2025 akiwa anajua kwamba asilimia 85 ya wagombea wake wataenguliwa hata kabla ya kampeni kuanza.
2. Ni kichaa peke yake anaeweza kuweka wagombea wake ambao wanaweza kuuliwa na watu waliojificha katika mwavuli wa watu wasiojulikana.
3. Ni kichaa peke yake anaeweza kuweka wagombea ambao wakati wa kurudisha fomu Mkurugenzi anayo mamlaka ya kupokea au kutopokea fomu tena kwa utashi wake na bila kuchukuliwa hatua zozote na badala yake wanapandishwa vyeo.
4. Ni kichaa peke yake anaeweza kuweka wagombea ambao anajua kabisa wakati wa kurudisha fomu, wagombea hao wanaweza kutekwa na kupotezwa misituni
5. Ni kichaa peke yake anaweza kuingia katika uchaguzi wa October 2025 akiamini kuwa mawakala wake hawatapewa barua za uwakala kwa wakati.
6. Ni kichaa peke yake anaeweza kushiriki uchaguzi huo akiamini kwamba kura zitaanza kupigwa asubuhi na mapema kabla ya wakala wake kufika.
Ni mjinga peke yake anaeweza kushiriki uchaguzi huo huku akijua dola ipo upande wa pili kusaidia.
7. Ni mwendawazimu pekee yake anaeweza kushiriki uchaguzi huo huku akijua kutangazwa mshindi haijalishi umepata kura kiasi gani bali kutangazwa mshindi kunategemea unatoka chama gani
8. Ni mjinga pekee ndio anaeweza kushiriki uchaguzi huo huku akijua kwamba TUME haina tawimu sahihi za wapiga kura.
9. Unakwendaje kwenye uchaguzi ambapo tayali vyama vingine vimekwishaanza kampeni za wazi wazi mwaka mmoja kabla ya kipindi cha kampeni kuanza na hakuna wa kukemea.
10. Ni mjinga peke yake anaeweza kusimamisha wagombea ambao wakati wa kurudisha fomu watakuta ofisi ya Mkurugenzi/msimamizi wa uchaguzi itakutwa imefungwa na ni nyakati za saa za kazi.
Kwa hayo machache tu japo na mengine mengi tu yapo unaingia kwenye uchaguzi ILI IWEJE.
VYAMA VYA UPINZANI MJITAFAKARI.
KWA UPANDE WANGU " NO REFORM NO KWENDA KUPIGA KURA"
NAWASILISHA