Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Polepole: Moja, Polepole yeye anasema kuwa corona ni ugonjwa uliotengenezwa na big pharma ili yapige pesa. Kuwa mabeberu wanaachana na kuvamia nchi kuiba mafuta na sasa wanatengeneza magonjwa ili kupiga pesa.
Pili, Anasema kuwa kasi ya kirusi kubadilika(ku-mutate) inatia shaka, si ya kawaida.
Tatu, anauliza chanjo hiyo itamkinga kwa muda gani? Akatolea mfano kuwa chanjo zingine hudumu maisha yote ya mtu, je hii inadumu muda gani? Hapo anamaanisha kuwa atahitajika kuinunua mara ngapi?
Gwajima yeye anasema kuwa chanjo zile zina serial number, kuwa ukichanja zinakusajili. Kwamba ipo kama barcode, itafika wakikuwekea detector itasoma iwapo umechanja au haujachanja. Kuna mahali amewahi husisha chanjo hii na habari za 666 na ujio wa mfumo mpya, ndiyo maana anasema kuwa watu waananunua dhahabu kwa wingi ili kujiandaa na mfumo mpya, mfumo ambao pengine pesa za makaratasi zisiwe na thamani.
Pia anahoji kuwa kama ukichanja bado utatakiwa kuvaa barako, kutumia sanitizer, utaugua na utaambukiza wengine, ya nini kuchanja?
Amewahi kusema kuwa chanjo ya mRNA inabadilisha watu na kuwafanya mazombie, hivyo akashauri kuwa wanajeshi wasichanjwe.
Kifupi hizi ndizo hoja za hawa wabunge wawili walio mbele kupinga uchanjaji.
Mi kwa maoni yangu ni kuwa hawa jamaa hawana hoja za msingi bali ni Conspiracy theorist tu.